Habari za hivi Punde

WAAJIRI WATAKIWA KUACHA KUPOKEA RUSHWA KWA LENGO LA KUMPITISHA MFANYAKAZI BORA SIKU YA MEIMOSI



WAAJIRI wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani hapa wametakiwa kuacha kupokea rushwa na kupendelea pindi wanapoteuwa wafanyakazi bora ambao wanastaili kupewa zawadi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya sikukuu za wafanyakazi Duniani Meimosi

Akizungumza katika kikao cha wadau wa sherehe za Meimosi juzi mjini shinyanga mkuu wa mkoa Shinyanga Ally Rufunga, wakati wadau hao wakijadili mikakati ya kufanikisha maadalizi ya sherehe hizo alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya waajiri kupokea Rushwa na kuteuwa wafanya kazi wasio na vigezo.


Rufunga alisema sherehe za Meimosi ziliwekwa kwa madhumuni ya kuwapongeza  wafanyakazi wanaofanya vizuri kwa kuwapa zawadi mbalimbali pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi ambao ni wazembe  ili kuleta chachu ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi

“Muajiri unapopokea Rushwa au kupendelea kuteuwa wafanyakazi wasio staili kuzawadiwa katika sikukuu za Meimosi, utawavunja moyo wafanya kazi wanaojituma na hivyo kufanya utendaji kazi kwa wafanya kazi wako kushuka kiwango “alisema Rufunga

Naye mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoani Shinyanga (TUKTA) Fue Mlindoko aliahidi kuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha suala zima la Rushwa wala upendeleo halishiki nafasi katika sherehe za mwaka huu (2014) kama ilivyotokea mwaka jana katika manispaa ya Shinyanga ambapo zoezi la utoaji zawadi  lilisitishwa

‘Sherehe za Meimosi mwaka jana katika Halmashauli ya manispaa ya shinyanga kulitawala Rushwa ,upendeleo na kuteuwa wafanyakazi wasio staili kutunzwa zawadi hizo, mfano katika idara ya afya aliyeteuliwa kupokea zawadi ni mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti lakini akachakachuliwa na kupewa muuguzi ‘’alieleza Mlindoko na kuongeza kuwa

‘’Kutokana na kugundulika kwa kitendo hicho tuliamua kutoa taarifa kwa mgeni rasimi ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wetu Ally Rufunga kusitisha kutoa zawadi kwa baadhi ya wafanyakazi wa manispaa ya shinyanga mpaka hapo uchunguzi utakapo kamilika nani aliyekuwa anastaili kupewa zawadi hizo, hivyo kwa mwaka huu tunaomba isijitokeze tena”

 Hata hivyo Mlindoko alizitaja zawadi zitakazo tolewa kwa wafanyakazi bora katika siku hiyo ya madhimisho ya sikukuu za Meimosi mkoani humo ambapo katika sekta Binafsi zawadi ni shilingi 300,000,sekta ya Umma shilingi 500,000 ,Migodi ya kati shilingi 500,000 , Migodi mikubwa ni shilingi 1,000,000

Pia wadau hao walijadili mambo mbalimbali yatakayo fanikisha kukamilisha sherehe hizo ambapo waliziingiza taasisi zingine zikiwemo za kifedha ambazo hazikuwemo kwenye bajeti, huku kikitarajiwa kukusanywa kiasi cha shilingi milioni 90.6 fedha ambayo itakusanywa kutoka kwa wadau hao ambazo ndizo zitakazo fanikisha sikukuu hiyo.




0 Response to "WAAJIRI WATAKIWA KUACHA KUPOKEA RUSHWA KWA LENGO LA KUMPITISHA MFANYAKAZI BORA SIKU YA MEIMOSI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.