Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka
amewataka wakuu wa wilaya wapya kuhakikisha wanakomesha mahakama za kimila maarufu kama Ndagashida
ambazo zimekuwa zikitoa adhabu kwa watumishi wa umma wasio na hatia hali inayopelekea kutokea kwa mauaji , vilema vya maisha sambamba na
kuwafirisi mali zao.
Akitoa wito huo jana wakati wa
kuapishwa wakuu hao ,Mtaka alieleza kuwa ni muhimu kwa wakuu hao kuzingatia suala
hilo katika wilaya zao kwani limekuwa likionekana kuwa ni kikwazo kwa watumishi wa umma ambao
hawakubaliani na mila zisizokuwa za kwao.
Amesema ni dhahiri kwamba ili mkoa uendelee
kuwa na watumishi waishio kwa amani , ni lazima kukomesha Ndagashida ili watu
na watumishi waendelee kufurahia kuishi Mkoani Simiyu.
Sambamba na hilo Mtaka pia amewasihi
wakuu hao wa wilaya kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ambao
utaenda pamoja na upandaji wa miti ili kunusuru mkoa kuangamia na kuwa jangwa.
Ameeleza kuwa hali ya mazingira si zuri na kwamba Mkoa unakaribia kugeuka
kuwa jangwa ambapo inaweza kusababisha
maisha ya wakazi wa Mkoa kuwa magumu.
“hali ya utunzaji wa mazingira si nzuri…hivyo ninawaomba waheshimiwa wakuu
wa wilaya kuhamasisha watu kupanda miti…hasa kwa kuanzia katika taasisi kwani
itasaidia kuondokana na ukame uliotawala ndani ya Mkoa.
Aidha
mara baada ya kuapishwa mkuu wa
wilaya ya Meatu Joseph Chilongani amesema kipaumbele kimojawapo ambacho
ataanza kukifanyia kazi kabla ya
shule za msingi kufunguliwa hapo julai 11, mwaka huu ni kufanya uhakiki
wa wanafunzi wote ambao wako katika mpango wa elimu bure kama inavyoelekeza na
serikali ya awamu ya tano.
Chilongola amesema ni
lazimaashughulikie suala la uhakiki wa hao wanafunzi ili isije kuwa kuna
wanafunzi hewa ambao hela zao zinatumika na wajanga ndani ya idara ya elimu.
Sambamba na hilo ameomba ushirikiano
wa karibu kutoka mkurugenzi ,wakuu wa wilaya na watumishi ili waweze kufanya
kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Jumla ya wakuu wa wilaya watano wa wilaya
tano za mkoa wa Simiyu wameweza kuapisha leo na mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka ambao
ni Joseph Chilongani (Wilaya ya Meatu ,) Tano Mwera (busega), Seif
Shekalaghe(Maswa) Benson Kilangi(Itilima)na
Festo Kiswaga (Bariadi)
|
0 Response to "RC-SIMIYU AMEWATAKA WAKUU WA WILAYA WAPYA KUKOMESHA MAHAKAMA ZA KIMILA"
Post a Comment