WAJASILIAMALI wenye kipato kidogo manispaa ya Shinyanga wametakiwa kujiunga na mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma ( PSPF) mara
baada ya kutolewa elimu ikiwa imebainika kuwa asilimia kubwa bado hawajajiunga na mfuko huo kwa dhana iliyojengeka kuwa ni kwaajili ya watumishi pekee.
Inatakiwa wajasiliamali waone umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya
jamii hapa nchini na kuweza kunufaika nayo kwa kutunza fedha ambazo
zitawasaidia katika maisha ya sasa nayabaadae.
Akitoa elimu hiyo kwa wajasiliamali wa soko kuu la mjini
Shinyanga mjumbe wa Bodi wa mfuko huo kutoka Jijini Dar es salaam Clement Mswanyama alisema asilimia kubwa ya
wajasiliamali hapa nchini hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na
kuwafanya kukosa fedha za kuwasaidia katika maisha hasa pale wanapopatwa
na matatizo.
“ Watu
wanaofanya shughuli zenye kipato kidogo asilimia kubwa wamekuwa
wakisahaurika kupewa fursa ya kujiunga na mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii na
kuwathamini watumishi ambao wameajiriwa hali ambayo huwajengea watu hao
mazingira ya kuwa na maisha magumu”alisema .
Alisema mtu anapojiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii
itamsaidia kujiwekea hazina ya fedha ambazo zitamsaidia katika maisha yake hasa
pale anapopatwa na matatizo ya kifamilia ikiwa ni pamoja na kupata mafao yake
ya uzeeni na hivyo kumfanya kuendelea kuwa na maisha.
Alibainisha kuwa shirika hili la PSPF lilikuwa linahudumia watumishi wa
serikali peke yao lakini kutokana na serikali kuona idadi kubwa ya
wafanyabishara wa kujitegemea kusahaulika kupewa fursa ya kujiunga na mifuko
hiyo ambapo imeweza kupanua wigo na kuwapa nafasi wajasiliamali kuchangia fedha
kidogo kidogo kwa kila mwezi katika mfuko huu ilikuboresha maisha yao.
Naye meneja wa Shirika hilo mkoani Shinyanga Elick Chanimbaga alisema wameamua kutoa elimu hiyo kwa
wajasiliamali wote mkoani hapa kwa kushirikisha wafanyabishara wa masoko,
mama Lishe,waendesha bodaboda, wafanyakazi wa viwandani na lengo kubwa likiwa
ni kuwajengea msingi mzuri wa maisha kutokana na utunzaji wa fedha katika mifuko
ya hifadhi ya jamii.
Kwa upande wao baadhi
ya wajasiliamali wa soko hilo James Jilinde
na Hawa Ngoshaji kwa nyakati
tofauti walishukuru elimu iliyotolewa huku wakidai kuwa walikuwa hawajui faida ya
kujiunga na mifuko hiyo na kufikiri
walengwa ni watumishi wa serikali pekee.
0 Response to "PSPF YATOA ELIMU KWA WAJASILIAMALI SOKO KUU MANISPAA YA SHINYANGA."
Post a Comment