MADIWANI wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu
wamemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Paschal Mabiti kutekeleza agizo la Raisi Jakaya
Kikwete alilotoa wakati wa ziara yake mkoani hapa, la kupandisha kiwango
hospitali ya Wilaya ya Bariadi kuwa hospitali ya Mkoa.
Mbali na Mkuu huyo wa Mkoa kutakiwa kuhakikisha
anatekeleza agizo hilo la Rais , madiwani hao walishangazwa na kitendo cha
Kiongozi huyo wakati wa kikao cha ushauri cha Mkoa kilichokaa hivi karibuni
kukataa kutekeleza agizo hilo kwa madai kuwa
Rais hakuagiza kupandishwa
kiwango hospitali hiyo.
Akiongea wakati wa kufunga kikao cha Baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo kilichofanyika jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Robert Lweyo, alimtaka Mkurugenzi Erika Msika kuandika barua kwenda kwa mkuu wa
mkoa ya mkutaka kutekeleza agizo hilo.
Alisema kuwa wakati wa majumuhisho ya ziara ya Rais Mkoani
hapa katika wilaya ya Busega, uongozi wa mkoa uliagizwa kufanya utaratibu wa
kuhakikisha hospitali hiyo inapandishwa kiwango na kuwa hospitali ya mkoa
kutokana kwa sasa kukabiliwa na
msongamano wa wagonjwa.
Alisema kuwa mara baada ya mkoa wa simiyu kuanzishwa, na
makao makuu yake kuletwa wilayani bariadi, Hospitali hiyo imekuwa ikitumiwa na
watu wengi kutoka katika kila wilaya kuleta wagonjwa wao kutokana na kuitwa
hospitali ya mkoa.
“Raisi Kikwete aligiza kupandishwa kwa hospitali ya wilaya
ya Bariadi, lakini Mkuu wa Mkoa amepinga agizo hilo, kwa kusema kuwa Raisi
hakuagiza hivyo badala yake aliagiza Halmashauri hiyo isaidiwe na uongozi wa
Mkoa katika kuongeza watumishi, pamoja na madawa ikiwemo fedha za matumizi
kutokana na Halmashauri hiyo kuelemewa na wingi wa wagonjwa”alisema Lweyo.
Alibainisha kuwa uamuzi wa mkuu wa mkoa siyo sahihi, na Rais
hakuagiza hivyo, ambapo walimtaka kurejea hotuba ya Rais wakati wa majumuisho
yake kwenye ziara yake mkoani hapa kwa
kile alichokiongea juu ya hospitali hiyo.
Alisema azimio la Baraza hilo juu ya suala hilo limemtaka
Mkurugenzi kuiandikia barua ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuitaka kurejea hutuba
ya Rais, ikiwa kuhakikisha agizo hilo la kiongozi wan chi linatekelezwa
ipasavyo.
.
0 Response to "MADIWANI HALMASHAURI MJI WA BARIADI WATAKA AGIZO LA RAIS KUTEKELEZWA HOSPITALI YA WILAYA KUWA YA MKOA"
Post a Comment