Habari za hivi Punde

MZAZI ATINGA SHULENI NA BAKORA KISA ATAKA BINTI YAKE AKAELEE MTOTO NYUMBANI.

MZAZI ATINGA SHULENI NA BAKORA KISA  ATAKA  BINTI YAKE AKAELEE MTOTO NYUMBANI.



MZAZI wa Mgreth  Tilu anayesoma  shule ya msingi  Bugimbagu darasa la saba  iliyopo kata ya Mwawaza  manispaa ya Shinyanga  alitolewa  darasa na baba yake mzazi  huku akiwa ameshika fimbo  mkononi  kwa kumtaka arudi nyumbani  kwa lengo la kwenda kumlea  mdogo wake.

Mzazi huyo aliyefahamika kwa jina la Tilu Bushi alifanya kitendo hicho  katika shule hiyo wakati  muda  wa kufanya  mtihani  wa mocko  ukiendeleo ndipo aliamua  uamuzi wa kumfuata shule  na kusababisha  mwanafunzi  huyo  kushindwa  kufanya mtihani wake.

WAEKEZAJI MANISPAA YA SHINYANGA WALALAMIKIWA.

WAEKEZAJI MANISPAA YA  SHINYANGA  WALALAMIKIWA.


WAWEKEZAJI   manispaa ya Shinyanga wamelalamikiwa kutotekeleza  matakwa waliyokubaliana mara baada ya kuwa wameomba kuwekeza  maeneo mbalimbali na kuchukua ardhi kubwa jambo ambalo limefanya kuzua migogoro mikubwa kwenye maeneo  ya wakazi hao.

Kitu kilichobainika mara baada ya kukaa  kamati ya miundombinu ya madiwani,ilijionea  mwekezaji katika eneo la N’helegani alichukua ekari  zaidi ya 100 huku akiahidi kujenga  madarasa  kwaajili ya kuanzisha shule ya wakulima , kuajiri  wafanyakazi wazawa huku wawekezaji wengine wakiahidi pia kuweka  kiwanda cha kusindika nyama   mambo ambayo yamekwenda kinyume.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa kamati ya miundombinu  ambaye pia ni diwani wa kata ya Chamaguha  Morice  Mghin   kwenye  baraza la madiwani   lililofanyika  katika ukumbi wa mkoa huku akieleza kuwa  kutokana na makubaliano hakuna madarasa yaliyojenga wala shule, hakuna ajira iliyotolewa  matokeao yake  wananunua  marobota na kutenge nyuzi kwa kusafirisha nje ya nchi.

“Jambo lingine  wawekezaji  kampuni ya  wachina eneo la ibadakuli  tulikubaliana  kiwanda cha kusindika nyama  wanachokifanya wanasindika ngozi  pekee tena   wameajiri vijana  wanaowatumia  bila vitendea kazi mikono yao imeanza kuchumbuka  hivyo wanaonekana  kutotii sheria ya Osha,huku mwekezaji  kampuni ya jambo  akilalamikiwa kuchukua eneo zaidi tofauti na alivyopimiwa hali ambayo imezua migogoro  kwa wananchi wa eneo hilo  na kiasi cha zaidi ya shilingi  millioni 400 bado hakijalipwa.”alisema Mghini.

Hivyo alitoa ushauri kuwa  suala la wawekezaji  limeonyesha kuwa na ubabaishaji  kila wanapofuatwa hukumbilia  kwa mkuu wa mkoa  utaratibu uwepo  wa  wawekezaji  kupitia kwa wakurugenzi   wanaotoa ardhi   na uwe wa hisa  na sio uanzie mkoani kama ulivyo sasa  ambapo  imeonekana wananchi  kuwakosesha  haki zao za msingi.

Diwani wa kata ya Ibadakuli  Leonard   Richard  alisema kuwa kumekuwepo mgogoro wa ardhi  eneo hilo  kampuni ya jambo  kuchukua eneo zaidi  huku  Siri Yasin  diwani viti maalumu akieleza  kuwa   baadhi ya watumishi wamekuwa wakiegemea upande wa wawekezaji  bila kushirikisha  wananchi jambo ambalo linaonyesha kujidhalilisha  ikiwa wanatakiwa kuanzia uongozi wa vitongoji,vijiji na kata ambapo kunapatikana ukweli sio   kwenda   kwa mwekezaji.

Naye naibu  mstahiki meya  wa manispaa  David Nkulila alisema kuwa  hakuna sheria inayoua sheria   wawekezaji wamekuwa wakienda kinyume  na kuleta ubabaishaji  ikiwa wameonekana dhahiri pindi wanapofuatwa na  maafisa  mbalimbali hujifanya kutofahamu lugha  hasa hawa wachina  na mwisho wa siku humfuata mkuu wa mkoa na kutoa malalamiko yao.

Kaimu mkurugenzi  ambaye pia  ni ofisa ardhi wa manispaa  Dismas  Minja alisema kuwa yanayosemwa ni kweli   ila kinachotakiwa  ni kuanza  ufuatiliaji  wa karibu ili wananchi wanufaike  na ardhi yao, hivyo inatakiwa kuwa macho  na wawekezaji  wa namna hii haiwezekani wanachukua ekari 150 na hakuna kitu chochote kinacho fanyika  kwa wananchi.

Katibu  tawala wilaya.  ya Shinyanga  Boniface  Nchambi alisema kuwa   suala la mgogoro wa ardhi  limekuwa ni changamoto kubwa kwenye maeneo yaliyochukuliwa na wawekezaji  hivyo  uamuzi uliopo  waorosdheshwe   watu wote waliochukuliwa maeneo yao ili kuweza kubaini tatizo liko wapi.


KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA.


Mheshimiwa diwani wa kata ya Chamaguha manispaa ya Shinyanga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya miundombinu  akiwasilisha  taarifa ya kamati yake huku akitoa maelezo ya  wawekezaji wamekuwa hawatekelezi makubaliano kama mikataba yao inavyoeleza.


ZAO LA MTAMA LINALODAIWA KUSHAMBULIWA NA NDEGE AINA YA KWELEA KWELEA

Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu  akiwemo mkurugenzi  wa halmashauri  hiyo  wakikagua  zao la mtama shambani mara baada ya kuripotiwa kutoka kwa wakulima kuwa linaliwa na ndege aina ya kwelea kwelea.

PSPF YATOA ELIMU KWA WAJASILIAMALI SOKO KUU MANISPAA YA SHINYANGA.

PSPF YATOA   ELIMU KWA WAJASILIAMALI   SOKO KUU MANISPAA YA SHINYANGA.



WAJASILIAMALI   wenye kipato kidogo manispaa ya Shinyanga   wametakiwa kujiunga na  mfuko  wa Pensheni kwa watumishi wa Umma ( PSPF) mara baada ya  kutolewa   elimu   ikiwa imebainika  kuwa asilimia kubwa bado hawajajiunga na  mfuko huo kwa dhana iliyojengeka  kuwa ni kwaajili ya watumishi pekee.

Inatakiwa wajasiliamali waone  umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini na kuweza kunufaika nayo  kwa kutunza fedha ambazo zitawasaidia katika maisha ya sasa nayabaadae.

Akitoa elimu hiyo kwa wajasiliamali wa soko kuu la mjini Shinyanga  mjumbe wa Bodi wa mfuko huo kutoka Jijini Dar es salaam  Clement  Mswanyama alisema asilimia kubwa ya wajasiliamali hapa nchini hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwafanya  kukosa fedha za kuwasaidia katika maisha hasa pale wanapopatwa na matatizo.

 “ Watu wanaofanya shughuli zenye kipato kidogo  asilimia kubwa wamekuwa wakisahaurika kupewa fursa ya kujiunga na mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii na kuwathamini watumishi ambao wameajiriwa hali ambayo huwajengea watu hao mazingira ya kuwa na maisha magumu”alisema .

MWENDESHA DALADALA YA BAISKELI ATUHUMIWA KWA UBAKAJI WA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI NA KUMTOBOA MACHO

MWENDESHA DALADALA  YA BAISKELI ATUHUMIWA KWA UBAKAJI WA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI NA KUMTOBOA MACHO
KIJANA   Omary  Simon (30) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga  kwa tuhuma ya kumbaka   mwanafunzi wa darasa la pili (9)  anayesoma katika  shule ya Msingi Kitangili Manispaa ya Shinyanga kisha kumtoboa macho  kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumuacha porini akisota kwa muda wa siku mbili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga  Evarist  Mangalla alisema tukio hilo lilitokea Aprili 20, mwaka huu majira ya saa 10;00 jioni katika kitongoji cha  Bugweto  nje kidogo ya mji  baada ya siku hizo aliokotwa na wanawake wawili.

Kamanda Mangalla alisema siku ya tukio mwanafunzi huyo ambaye nanaishi na Bibi yake Kata ya Ibinzamata alipewa shilingi 500/= na bibi yake kwa ajili ya kupanda Daladala  ya baiskeli kwenda kwa mama yake mkubwa anayeishi kata ya Ngokolo.

WAZAZI WAHIMIZWA KUONA UMUHIMU WA CHANJO KWA WATOTO

WAZAZI WAHIMIZWA KUONA UMUHIMU WA CHANJO KWA WATOTO

WAZAZI  na walezi  wilayani Maswa mkoani Simiyu wamehimizwa kuona umuhimu wa chanjo kwa kuwapeleka watoto  kupata chanzo  mbalimbali  za kuzuia maradhi ya kuhara na Nimonia zinazostahili kupatiwa kwa watoto walio chini ya mwaka mmoja ikiwa zaidi ya watoto 13,000 hawakupatiwa chanjo.

Changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa zoezi hilo ambazo ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu umuhimu na ukamilishaji wa chanjo zote,watotohao  hawakupata au kukamilisha chanjo sabau  ikielezwa ni  ukosefu wa usafiri kwa ajili za kliniki za mkoba za chanjo kwa baadhi ya vituo vya
kutolewa huduma za afya.

Mganga Mkuu wa wilaya  hiyo Dkt  Jonathan Budenu alibainisha hayo katika uzinduzi  wa wiki ya chanjo  uliofanyika katika zahanati ya kijiji cha Malita kata ya Zanzui  na kuhudhuria  na baadhi ya wananchi  hasa akina mama wachache waliojitokeza

WAZAZI NA WALEZI WANASHINDWA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.

WAZAZI NA WALEZI WANASHINDWA KUCHANGIA MIRADI  YA MAENDELEO.
.

BAADHI  ya wazazi  na walezi  manispaa ya Shinyanga  asilimia kubwa wamekuwa  hawapendi kuchangia miradi ya maendeleo  mbalimbali ikiwemo  sekta ya elimu  hali ambayo imeonyesha  katika shule ya sekondari Mazinge kushindwa kuchangia  huduma ya wanafunzi kupata uji na chakula cha mchana.

Ikiwa kila mwanafunzi  inatakiwa achangie kiasi cha shilingi 3000,  hivyo Idadi ya wanafunzi waliotoa michango yao ni 6 pekee kwa shule nzima kati ya  wanafunzi 664 kwa lengo la kupata uji  wawapo shuleni hapo, imeelezwa  wazazi ndio chanzo cha kudhorotesha  kutokupata huduma hiyo ikiwa katika sherehe za harusi wanakuwa mstari wa kwanza  kuchangia.

Diwani wa kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga David Nkulila,ambaye pia ni naibu meya wa manispaa hiyo aliyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo.

kIJANA ACHOMWA KISU NA KUFA KISA ATAKA KUMBAKA MSICHANA.

kIJANA ACHOMWA KISU NA KUFA  KISA ATAKA KUMBAKA MSICHANA.


KIJANA  mmoja (30) aliyejulikana kwa jina la Stephen Philbert ameuawa kwa kuchomwa kisu kichwani na mwanamke  aliyekuwa anamfanyia jaribio la kumbaka  katika eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla alisema tukio hilo limetokea usiku wa Aprili 20,mwaka huu saa tisa usiku ambapo Stephen Philbert mkazi wa Ngokolo alichomwa kisu kichwani wakati akitaka kumbaka mwanamke aitwaye Pili Michael(24).

Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo kamanda Mangalla alisema siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo anayeishi Ngokolo mjini Shinyanga na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka.

WAZAZI NA WALEZI WALAUMIWA KUWATELEKEZA WATOTO WAO KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WALEMAVU

WAZAZI NA WALEZI WALAUMIWA KUWATELEKEZA WATOTO WAO KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO WALEMAVU




WAZAZI  na walezi  waliopeleka watoto wao katika kituo   maalumu cha  kulelea  watoto wenye ulemavu  mbalimbali kilichopo  Buhangija manispaa ya Shinyanga wameombwa kujenga desturi ya kuwatembelea watoto  hao mara kwa mara na sio kukiachia  kituo pekee hali ambayo inawafanya  kukosa haki zao za msingi  kwa kupata malezi bora kama watoto wengine.

Baadhi ya watoto hao tangu waletwe kituoni hapo  hakuna hata mzazi au mlezi mmoja aliyekuja katika kituo hicho kumuona mwanaye  na kumjulia hali  jambo ambalo linaonywesha kuwa watoto tayari wamekosa imani na wazazi wao kwa kutowaona muda mrefu.

SHULE INACHANGAMOTO NYINGI WALIMU WALALA MADARASANI,SHULE HAINA VYOO WALA MADAWATI

 SHULE INACHANGAMOTO NYINGI WALIMU WALALA MADARASANI,SHULE HAINA VYOO WALA MADAWATI




SHULE  ya msingi Mwamashimba  katika kijiji  hicho  kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vyoo,madawati na nyumba za walimu hali inayosababisha baadhi ya walimu kuishi kwenye vyumba vya madarasa.

Shule hiyo yenye muonekano tofauti  na kuwa hali halisi ya kuwepo kwa wanafunzi na walimu   waandishi wa habari  walitembelea shule hiyo  kutaka kufahamu  wanafunzi wanapataje elimu kupitia vyumba hivyo na mazingira yaliyopo huku wakihoji baadhi ya viongozi.

TUME YA WATU 18 IMEUNDWA KUCHUNGUZA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

TUME YA WATU 18 IMEUNDWA KUCHUNGUZA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


TUME  iliyoundwa ya watu kumi na nane na wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwemo  mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nasoro Rufunga na mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwasa kuwa baini na kuwakamata watu waliohusika na mauaji ya watu watano katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea mpakani mwa mikoa hiyo miwili.

Mwenyekiti  wa  chama cha Mapinduzi  mkoani Shinyanga Khamis Mgeja  aliyasema hayo  kwenye kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika wilayani Kishapu wakati wa ziara yake wilayani humo mara baada ya kusomewa taarifa ya mauji hayo na mkuu wa wilaya ya hiyo Wilson  Nkhambaku kuwa mapigano hayo yalitokea tarehe 29 marchi mwaka huu katika kijiji cha magogo wilayani kishapu mkoani shinyanga mpakani na wilaya ya Igunga mkoani Tabora na kusababisha mauaji wakati wakigombania Ardhi.

JAMII IMETAKIWA KUJIOMBEA NA KULIOMBEA TAIFA HASA KIPINDI HIKI CHA MCHAKATO WA KUUNDA KATIBA MPYA.

JAMII IMETAKIWA KUJIOMBEA NA KULIOMBEA TAIFA HASA KIPINDI HIKI CHA MCHAKATO WA KUUNDA KATIBA MPYA.



JAMII mkoani Shinyanga imetakiwa kujiombea  na kuliombea taifa katika mchakato huu wa  kuunda katiba mpya  kwenye msimu huu wa kumalizika  kwa mateso ya yesu kristo aliyejitoa  na kusulubiwa  msalabani kwaajili ya dhambi za wanadamu huku akiwataka kutenda yaliyo mema duniani.

Hayo  yalisemwa  jana  na  mchungaji  peter   Msengi   wa kanisa la Moravian lililopo Ngokolo kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga  katika ibada ya  siku ya ijumaa kuu mbele ya waumini wa kanisa hilo huku ikiwemo imani kutoka kwenye  kitabu cha maandiko kuwa  binadamu hana kosa  na kufikia hatua ya kukiri mwenyewe.

JAMII YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KUBAINI WAHAMIAJI HARAMU.

JAMII YATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KUBAINI WAHAMIAJI HARAMU.




JAMII imetakiwa kutoa ushirikiano katika kuwabaini wahamiaji haramu ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,hatua itakayosaidia kupata viongozi ambao ni wazalendo wenye uchungu na nchi yao badala  ya kuchagua mtu bila kujua historia yake matokeo yake uzalendo unakosekana.


Hayo yalibainishwa na Naibu Kamishina wa uhamiaji  wilaya ya shinyanga Salumu Farahani katika ofisi za uhamiaji mkoani shinyanga ambapo alisema kuwa kumekuwepo na wimbi la wahamiaji, ambao wamekuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria na jamii kushindwa kuwafichua.

ZAHANATI YA KIJIJI CHA SINGITA KATA YA USANDA YAKABILIWA NA UHABA WA MAJI,MAABARA NA DAWA.

ZAHANATI YA KIJIJI CHA SINGITA KATA YA USANDA YAKABILIWA NA UHABA WA MAJI,MAABARA NA DAWA.


ZAHANATI ya kijiji cha  Singita kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali ambayo inayowalazimu mama  wanaokwenda kujifungua  kununua maji dumu la lita  ishirini shilingi mia mbili ikiwemo ukosefu wa maabara.

Wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea zahanati iliyopo kijijini hapo,walisema kuwa  wanapokwenda kujifungua  hulazimika kununua maji kwaajili ya kufulia nguo na kuoga jambo ambalo limekuwa ni changamoto  kwao yakuwafanya kutumia gharama kubwa  huku kipato chao ni kidogo.

Walisema kuwa Zahanati hiyo haina huduma ya maji hulazimika kununua dumu moja la lita ishirini shilingi miambili ambayo ndiyo changamoto kubwa  ikiwemo ukosefu  wa dawa mara kwa mara,maabara  na baadhiya ya vifaa tiba ikiwa hulazimika  kufuata vipimo vingine katika hospitali ya serikali ya  mkoa au binafsi zilizoko mjini.

WAZIRI MKUCHIKA ASEMA RUSHWA KATIKA HALMASHAURI BADO NI KITENDAWILI

WAZIRI   MKUCHIKA  ASEMA   RUSHWA KATIKA HALMASHAURI BADO  NI KITENDAWILI
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais  Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema rushwa katika halmshauri nchini, bado ni kitendawili, kutokana na kuongezeka kila mara licha ya serikali kupitia Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) kukabiliana nayo.

Alisema mbali na mapambano hayo halmashauri nyingi nchini suala la  matumizi bora ya fedha za serikali bado halingatiwi, na kusababisha kuongezeka kwa rushwa kwa watumishi wake hasa wakuu wa idara ambao ndiyo wahusika wakuu katika matumizi ya fedha hizo.

Waziri Mkuchika alisema hayo jana wakati akiongea na wajumbe wa kikao cha ushauri cha Mkoa wa Simiyu (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Barideco ulioko Mjini Bariadi, kikao kilichokuwa maalumu cha kupitisha bajeti ya mwaka 2014/15.

WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA WAUDHI BAADHI YA WANANCHI.

 WAJUMBE  WA BUNGE  MAALUMU LA KATIBA WAUDHI  BAADHI YA WANANCHI.



HATUA iliyofikia kwa bunge  maalumu la katiba  limewafanya baadhi  ya  wananchi  wa kijiji cha Mwamashimba kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga  kusikitishwa  na vitendo vya baadhi ya wajumbe wa bunge hilo  kutoa maneno machafu yenye  kudhihaki waasisi wa taifa ,wakidai  kuwa watu hao  wanaokashfu viongozi huenda wana ugonjwa wa kansa ya ubongo.

Baada ya kuhojiwa na  waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho,wananchi hao walisema vitendo vya kuwakosea heshima waasisi wa taifa akiwemo baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hayati Amani Abeid Karume siyo vya kiungwana kwani viongozi hao ndiyo waliolifikisha taifa hapa lilipo.

WANAFUNZI 47 WASHINDWA KURIPOTI KUANZA KIDATO CHA KWANZA.

WANAFUNZI   47  WASHINDWA KURIPOTI   KUANZA KIDATO CHA  KWANZA.


WANAFUNZI  47  waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2013/14  katika shule za sekondari  zilizopo manispaa ya Shinyanga hawajaripoti shule  na kutojulikana walipo.

Hayo yalisemwa na ofisa elimu wa shule ya sekondari  manispaa ya Shinyanga  Daud Mkumbwa  kwenye kikao  kilichojumuisha viongozi wa sungusungu kutoka wilaya za manispaa,shinyanga na Kishapu kwaajili ya kujadili ajenda  ya utoro mashuleni.

Mkubwa alisema kuwa  kumekuwepo na wimbi la utoro mashuleni ikiwemo wanafunzi wa kike kupata mimba, kutohuduria masomo mara kwa mara  ikiwa  wanafunzi wakiume ni 21 na wakike 26 hawajaripoti  shule mpaka sasa,ambapo aliwataka viongozi hao kushirikiana ili kuweza kuondoa changamoto hiyo.

JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU MBILI

 JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA  PEMBE ZA NDOVU MBILI


MAHAKAMA  ya wialya ya Bariadi Mkoani Simiyu imemuhukumu Mkazi wa mmoja liyejulikana kwa jina la Maganzo Zelamoshi mkazi wa kijiji cha Zangho kata ya Mwabali wilayani humo, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali bila ya kibali.

 Akimsomea shtaka linalomkabili mtuhumiwa kabla ya hukumu hiyo Mwendesha mashtaka wa TANAPA Eliasi Benjamini, alisema kuwa mnamo tarehe 21 octoba 2013 mtuhumiwa alikutwa akiwa na pembe 2 za ndovu.

KUNDI LA TEMBO LAVAMIA MAKAZI YA WATU NA KULA MAZAO YALIYOKUWA MASHAMBANI NA VYAKULA WALIVYOHIFADHI

KUNDI LA TEMBO LAVAMIA MAKAZI YA WATU  NA KULA MAZAO  YALIYOKUWA MASHAMBANI  NA VYAKULA WALIVYOHIFADHI




KUNDI  kubwa la Tembo  zaidi ya 40  kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  wamevamia katika makazi ya watu na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao pamoja na vyakula vilivyokuwa vimehifadhiwa katika kijiji cha Mwachumu kata ya Girya Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

 Diwani wa kata ya Girya Safari Lewa alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10:00 jioni katika kijiji hicho ambapo tembo hao waliingia kwenye makazi ya watu na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao mbalimbali yakiwemo Mahindi pamojana na Pamba  katika mashamba ya wananchi.

MASHIRIKA YA UMMA YAPATA HASARA KUBWA KUTOKANA NA KUIBIWA KWA MIUNDOMBINU YAKE

MASHIRIKA YA UMMA YAPATA HASARA KUBWA KUTOKANA NA  KUIBIWA KWA MIUNDOMBINU YAKE
CHANGAMOTO  inayowakumba mashirika ya umma nchini ni kuibiwa kwa miundombinu mbalimbali ya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi  wa miundombinu mbalimbali  ambapo  shirika la  umeme (TANESCO)  mkoani  Shinyanga limeeleza kupata hasara kiasi cha shilingi millioni 9.5 kwa  mwaka 2012 huku shirika la mawasiliano  mkoani Shinyanga (TTCL) likipata hasara ya  zaidi ya shilingi millioni 108.
Ambapo Shirika la Reli  (TRL) kwa  wizi wa Mataluma ya kwenye barabara wameeleza   kuwepo kwa biashara ya vyuma chakavu,kutumia  kwenye majembe yanayokokotwa na ng’ombe pamoja na shirika la mawasiliano nchini  TTCL wakieleza baadhi ya wakulima kuchimbua nyaya zilizopo ardhini zinazohusika kupita kwa mkongo  wa  mawasiliano wa Taifa.

HALMASHAURI YA WILAYA YA BARIADI INAKABILIWA NA ZAIDI YA WANAFUNZI 450 HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA

HALMASHAURI YA WILAYA YA BARIADI INAKABILIWA NA  ZAIDI YA WANAFUNZI 450 HAWAJUI KUSOMA WALA KUANDIKA



HALMASHAURI  ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, inakabiliwa na idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), kutokana na uwajibikaji mdogo wa walimu na kutofundisha kwa vitendo, ikiwemo msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani.

Jumla ya wanafunzi 4999 ikiwa ni asilimia 8.5 ya wanafunzi wote katika wilaya , wasichana wakiwa 2660 asilimia 8.8, na wavuluna wakiwa jumla 2339, ikiwa ni asilimia 8.1, wote hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, hali inayosababisha kiwango cha taaaluma kushuka wilayani hapa.

MWENYEKITI CCM MKOANI SIMIYU ASISITIZA WANANCHI MUUNGANO WA SERIKALI MBILI

MWENYEKITI CCM  MKOANI SIMIYU  ASISITIZA WANANCHI MUUNGANO WA SERIKALI MBILI


MWENYEKITI  wa chama cha Mapinduzi  (CCM)  mkoani Simiyu ambaye pia ni  mbunge wa jimbo la Busega dkt  Titus Kamani ameendelea kusisitiza muungano wa serikali mbili  kwa sababu waasisi wa wazamani wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abed Karume walikaa na kujadili mafanikio ya muungano wa Tanzania na kusisitiza uwepo wa serikali mbili.

Mbunge huyo ambaye ni waziri wa maendeleo ya uvuvi na mifugo alisema  ni  busara za waasisi hao za kusistiza muungano na kuenzi zilizopelekea kuundwa kwa muundo wa serikali mbili zimesababisha hali ya muungano mpaka sasa kuwa imara na kuleta amani baina ya watanzania, na kutaka muundo huo ni vyema ukaendelea ili kulinda muungano.

MWANAMKE ALIWA FISI SHAMBANI KWAKE AKICHUMA MBOGA

MWANAMKE ALIWA FISI SHAMBANI KWAKE AKICHUMA MBOGA



MKAZI  mmoja wa kijiji cha Giriku  kata ya Bunamhala  wilayani Bariadi mkoani Simiyu  aliyefahamika kwa jina la Nshoma  Mawe (29) amepoteza maisha  baada ya kuvamiwa na fisi kisha kun’gata wakati akiwa shambani nyumbani  kwake akichuma mboga.

Kwa mujibu wa  taarifa ya kamanda wa jeshi la polisi  mkoani humo  Charles Mkumbo  aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake amesema  kuwa tukio hilo  limetokea mnamo  majira ya saa 6:00 jioni.

KARENY BLOG: ZAHANATI YA KIJIJI CHA BUGANIKA HAINA CHOO, WALA M...

KARENY BLOG: ZAHANATI YA KIJIJI CHA BUGANIKA HAINA CHOO, WALA M...
KARENY BLOG: ZAHANATI YA KIJIJI CHA BUGANIKA HAINA CHOO, WALA M...: AKINAMAMA  wajawazito wanaokwenda kujifungua katika zahanati ya Buganika wilayani Kishapu mkoani  wamekumbwa na changamoto ya kulazimisha  k...

ZAHANATI YA KIJIJI CHA BUGANIKA HAINA CHOO, WALA MAHALI PA KUTUPIA TAKA NGUMU.

ZAHANATI YA KIJIJI CHA BUGANIKA HAINA CHOO, WALA MAHALI PA KUTUPIA TAKA NGUMU.
AKINAMAMA  wajawazito wanaokwenda kujifungua katika zahanati ya Buganika wilayani Kishapu mkoani  wamekumbwa na changamoto ya kulazimisha  kubeba uchafu  wao mara  baada ya kujifungua kutokana na kukosekana kwa choo wala eneo la kutupia taka ngumu  katika zahanati hiyo.

Hali hiyo imeonekana  wauguzi kuwalazimisha wajawazito kwenda wakiwa wamebeba mifuko ya rambo kwa ajili ya kubebea makondo ya nyuma na uchafu mwingine baada ya kujifungua jambo ambalo  ni hatari kiafya ikiwa hutozwa kiasi cha shilingi 10,000 kama gharama za huduma  badala ya wajawazito kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya afya.

Akizungumzia hali hiyo hivi karibuni mjini Shinyanga mmoja wa wezeshaji  kutoka mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai alisema wakazi wa kijiji cha Buganika walitoa malalamiko hayo wakati wa zoezi la uraghabishi katika vijiji vya Buganika, Mwabayanda, Ngh’wigumbi na Buchambi ambapo baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walihoji utaratibu huo iwapo unatumika kwingineko.

BAADHI YA WANANCHI WA KATA ZA NDALA NA MASEKELO MANISPAA YA SHINYANGA WAILALAMIKIA HOSPITAL YA MKOA KUPANDISHA GHARAMA.

BAADHI YA  WANANCHI WA KATA ZA NDALA NA MASEKELO MANISPAA YA SHINYANGA  WAILALAMIKIA HOSPITAL YA MKOA KUPANDISHA GHARAMA.

BAADHI ya WANANCHI wa kata za Ndala na Masekelo manispaa ya Shinyanga  wameilalamikia hospitali ya mkoa wa Shinyanga kupatindisha gharama ya kuchukua cheti  cha kuanza matibabu kutoka shilingi 1000 hadi 5000,hali ambayo inasababisha   wenye kipato cha chini kushindwa kupata matibabu  ikichangiwa  kukosekana vituo vya afya na zahanati kwenye maeneo yao.

Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hizo ambazo ziko manispaa ya Shinyanga,walisema gharama imekuwa kubwa ni vema kwanza serikali ingeboresha vituo vya afya  na zahanati na kujenga kila kata, ili kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini kwenda kupata huduma tofauti na ilivyo sasa.

WAKAZI WA KIJIJI CHA SANGITA KATA YA USANDA WAKABILIWA NA UHABA WA MAJI

WAKAZI WA KIJIJI CHA SANGITA KATA YA USANDA WAKABILIWA NA UHABA WA MAJI


BAADHI ya wakazi   wa kijiji cha Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma za maji, hali inayowalazimu kwenda kuchota maji mto Shimiwi huku wakihofia afya zao kukumbwa na magonjwa  ya mlipuko  pia kuchangia  na mifugo.

Hayo yalielezwa  na baadhi ya wananchi  wakati wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kijijini humo,ambapo walisema hakuna visima vya maji wala  mabomba na kwamba maji wanayotumia wanakwenda kuchimba mtoni na wakati mwingine hukuta fisi wakinywa maji.

HALMASHAURI WILAYA YA KISHAPU IMEBAINI KAYA 5881 KUKOSA VYOO

HALMASHAURI WILAYA YA KISHAPU  IMEBAINI  KAYA 5881 KUKOSA VYOO



HALMASHAURI ya  wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga imebaini kaya  5881 kutokuwa na vyoo ikiwa kaya  3335 zimejenga vyoo vya muda  hali ambayo  inaonyesha kuwa  hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko hasa ya  kuhara na kipindupindu.

Kaya hizo zilibainika wakati  wa kampeni  inayoendelea ya usafi wa mazingira na kuihamasisha jamii kuwa na vyoo bora katika kata zote za wilaya hiyo  kwa kutumia sheria ndogo za halmashauri, huku mila na desturi  zikitajwa kuwa ni chanzo cha kuwepo tatizo hilo  na kuona ni muhimu kwa kujisaidia vichakani.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa mazingira wa wilaya ya Kishapu Mohamed Mlewa, alisema wilaya inakaya 42,000 kati ya hizo zenye vyoo bora ni 12,680 vya kawaida 20,114 na ambavyo  vimejengwa kwa matumizi ya muda ni 3335 huku kaya 5881 vikiwa havina vyoo .

“Ni muhimu kila kaya iwe na choo tena tunasisitiza kiwe bora na ndiyo maana tunaendelea kutoa elimu kwa jamii, iweze kubadilika iache mila na desturi zilizopitwa na wakati kama sasa hivi  tumebaini kuwepo kaya 5881 zisizokuwa na vyoo  hata vya muda hawana”alisema Mlewa.

Alisema walitembelea kata za Masanga ,Shagihilu,Mwamashele na Ukenyenge  ambapo walizungumza na wananchi na kutoa elimu sanjari na kukagua kaya  kama zinavyoo nakukuta baadhi hazina ambazo walizitaka kuhakikisha wanachimba haraka il kuzuia kuibuka magonjwa ya mlipuko.

Ameitaka  jamii kubadilika kwa kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa safi ,hatua itakayosaidia kujiepusha kukumbwa  na kipindupindu hasa kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha, ambapo hutokea mlipuko wa magonjwa mbalimbali mazingira yakiwa machafu.

Wakati huo huo ilibainika pia  kukosekana  kwa miundombinu bora ya maji na vyoo pamoja na mazingira machafu umesababisha nyumba za kulala wageni tatu na hoteli mbili kufungwa, katika halmashauri  hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya idara  ya usafi wa mazingira wilayani humo kufanya ukaguzi na kubaini kuwepo changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa maji,kalo la maji machafu na miundombinu ya ndani kutoridhisha yakiwemo mashuka hivyo kuhatarisha afya za wateja.

.“Hili zoezi lilifanyika march 27 mwaka huu katika mji wa mhunze ambapo tulifunga hotel  mbili na kisha mji mdogo wa Maganzo hoteli moja na nyumba za kulala wageni mbili,tunaendelea na zoezi hili kwa wilaya nzima ili kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi ”alisema Mlewa.

Afisa mazingira alisema zoezi hilo limeanza kwa kupitia hoteli na baa na kwamba hatua itakayofuata ni kukagua migahawa,ambapo aliwataka  wananchi kuhakikisha wanaweka mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ambao unaweza kutokea kwa kusababishwa na uchafu.

CHANGAMOTO KUBWA INAYOWAKUMBA WATOTO KWEYE KITUO MAAMULU CHA WALEMAVU BUHANGIJA NI UHABA WA VITANDA

CHANGAMOTO KUBWA INAYOWAKUMBA WATOTO KWEYE KITUO MAAMULU CHA WALEMAVU  BUHANGIJA NI UHABA WA VITANDA



CHANGAMOTO kubwa inayowakabili watoto  kwenye kituo  maalumu cha kulea watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali cha Buhangija manispaa ya Shinyanga, ni upungufu  wa vitanda hali inayowalazimu kulala watatu watatu  kutokana na kutokidhi mahitaji ambapo vilivyopo ni 156 huku watoto wakiwa 258.

Hayo yalielezwa  na mwalimu mkuu wa  shule ya Buhangija ambaye anasimamia kituo hicho,wakati akipokea msaada wa chakula,sukari na mafuta kutoka kwa mbunge wa viti maalumu(CCM) mkoa wa Shinyanga Azza Hamad,aliyetembelea kituo hicho.

Ambapo mbunge huyo alijionea  kero mbalimbali zinazowakabili watoto hao ukiwemo upungufu wa mabweni pia yaliyopo ni matatu yenye uwezo wa kuchukua watoto 100 pekee.

UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) KANDA YA ZIWA WATAKA MUUNDO WA SERIKALI MBILI

UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) KANDA YA ZIWA WATAKA MUUNDO WA SERIKALI MBILI



UMOJA wa vijana  wa chama  cha Mapinduzi    kanda ya ziwa  (UVCCM) umewataka watanzania kutokubali muundo wa serikali tatu na kuwaeleza kuwa  iwapo zitakuwepo hizo serikali  upatikanaji wa  fedha zinazotokana na ulipaji kodi  hazitatosheleza ikiwa  jamii bado zinahitaji  huduma   bora   kwenye  afya,elimu na  mambo mengine .

 

  Hayo wameyasema kwenye matembezi ya mbio za pikipiki  ya muungano  taifa yaliyoandaliwa na umoja wa vijana  wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)  taifa  ambapo matembezi hayo  yalikuwa yamebeba ujumbe wa  dumisha  muungano  vijana  kwa fursa  zilizopo kwa maendeleo yetu,  kwa mkoa wa shinyanga yalipokelewa kutoka mkoani Simiyu  katika kijiji cha Wigelekelo  wilayani Maswa.

 

Kiongozi wa matembezi ya mbio hizo  kanda ya ziwa Zuberi Bundala alisema kuwa  wameamua kuzunguka wilaya zote za kanda kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi  ikiwa baadhi ya vyama  wanadai kuwepo kwa serikali tatu  jambo ambalo litafanya jamii kukosa mambo ya msingi kwa kupitia kodi wanazolipa.

WAKULIMA WALIA NA NDEGE WAITWAO KWELEA KWELEA KWA KULA MAZAO YAKIWA SHAMBANI

WAKULIMA WALIA NA NDEGE  WAITWAO KWELEA KWELEA  KWA KULA MAZAO YAKIWA SHAMBANI



WAKULIMA  kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga wameiomba  serikali kuchukuwa hatua za haraka  kuangamiza ndege waharibifu wa mazao kwelea kwelea ili kunusuru mazao yao kumalizwa na kuwepo tishio la kukumbwa na njaa pamoja na watoto kushindwa kuhudhuria masomo kwa kulinda ndege.

Wakiongea  na  waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo,walisema mazao yao yanaliwa na ndege hao ukiwemo mpunga,mtama na uwele na kwamba wanahofia kukosa chakula kutokana na kushambulia kwa kasi na kubakiza mabua pekee.

Mkulima wa kijiji  cha Manyanda  Nyanda Jumanne  alisema hali kwa sasa ni mbaya na wanahitaji msaada wa haraka wa serikali, vinginevyo muda ukizidi kwenda kabla ya kuwadhibiti wakulima hawataambulia kitu na matokeo yake watakuwa wamepoteza nguvu zao bure.

KARENY BLOG: ajinyonga

KARENY BLOG: ajinyonga
KARENY BLOG: ajinyonga: MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga a...

KARENY BLOG: ajinyonga

KARENY BLOG: ajinyonga
KARENY BLOG: ajinyonga: MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Shija Mfuko (60) mkazi wa kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga a...

KARENY BLOG: KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU ...

KARENY BLOG: KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU ...
KARENY BLOG: KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU ...: KITUO cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC)  kimetoa elimu ya Rasmu ya pili ya  katiba  kwa wananchi wa kata ya kitangili mjini s...
KARENY. Powered by Blogger.