Habari za hivi Punde

RC-SIMIYU AMEWATAKA WAKUU WA WILAYA WAPYA KUKOMESHA MAHAKAMA ZA KIMILA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amewataka wakuu wa wilaya wapya kuhakikisha wanakomesha  mahakama za kimila maarufu kama  Ndagashida  ambazo zimekuwa zikitoa adhabu kwa watumishi wa umma  wasio na hatia hali inayopelekea kutokea kwa  mauaji , vilema vya maisha sambamba na kuwafirisi mali zao.
 
Akitoa wito huo jana wakati wa kuapishwa  wakuu hao  ,Mtaka alieleza kuwa  ni muhimu kwa wakuu hao kuzingatia suala hilo  katika wilaya zao kwani  limekuwa likionekana  kuwa ni kikwazo kwa watumishi wa umma ambao hawakubaliani na mila zisizokuwa za kwao.

SHINYANGA BADO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADAWATI 9,545


MWENYEKITI MPYA WA TIMU YA STEND UNITED ATAKA USHIRIKIANO,ATAJA WACHEZAJI WALIOACHWA KUWA WAKO HURU

MWENYEKITI wa  timu ya Stend United iliyopo mkoani Shinyanga  Ellyson Maeja   ametaka ushirikiano   wa kuinyanyua timu  nakuondoa tofauti zilizokuwepo kipindi cha nyuma   huku akitangaza wachezaji watakao achwa msimu ujao. 

Wachezaji walioachwa na wako huru ni Haruna Chanongo,Nassoro Choro,Rajab Zahir,Hassan Self, Philipo Metusela huku waliomaliza mkataba wao ni  Salum Kamana  na Elius Maturi.

MIKAKATI YA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WILAYANI SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  ameeleza mikakati dhidi ya kupinga mimba  na ndoa za utotoni  ili kufanikisha   kuwakamata waliosababisha ni wasichana  waliobainika kuwa na mimba kukataa  kusema ukweli  watalazimika  kuwekwa ndani.
Mkuu wa wilaya huyo alisema  hayo  jana alipokuwa mgeni rasmi  mbele ya wadau wa maendeleo katika mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni kupitia shirika la Agape  ikiwa utekelezaji wake kwenye kata nne za Samuye,Lyabusalu,Iselamagazi

UWT WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI WAKIWA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU.

Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini akitoa  akijitolea kuchangia damu.

Wakwanza  kushoto ni  mwenyekiti wa UWT  Hellen David akiwa na wajumbe wa UWT wakijitolea uchangiaji damu  lengo kuokoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na ukosefu wa damu.

Wakipewa maelekezo na kufarijiwa.

Wajumbe wa UWT wakijiandaa kwa uchangiaji damu  hapa wanajiandikisha tayari kwa kupata vipimo.

Katibu wa UWT  Grace Haule akiendelea  kuchangia damu .

Wajumbe  wa UWT wakiandaliwa kisaikolojia.

WATU 40,364 WAMEPIMWA,1,871 WAMEBAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VVU

Kati ya  watu 40,364 waliojitokeza kupima  afya kwa hiari katika halmashauri Msalala  mkoani Shinyanga   1,871 wamekutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Mratibu wa ukimwi wa halmashauri  hiyo Jackson Faustine  anasema kuwa  watu hao walijitokeza kupima afya kati ya Januari hadi Novemba  2015.

DC SHINYANGA ATOA AGIZO MHANDISI WA MANISPAA KUWEKWA RUMANDE

MKUU wa  wilaya  ya  Shinyanga  Josephine  Matiro  ametoa  amri  ya kumuweka  ndani  mhandisi  wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga  Saimon  Ngagani ,  kutokana  na kukaidi  agizo lake  la kufanya  maandalizi  mapema  ya  shughuli  za  kuchimbia  mapipa  ya  kuweka  taka  nyepesi  katika  maeneo  mbalimbali  ya manispaa  hiyo. 

Akizungumza na  baadhi ya   wananchi  katika  stendi  ya  mabasi  ya zamani  wakati wa kuweka mapipa hayo ,mkuu wa wilaya alisema zoezi  hilo lilitakiwa lifanyike saa  1.30 asubuhi lakini wamelazimika kufanya saa 3.30  kutokana  na uzembe uliofanywa na injinia  ambaye alipewa  kazi ya  kuandaa  kokoto  na  mchanga mapema matokeo  yake  hakufanya  hivyo.

WATOTO KWENYE KITUO CHA BUHANGIJA WAPATA MSAADA.

Watoto wenye ulemavu mbalimbali katika kituo cha Buhangija manispaa ya Shinyanga wakisubiri kupewa msaada wa nguo na vyakula  siku ya pasaka.

Watoto wakiendelea kusubiri msaada.


Familia ya  Mwalongo ikijitambulisha tayari kwa kutoa msaada siku ya Pasaka

Mbuzi aliyetolewa na familia ya Anna na Josephat Mwalongo siku ya Pasaka katika kituo cha Buhangija.

MFUMODUME WAWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUKUZA UCHUMI

WANAWAKE  nchini wameelzwa kuwa mfumo dume ndio unaowakwamisha kuweza kupata mikopo katika taasisi za fedha kwa kukosa dhamana
 
Licha ya kuwa waaminifu zaidi kuliko wanaume wamekuwa kwakipata vikwazo mbalimbali vyakushindwa kuendesha biashara`zao na pindi  wanapohitajika kutoa dhamana kwaajili ya mikopo wengi wao hushindwa sababu ya  mfumodume

KUKOSEKANA KWA MASHINE ZA CD4 ZAWATESA WENYE MAAMBUKIZI YA VVU.

VITUO vya kutolea huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi mkoani Shinyanga vinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa mashine za  kupimia CD4 hali inayosababisha hofu kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali   (ARV).

MENO YA TEMBO YAKAMATWA HUKU WATU TISA WAKISHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

WATU wadhanwao ni  majangili katika pori la akiba Maswa waliofanya tukio la  kutungua
helkopita ya kampuni ya Mwimba Holding Limited na kusababisha kifo cha
Rubani,  Rodgers Charvis  raia wa Uingeleza ambaye alikuwa
akitekelezamajikumu yake jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata
wahusika 9 pamoja na bunduki 29  ikiwemo  meno ya tembo matatu.

Akiongea  jana na waandishi wa habari mkoani Simiyu, Kamanda wa polisi
mkoani hapa Lazaro Mambosasa alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 9 ambao walihusika na tukio la kuangusha
helkopita pamoja na kusababisha kifo cha Rubani wa ndege hiyo.

WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MAHAKAMA ZA MWANZO




 WATUMISHI  wa idara ya mahakama mkoani Shinyanga wametolewa hofu ya kuhakikisha wananchi  wanashirikishwa ili kuweza  kuboresha miundombinu ya majengo  kama wafanyavyo kwenye sekta zingine.

Hayo yamesemwa   na mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga   kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyka kwenye viwanja vya mahaka mkazi wilaya nakuhusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA ATAKA WANANCHI KUFAHAMU TARATIBU NA SHERIA DHIDI YA VYOMBO VYENYE DHAMANA


MKUU wa wilaya ya Shinyanga  Josephine Matiro  ametoa wito kwa wananchi  kushiriki utolewaji wa elimu  katika vyombo vinavyosimamia haki na sheria  ili kuweza kujua pindi haki inapotendeka nakuondoa manung’uniko yanayotokea mara kwa mara katika vyombo hivyo.
KARENY. Powered by Blogger.