Habari za hivi Punde

WAFANYABIASHARA SOKO LA NGUZONANE WALALAMIKIA ONGEZEKO LA USHURU

WAFANYABIASHARA SOKO LA NGUZONANE WALALAMIKIA ONGEZEKO LA USHURU




WAFANYABIASHARA  wa vibanda katika soko la Nguzo nane manispaa ya Shinyanga mkoani hapa wamelalamikia ongezeko la kutozwa ushuru kutoka shilingi 15,000 na kupandishiwa shilingi 30,000 jambo ambalo wamemuomba mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang’ombe kuongea nao ili kutatua suala hilo.

Wafanya biashara hao wakizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo jana walisema kuwa kilio chao kikubwa ni kumuomba mkurugenzi wa manispaa hiyo waongee nae kwani wamekuwa wakipandishiwa ushuru bila hata kuwashirikisha wao hali ambayo wanadai wananyongwa kulingana na kipato kidogo wanachokipata katika biashara zao.

WAAJIRI WATAKIWA KUACHA KUPOKEA RUSHWA KWA LENGO LA KUMPITISHA MFANYAKAZI BORA SIKU YA MEIMOSI

WAAJIRI WATAKIWA KUACHA KUPOKEA RUSHWA KWA LENGO LA KUMPITISHA MFANYAKAZI BORA SIKU YA MEIMOSI


WAAJIRI wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani hapa wametakiwa kuacha kupokea rushwa na kupendelea pindi wanapoteuwa wafanyakazi bora ambao wanastaili kupewa zawadi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya sikukuu za wafanyakazi Duniani Meimosi

Akizungumza katika kikao cha wadau wa sherehe za Meimosi juzi mjini shinyanga mkuu wa mkoa Shinyanga Ally Rufunga, wakati wadau hao wakijadili mikakati ya kufanikisha maadalizi ya sherehe hizo alisema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya waajiri kupokea Rushwa na kuteuwa wafanya kazi wasio na vigezo.

MADIWANI WALIOJIUZURU NA KUJIVUA UANACHAMA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM MKOANI SHINYANGA

MADIWANI WALIOJIUZURU NA KUJIVUA UANACHAMA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM MKOANI SHINYANGA



MADIWANI waliojiuzuru  nyasifa hiyo na kuamua kuondoka  katika chama cha CHADEMA  ambao ni  Sebastiani  Peter na Zacharia Mfuko  wamejiunga rasmi  na chama cha Mapinduzi  (CCM) mbele ya katibu wa itikadi na uenezi Nape Nnauye na uongozi wa mkoa wa chama hicho.

Maelfu ya wakazi  wa mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano wa hadhara  uliofanyika katika viwanja  vya  Mahakama Nguzo nane  huku wakishuhudia waliokuwa wananchama  na viongozi ndani ya Chadema wakipanda jukwaani ghafla huku wakiwa wamevaa kofia za CCM na kueleza kiliwafanya kujiunga na chama hicho  kutokana na kutuhumiwa kila kukicha kuwa ni mamluki ndani ya Chadema.

TANESCO MIKOA YA SIMIYU NA SHINYANGA YAWAONYA VISHOKA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU

TANESCO MIKOA YA SIMIYU NA SHINYANGA YAWAONYA VISHOKA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU




SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) katika mikoa ya simiyu na shinyanga limewaonya  wale wote watakao haribu miundo mbinu ya shirika hilo  wakiwemo  vishoka ambao wamekuwa wakililetea shirika hasara kubwa  kwa kuharibu mita na kufanya gharama za uzalishaji na uendeshaji kuwa kubwa hivyo watakao bainika  kwa uhalibifu  huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Hayo yalibainishwa mjini shinyanga kwenye mkutano wa hadhara na Afisa mkuu wa huduma kwa wateja TANESCO katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga Musa Kasimu wakati akitoa elimu kwa wakazi wa mjini humo  juu ya huduma zinazotolewa na shirika la TANESCO  kwa wananchi

MADIWANI WA CHADEMA MANISPAA YA SHINYANGA WAJIUZURU NYASIFA HIZO

MADIWANI WA CHADEMA MANISPAA YA SHINYANGA WAJIUZURU NYASIFA HIZO



MADIWANI wawili wa chama cha maendeleo chadema  wametamka rasmi kujiuzuru nyasifa hiyo kutokana na madai ya uongozi ngazi ya taifa  kuendelea kusikiliza majungu,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwaita  wahaini au wasaliti katika chama  bila kuchambua ukweli na kutotekeleza waliyoyaahidi kwa wanachama wao.


 Madiwani hao ni Sebastiani Peter  kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo kwa pamoja jana waliongea na waandishi wa habari katika ofisi ya naibu meya wa manispaa hiyo huku wakieleza kuwa  wanayatamka rasmi maneno  mbalimbali yaliyopelekea kujiuzuru kama inshara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa kitaifa kwa nyakati tofauti.

Ambapo diwani Sebastiani alisema kuwa kuna sababu tatu zilizopelekea yeye kujiuzuru nafasi ya udiwani na ukatibu wa mbunge vita maalumu , ya kwanza ni mwezi Novemba  mwaka 2013 kikundi cha Briged kiliweza kuandika  barua kwa katibu mkuu wa chama hicho taifa na kulenga kuwadhalilisha  viongozi  akiwemo katibu  mkoa na wilaya kuwa wamehongwa kiasi cha shilling millioni  90.

“Tuhuma hii  leo ninaamini ni tuhuma ya uongo iliyolenga kuwadhalilisha viongozi  ambao ni Nyangaki Shilungusheila katibu wa mkoa na Siri yasini mwenyekiti wa wilaya  ambapo kimsingi  ndio walipotufikisha  hapa tulipo,kitendo cha katibu mkuu wa chama kupokea  barua hiyo na kushindwa kuifanyia kazi  wakati viongozi hawa  wamewahi kufungiwa  hata kwenye mkutano mkuu wa wilaya jambo hili limenifanya  niamini nyumba ya red brigedia  wapo viongozi  wa kitaifa  wanaowaagiza kufanya hayo”alisema diwani Sebastiani Peter.

Alisema jambo la pili ni kutokana na ahadi za mwenyekiti wa taifa Freeman Mbowe kuahihdi chama kitamaliza kujenga nyumba ya marehemu Shelembi  aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini na diwani kata ya Masekelo ambapo ahadi aliitoa siku ya mwisho  kwenye mazishi ya kiongozi huyo  katika viwanja vya shy-com huku mwenyekiti huyo katika kikao kingine alichokuwa akikiongoza kupinga ujenzi wa nyumba hiyo.

MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YAANZA KUSIKILIZA KESI ZA MAUAJI MKOANI SHINYANGA NA SIMIYU.

MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YAANZA KUSIKILIZA KESI ZA MAUAJI MKOANI SHINYANGA NA SIMIYU.
MAHAKAMA  kuu kanda ya Tabora imeanza kusikiliza kesi za mauaji  mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga kwa mwaka huu ikiwa kesi kumi na moja  zitasikilizwa ndani ya mwezi mmoja ikiwemo  mauaji yanayotokana na imani za kishirikina.

Ambapo mara baada ya kumalizika ufunguzi wa kusikiliza kesi hizo mahakama  ilianza  kwa kuangalia upande wa  mtuhumiwa Mbula  Mako aliyekuwa mganga wa kienyeji  kufanya mauaji  dhidi ya kikongwe Buguta Mashilima huko katika kijiji cha Nobora wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

VIJANA KUTOJITAMBUA WAMESHINDWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MCHAKATO WA KUTOA MAWAZO YAO RASMU YA KATIBA MPYA

VIJANA KUTOJITAMBUA WAMESHINDWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MCHAKATO WA KUTOA MAWAZO YAO RASMU YA KATIBA MPYA
KITENDO cha vijana kutokujitambua  kumesababisha washindwe kushiriki kikamilifu katika  mchakato wa kutoa mawazo yao kuhusu rasmu ya katiba mpya.
Hayo yalielezwa na Mkurungenzi wa Asasi  isiyo ya kiserikali inayotetea haki za wanawake na  watoto wenye maambukizi ya virusi  vinavyosababisha  Ukimwi  (AGAPE)   John  Myolla   katika ufunguzi   wa kongamano la vijana kujadili rasmu ya katiba mpya lililofanyika mjini hapa  jana.
Myolla alisema  kundi la vijana lina umuhimu wa pekee kwa jamii, lakini wameshindwa kujitambua  na kujikuta wakijishughulisha na mambo  ya  mzaha na kupuuza  yale  yenye  kuleta tija kwa taifa.

ZAIDI YA ASILIMIA 80 YA VIJANA NCHINI HUFANYIWA UKATILI

ZAIDI YA ASILIMIA 80 YA VIJANA NCHINI HUFANYIWA UKATILI




ZAIDI ya asilimia 80 ya vijana nchini  wenye umri  kati ya miaka   13 hadi 24 wameripotiwa kunyanyaswa kingono,kudhalilishwa kihisia na kujeruhiwa walipokuwa watoto chini ya umri wa miaka 18 huku matukio hayo  yakishamiri zaidi sehemu za shule na kuathiri uwezo wa
 watoto kielimu.
 
 Hayo yalielezwa jana na meneja wa shirika la  Save The Children mkoa wa Shinyanga Augustino Mwashiga wakati wa uzinduzi  mradi wa kudhibiti ukatili dhidi ya watoto,alisema utafiti uliofanywa na UNCEF mwaka 2008  ulibaini kuwepo ukatili huo hapa nchini huku wastani wa matukio nane hadi 10 ya ukatili hutokea kila mwezi mkoani
 humo.

SHULE ZA MSINGI TATU KATA YA NDEMBEZI MANISPAA YA SHINYANGA ZAPATA MSAADA WA MAHINDI

SHULE ZA MSINGI TATU  KATA YA NDEMBEZI  MANISPAA YA SHINYANGA ZAPATA MSAADA WA MAHINDI



SHULE za msingi  tatu zilizopo  kata ya ndembezi  manispaa ya shinyanga  zimepatiwa jumla ya magunia  kumi na moja ya  msaada wa mahindi yenye thamani ya shilingi  lakitano na nusu kwaajili ya  wanafunzi kupata  uji asubuhi  wakiwa shuleni hapo ili kuondokana na ubagudhi wa wasiolipa fedha kutokunywa uji na waliolipa kunywa.
Msaada huo wa mahindi yaliyotoka kwenye kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu na kuamua kuyanunua    diwani wa kata hiyo David Nkulila  ambaye pia ni naibu meya wa halmashauri  ya manispaa hiyo  kwa gunia moja shilingi 500 huku akidai kuwa  aliamua kutoa msaada  kutokana na  baadhi ya wazazi kushindwa kutoa mchango wa kupata uji wanafunzi .

SHULE YA SEKONDARI MASEKELO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UKOSEFU WA VIWANJA VYA MICHEZO,UHABA WA MAJI PAMOJA NA MASHAMBA

SHULE YA SEKONDARI MASEKELO  INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UKOSEFU WA VIWANJA VYA MICHEZO,UHABA WA MAJI PAMOJA NA  MASHAMBA
SHULE ya sekondari   Masekelo iliyopo kwenye kata hiyo manispaa ya Shinyanga  inakabiliwa na changamoto mbalimbali  ya kukosa eneo kwaajili viwanja vya michezo, mashamba ya kulima vyakula ,uhaba wa maji , hali ambayo inawafanya  wanafunzi wa shule hiyo kukosa haki zao za msingi.

Zoezi la utekelezaji kilimo cha mtama kwa shule hiyo halipo sababu ya kukosa mashamba,hakuna eneo lililotengwa  viwanja vya michezo ikiwa wananchi wanalima mpaka nyuma ya madarasa ya shule  huku bado wenye mashamba yao walionyang’anywa na manispaa hawajalipwa fidia,pia haina maji ingawa wanapata uji wanafunzi shuleni hapo kwa kulipia shilingi  40,000 kwa mwaka.

 Mkuu wa shule hiyo  Stephen Mihambo  aliongea na baadhi ya  waandishi wa habari waliotembelea shuleni hapo  huku akieleza kuwa shule  inajumla ya wanafunzi  319 ,vipindi vya michezo vipo ila hakuna uwanja wa michezo, hali inayojionyesha ni mwamko mdogo wa jamii katika suala zima la elimu  kwa kushindwa kutoa maeneo ya mashamba yao ili shule ipate viwanja vya michezo.

CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA IMEKUWA NI TATIZO MKOANI SHINYANGA.

CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA IMEKUWA NI TATIZO MKOANI SHINYANGA.
CHANGAMOTO ya kuozesha wanafunzi wa kike mara wanapohitimu darasa la saba  huku wavulana wakiendelea kutumikishwa na shughuli za uchungaji mifugo na mambo mengine imekuwa  kubwa  ndani ya jamii na kufanya hali  ya kuripoti kwa wanafunzi wa  shule za sekondari waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza  mkoani Shinyanga  kufikia  asilimia 78 .

 Hayo yalisemwa  na mkuu wa mkoa wa huu  Ally Rufunga wakati akiongea na waandishi wa habari  huku akieleza kuwa  wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari wamepata nafasi wote sawa na asilimia 100 lakini kuripoti ndio imekuwa changamoto ambapo watendaji wa vijiji na kata wamepewa jukumu la uangalizi huo ikiwa mwisho wa kuripoti ni mwezi huu.

MAUAJI YA ALBINO YAMEPUNGUA ,YANAYOENDELEA NI MAUAJI YA KUWANIA URITHI,ARDHI PAMOJA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

MAUAJI YA ALBINO YAMEPUNGUA ,YANAYOENDELEA NI MAUAJI YA KUWANIA URITHI,ARDHI PAMOJA NA IMANI ZA KISHIRIKINA


SERIKALI mkoani Shinyanga  imeeleza kupungua kwa mauaji ya albino kwa kiwango kikubwa  ikiwa kwa mwaka jana hakuna tukio lolote lililotokea la mauaji hayo isipokuwa mauaji ya watu wengine wakimweo vikongwe kuendelea kujitokeza  kwa kusababishwa  kugombea  mirathi,ardhi pamoja na  imani za kishirikina.

Hayo yalisemwa  na mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga wakati akiongea na waandishi wahabari katika ukumbi  wa mkoa huku akieleza  kuwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yamepungua kwa asilimia 100 huku mauaji vikongwe na watu wengine yamepungua kwa asilimia 96.

Alisema hali ya ulinzi na usalama  kwa sasa ni shwari ikiwa mwaka wa 2012 kulitokea tukio moja la mauaji wilayani Kahama ,ambapo mwaka wa 2013 hakuna tukio lolote lililotokea  ila hali ya mauaji ya vikongwe na watu wengine imeendelea kujitokeza kwa sababu ya w engine kuwania mali,mirathi na imani za kishirikina.

MAMA NA MWANAYE WAULIWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA

MAMA NA MWANAYE WAULIWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKANA



MAMA na mwanaye  wameuwawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana kwa kuwavamia nyumani kwao  majira ya  usiku  huko  katika kijiji cha Ngokolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga

 Watu hao  waliofahamika kwa majina  ya Helena Charles(30)   na Mlu Nambo ( 50) 

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga  Evarist Mangala tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja na nusu usiku katika kijiji hicho  wakati wakijiandaa kupata chakula cha uskiku nyumbani hapo.

UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII UNALETWA NA MTAZAMO HASI

UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII UNALETWA NA MTAZAMO HASI




UKATILI wa kijinsia  katika jamii na familia   unaletwa  na mtazamo hasi  kwani  matendo kati ya mwanamke na mwanaume  yanategemeana  ambapo  mifarakano hutokea kwa kupingana na kuendeleza changamoto zilizomo kwenye mila na desturi   ikiwemo kuwazuia watoto wa kike  kupata elimu ,ndoa za utotoni   pamoja na ukeketwaji.

Hayo yalisemwa na mwezeshaji  ambaye ni pia ni mhariri mtendaji wa gazeti la jamhuri  Deogratius Balile kwenye semina iliyowajumuisha waandishi wa habari  kutoka mikoa ya Simiyu na Shinyanga yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) huku  akieleza kuwa waandishi  wananafasi kubwa ya kuibadilisha jamii .

WANANCHI MKOANI SIMIYU WALILALAMIKIA SHIRIKA LA UMEME TANESCO

WANANCHI MKOANI SIMIYU WALILALAMIKIA SHIRIKA LA UMEME TANESCO


WANANCHI  mkoani Simiyu wamelilamikia Shirika la Ugavi Umeme (TANESCO)  kwa tabia ya kukata kata umeme bila taarifa na kuwaweka gizani wateja wake kwa mara kwa mara hali ambayo inawatia hasara kubwa kwa kuunguza vyombo mbalimbali vinavyotumia umeme ikiwemo wajasiriamali kushuka kwa vipato vyao.
Licha ya shirika hilo kuahidi mara kadhaa kuondwa tatizo la umeme linaondolewa tangu mwishoni mwa mwaka jana lakini hali ya katakata umeme na wananchi kulala gizani na kushindwa kufanya kazi za kila siku zikiwemo za ujasilia mali limekuwa kero kubwa sana kwao.

MADIWANI BARIADI WAKATAA KUPITISHA TAARIFA YA MAAFA KWA KUDAI NI MWAKA JANA

MADIWANI BARIADI WAKATAA KUPITISHA TAARIFA YA MAAFA  KWA KUDAI NI  MWAKA JANA






Baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Bariadi  mkoani Simiyu  limeikata taarifa ya maafa katika vijiji mbalimbali vilivyotokea na kudai kuwa ni ya mwaka jana huku afisa kilimo Issa Mtweve akishindwa   kuorodhesha vijiji vilivyoadhirika na janga  la njaa wilayani humo.

Wakiongea ndani ya kikao cha baraza hilo madiwani hao walisema kuwa vijiji vilivyokuwa vimeorodheshwa katika taarifa hiyo havikuwa sahihi, kutokana na kuwa vichache kulinganisha na hali halisi ya tatizo hilo lilopo katika kata zao.

ZOEZI LA UNYWAJI UJI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IHUGI HUENDA LIKASITISHWA KUTOKANA NA WAZAZI KUKOSA FEDHA ZA MICHANGO

ZOEZI LA UNYWAJI UJI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IHUGI  HUENDA LIKASITISHWA KUTOKANA NA WAZAZI KUKOSA FEDHA ZA MICHANGO
ZOEZI  la  kunywa uji kwa wanafunzi wa  shule  ya msingi Ihugi kata ya Lyamidati   katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga huenda likasitishwa kutokana na shule hiyo kukosa chakula na wazazi kuwa na hali ngumu ya kifedha katika kusaidia upatikanaji  wa unga.

 Akiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea shuleni hapo , mwalimu mkuu wa shule hiyo  Ayoub Mesoyo   alieleza  kuwa  shule imefunguliwa lakini zoezi la kupata uji shuleni hapo litasitishwa kutokana na ugumu wa kupata msaada wa mahindi na kifedha   kutoka kwa wazazi.

WAUZAJI TINDIKALI WATAKIWA KUJISAJILI KATIKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

WAUZAJI TINDIKALI WATAKIWA KUJISAJILI KATIKA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
JESHI la polisi mkoani Simiyu limewataka wauzaji wa tindikari mkoani humo  kuhakikisha wanasajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali, ili kutambulika kisheria sambamba na kupewa utaratibu wa matumizi sahihi ya bidhaa hiyo kwa lengo la kuondoa matumizi mabaya ikiwemo kuwadhuru watu.

Mbali na hilo kamanda  wa jeshi hilo Charles mkumbo amewatahadharisha wananchi wote ,kuwa kwa yeyote atakayekutwa na tindikari mtaani, atakamatwa, ikiwa pamoja na kufikishwa mahakani.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda Mkumbo alisema kuwa katika utaraatibu uliowekwa kwa sasa kwa wauzaji wa bidhaa hiyo unamtaka kila muuza tindikari kusajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu,sambamba na kupewa maelekezo ya jinsi ya kutumia au kuuza bidhaa hiyo.

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU TISA KWA TUHUMA YA MAUAJI YA WANAWAKE WAWILI WALIOTUHUMIA KUZUIA MVUA ISINYESHE KATIKA KIJIJI CHA MWABULIMBU WILAYANI MASWA

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU TISA KWA TUHUMA YA MAUAJI YA WANAWAKE WAWILI WALIOTUHUMIA KUZUIA MVUA ISINYESHE KATIKA KIJIJI CHA  MWABULIMBU WILAYANI MASWA




JESHI  la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake wawili wa kijiji cha Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya akina mama wawili kuuawa na kuchomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha.

Licha ya wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi wa jadi "Sungusungu" akiwemo Mtemi  na Kamanda wake mkuu kwa tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao waliochomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani  humo.

MADIWANI HALMASHAURI MJI WA BARIADI WATAKA AGIZO LA RAIS KUTEKELEZWA HOSPITALI YA WILAYA KUWA YA MKOA

MADIWANI  HALMASHAURI MJI WA BARIADI WATAKA AGIZO LA RAIS KUTEKELEZWA HOSPITALI YA WILAYA KUWA YA MKOA


MADIWANI  wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wamemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Paschal Mabiti kutekeleza agizo la Raisi Jakaya Kikwete alilotoa wakati wa ziara yake mkoani hapa, la kupandisha kiwango hospitali ya Wilaya ya Bariadi kuwa hospitali ya Mkoa.

Mbali na Mkuu huyo wa Mkoa kutakiwa  kuhakikisha anatekeleza agizo hilo la Rais , madiwani hao walishangazwa na kitendo cha Kiongozi huyo wakati wa kikao cha ushauri cha Mkoa kilichokaa hivi karibuni kukataa kutekeleza agizo hilo kwa madai kuwa  Rais  hakuagiza kupandishwa kiwango hospitali hiyo.

HUHESO YATOA ELIMU KWA MADREVA MATUMIZI SAHIHI YA CONDOM

HUHESO YATOA ELIMU KWA MADREVA MATUMIZI  SAHIHI YA CONDOM



SHIRIKA la The Foundation for Human Health Society [HUHESO FOUNDATION] lenye makao makuu yake mjini Kahama limetoa elimu kwa wanaume wanaofanya kazi kwenye malori,migodini na madreva wa bodaboda juu ya matumizi sahihi ya Kondomu.

Mafunzo hayo yalitolewa na Shirika hilo baada ya kubaini chanzo kikubwa cha wanawake kufanya mapenzi yasiyo salama ni wanaume ambao wengi wao hufikia nyakati za matamanio kwenye mazingira ya starehe.

WADAU WA ELIMU WATAKA MFUMO UBADILISHWE ILI KUWEPO NA ULINGANO KWA WAZAZI

WADAU WA ELIMU WATAKA MFUMO  UBADILISHWE ILI KUWEPO NA ULINGANO KWA WAZAZI




WAMILIKI na  mameneja  wa shule za msingi,sekodandari na vyuo binafsi   kutoka mikoa nane ya nchini Tanzania   wameitaka serikali  kubadilisha  mfumo  wa elimu  kutokana  na  wazazi wanaosomesha watoto wao  kukosa msaada  wowote  unaopelekea kutozwa   kodi  mbalimbali  zenye kiwango kikubwa.

   Hayo yalisemwa  na   mwenyekiti wa Tamongsco  Jerrry Nyabululu   kwenye mkutano wa wamiliki na mameneja  wa vyuo na shule zisizokuwa za serikali kanda ya Magharibi,kanda ya ziwa na kanda ya ziwa magharibi  kwa mikoa ya Kagera,Mara,Mwanza ,Simiyu,Geita ,Kigoma,Tabora na Shinyanga  katika  risala yao mbele ya mgeni rasmi ambaye ni  mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga akiwa ameambatana  na Hadija Mcheka  mkurugenzi msaidizi wa usajili  kutoka wizara ya elimu.

Hata hivyo  waliiomba serikali ianzishe mjadala wa kitaifa miongoni mwa wadau wa elimu ili ikiwezekana mfumo wa elimu ubadilishwe  kwani imeonekana kuwa mtoto ambaye anasoma shule  binafis hapati msaada wowote  kutoka  serikalini kwa kutozwa kodi  nyingi  kwa kiwango kikubwa  ikiwa wazazi wao ni walipaji wakubwa wa kodi  mbalimbali za serikali kama wazazi wengine wanaosomesha  shule  zingine.

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKUTWA AMEJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITO

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI  AKUTWA AMEJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITO


MWALIMU  wa shule ya msingi Mwang’osha kata ya nyamalongo wilaya ya shinyanga  mkoani hapa Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika choo kilichopo nyumbani kwake huku akiacha ujumbe mzito uliotia simanzi.

 Mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Maleko aliwaeleza waandishi wa habari kuwa  marehemu aligundulika akiwa amejinyonga juzi majira ya saa tisa na nusu alasiri mara baada ya kutoonekana shuleni kwa mda mrefu.

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU KUTOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO YAFIKIA ASILIMIA7.3 MKOANI SIMIYU

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU KUTOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO YAFIKIA ASILIMIA7.3 MKOANI SIMIYU



MKOA  Wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa sita nchini  ambayo inakabiliwa na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama Mjamzito kwenda kwa mtoto na kufikia asilimia 7.3
Hayo yamelezwa na Dkt  Hamis Kulemba ambaye ni Mratibu wa kuzuia magonjwa ya ngono na Ukimwi mkoa wa Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa  mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kwa mtoto kutoka kwa mama mkoani humo

ZAHANATI YAFUNGWA KWA KUKOSA VIGEZO.

ZAHANATI YAFUNGWA KWA KUKOSA VIGEZO.


ZAHANATI  inayomilikiwa na  mtu binafsi katika kijiji cha songambele kata ya Salawe wilayani Shinyanga  imefungwa na wataalamu  wa afya kutoka    mkoani  hapa  kutokana na kukosa vigezo  vya kuwa zahanati  babala  ya  duka la  madawa kama  ilivyokusudiwa  huku  daktari   msimamizi wa  wakimkataa kwa kukosa sifa,  ambapo  ilikuwa ikitoa huduma mbalimbali za matibabu  kama vile upimaji wa  damu,malaria  na uzalishaji wa mama wajawazito.

Zahanati hiyo imefungwa mwezi januari  mwaka huu,ambapo  mmiliki wake dkt Daniel Emanuel  aliwaeleza waandishi wa habari kuwa  zahanati imepata usajili  mwaka 1994 na kuanza kutoa huduma    katika kijiji hicho ambapo kwa siku  alikuwa akihudumia  wagonjwa zaidi ya  kumi.

HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UENDESHAJI WA KESI KUCHELEWA.

HAKIMU  AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UENDESHAJI WA KESI KUCHELEWA.





HAKIMU mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John  Chaba ameiomba serikali  mkoani  shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama kuu kanda ya ziwa linalojengwa kwa haraka  ilikurahisisha uendeshaji wa kesi hali ambayo itasaidia kesi nyingi kusikilzwa kwa wakati.

Hakimu Chaba alisema hayo  kwenye siku ya madhimisho ya sheria nchi ambapo kimkoa yalifanyika mjini shinyanga katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi kuwa mahakimu mkoani humo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali moja kuu ikiwa ni upungufu wa majengo ya mahakama ya kuendeshea kesi na hivyo kufanya kesi nyingi kurundikana mahakani

WAFUGAJI WILAYANI KISHAPU WATAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA UFUGAJI KUTOKANA NA HALI YA HEWA KUWA YA UKAME

WAFUGAJI WILAYANI KISHAPU WATAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA UFUGAJI KUTOKANA NA HALI YA HEWA KUWA YA UKAME



.
WAFUGAJI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wametakiwa  kubadilika kufuga mifugo wenye uwezo wa kuchukua muda mfupi wa kukomaa na kuweza kuingia sokoni, pia kulichukulia kama zao la biashara  kutokana na hali ya hewa ya ukame katika wilaya hiyo  ikiwemo changamoto ya kukosa   maeneo ya malisho  pamoja na majosho.

Hayo yalisemwa na waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi  Titus Kamani  katika ziara yake aliyotembelea wilayani humo huku akiwaeleza wataalamu na mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku kuwa wakulima wamekuwa wakilima kila eneo na kufanya wafugaji kukosa maeneo ambapo inatakiwa wapatiwe elimu hiyo na kuweza kuepusha migogoro inayoendelea kati ya wakulima na wafugaji nchini.

KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA CHAANZA MAZUNGUMZO NA WAFUGAJI KWENYE VIKUNDII

KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA CHAANZA MAZUNGUMZO NA WAFUGAJI KWENYE VIKUNDII


HATIMAYE kiwanda cha  kusindika nyama cha Triple  ‘S’ kilichopo manispaa ya Shinyanga kimeanza  kuingia mkataba  kwenye   vikundi vidogo vidogo vya wafugaji  vilivyopo mkoani hapa kwa lengo la kuwanyanyua kiuchumi  huku kikiwa kimekwisha pata soko la uuzaji nyama hizo nchi ya Uarabuni.

Hayo yalisemwa na mmiliki wa  kiwanda hicho Salum Seif mbele ya waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi  Titus Kamani  wakati wa ziara yake mkoani humo na kutembelea kiwanda hicho huku akieleza kuwa  anatarajia kukifungua  na kuanza kazi  mwezi Marchi mwaka huu  ikiwa ataanzia  na ng’ombe 50.

Alisema  wamekuwa na maongezi katika vikundi vidogo  vidogo vya ufugaji mkoani hapa  lengo  kuwanyanyua wafugaji hao kiuchumi ,hawakutaka kuwatumia madalali katika minada  ambao wamekuwa wakiwapunja wafugaji na kujinufaisha wenyewe  hivyo wameona watumie mwanya wa vikundi nao wapate faida kubwa na kuondokana na unyonywaji.

UVCCM MANISPAA YA SHINYANGA WAIBUKA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 37 KUSAIDIA WATOTO WALEMAVU

UVCCM MANISPAA YA SHINYANGA WAIBUKA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 37  KUSAIDIA WATOTO WALEMAVU



KITUO  cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) kilichopo Buhangija katika manispaa ya Shinyanga bado kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa  chakula,  vyandarua,vifaa vya kufanyia usafi pamoja na upungugufu wa vitanda ambapo kuna watoto 258 huku kukiwa na vitanda 60.

Hali hiyo ya ukosefu wa vitanda imewalazimu kulala kila kitanda watoto wanne wanne ambavyo pia ni vitanda vya dable deca vinavyofaa kulaliwa na watoto wawili tu.

Hayo yalibainishwa juzi kwenye sherehe za kutimiza miaka 37 ya Chama cha mapinduzi (CCM) wakati umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini  walipokuwa  wakiazimisha sherehe hiyo katika kituo hicho ambapo walifanya usafi katika maeneo hayo walifua nguo za watoto hao, walipanda miti pamoja na kutoa msaada wa chakula.

MBUNGE JIMBO LA KISHAPU ASAIDIA SHULE NNE ZA MSINGI MAJIKO YA GESI

MBUNGE JIMBO LA KISHAPU  ASAIDIA SHULE NNE ZA MSINGI MAJIKO YA GESI





WANAFUNZI wa shule za msingi nne wilayani Kishapu mkoani Shinyanga   wanakabiliwa na changamoto ya utumiaji wa nishati ya kuni   ambapo Mbunge wa jimbo hilo  kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM  Suleiman Nchambi amezindua mradi  wa jiko la kupikia  kwa kutumia  gesi  uliogharimu jumla ya shilingi millioni 80.

  Kabla ya kupatikana kwa  majiko hayo hivi sasa  bado wanaendelea kutumia nishati ya kuni katika shule karibu zote  za msingi ambazo zinatoa huduma ya chakula  kwa wanafunzi hali ambayo ilikuwa ikiwafanya kuacha masomo na kwenda kutafuta nishati ya kuni porini.

BAADHI YA WATUMISHI MANISPAA WADAIWA KUIHUJUMU KWA KUIBA NYARAKA ZA SIRI

BAADHI YA WATUMISHI  MANISPAA WADAIWA KUIHUJUMU KWA KUIBA NYARAKA ZA SIRI








BAADHI  ya watumishi katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wameanza kuihujumu manispaa hiyo kwa kutumia mbinu ya kufungua kesi dhidi ya manispaa hiyo na kuiba nyaraka za ofisi ili kujipatia kipato.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani  naibu mstahiki meya  David Nkulila  alisema  hivi sasa halmashauri hiyo inaandamwa na kesi nyingi za ajabu  zenye lengo la kuihujumu  manispaa kwa  kushindwa kuiba mapato matokeo yake kutumia mbinu hizo.


Alisema manispaa  inataka kuchezewa na watu kwa kuanza kuihujumu kwa kuanzisha makosa yasiyoeleka na kwamba kwa mujibu wa taarifa zinazohisiwa,zinazotia mashaka hujuma hizo zinafanywa na watumishi wa halmashauri hiyo.

“Data zinazohisiwa,zinazosemekana,zinazotia mashaka,watumishi wanahusika,Kesi nyingi sasa zinataka kuiandama halmashauri,mdau yupo anaambiwa anzisha kesi na kesi inaenda kushindikana,mtu huyo anadai alipwe na halmashauri, na hayo madai yanavyosemekana ni mgao wa watu,hizo ni hujuma kwa pesa za wananchi”,alieleza Nkulila.

Akifafanua zaidi alisema menejimenti ya manispaa hiyo imekosa nidhamu ya siri kwani wamekuwa wakitoa nyaraka za siri na kwamba sasa wamebuni njia nyingine ya ulaji kwa kuanzisha kesi badala ya kuwajibika.

Pia   aliwataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa nidhamu,kuridhika na walichonacho,kuwatumikia wananchi na kuwajibika kila mtu kwa nafasi yake kama inavyopaswa kwa kufuata yaliyoelekezwa.

Naye katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi aliwataka watumishi wa umma kutunza siri za ofisi na endapo mtu anaona kazi ya serikali ni ngumu aondoke taratibu badala ya kuchezea nyaraka za serikali.

AJIRA KWA WATOTO IMEPIGWA MARUFUKU LAKINI IPO KATIKA JAMII,TAZAMA PICHA HAPA

Ajira kwa watoto bado inaendelezwa katika jamii kama unavyoona watoto hao wakiwa katika eneo la kituo cha mabasi cha Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakisubiri magari ili wauze karanga 

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA BODI YA RUFAA YA MKOA

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA  AZINDUA BODI YA RUFAA YA MKOA
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga juzi amezindua rasmi bodi ya hospitali ya rufaa ya mkoa huku akiwataka wajumbe wa bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuboresha mfumo wa uendeshaji wa hospitali ya mkoa wa shinyanga.

MCHANGO WA SHILINGI MILLIONI 24 WAKATALIWA NA MADIWANI

MCHANGO WA SHILINGI MILLIONI 24 WAKATALIWA NA MADIWANI

MADIWANI wa halmashauri ya  manispaa ya Shinyanga  wametaka kuondolewa katika orodha ya kuchangia fedha kituo  maalumu cha   kulelea watoto  wenye ulemavu mbalimbali   Buhangija ikiwa katika mchango huo manispaa imelezwa kuchangia kiasi cha shilingi millioni 24.
 Hatua ya kukataa kuchangia imetokana na  kituo hicho kulea watoto wanao toka  maeneo tofauti kama vile mkoa wa Geita,Simiyu, Tabora, Mwanza pamoja na Shinyanga hali ambayo  mikoa hiyo imekuwa haitoi msaada wowote.

MADIWANI WAKATAA UTOAJI WA SHILINGI MILLIONI 24 KWENYE KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU

MADIWANI WAKATAA  UTOAJI WA SHILINGI MILLIONI 24 KWENYE KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU

MADIWANI wa halmashauri ya  manispaa ya Shinyanga  wametaka kuondolewa katika orodha ya kuchangia fedha kituo  maalumu cha   kulelea watoto  wenye ulemavu mbalimbali   Buhangija ikiwa katika mchango huo manispaa imelezwa kuchangia kiasi cha shilingi millioni 24.

 

 Hatua ya kukataa kuchangia imetokana na  kituo hicho kulea watoto wanao toka  maeneo tofauti kama vile mkoa wa Geita,Simiyu, Tabora, Mwanza pamoja na Shinyanga hali ambayo  mikoa hiyo imekuwa haitoi msaada wowote.

 

 Madiwani hao wakiongea katika baraza la madiwani jana  lililofanyika kwenye ukumbi wa mkoa  wamesema  kuwa hawatakuwa tayari kuchangia pesa hizo kutokana na kituo hicho kuwa ndani ya manispaa  na majukumu mengi wamekuwa wakikabiliana nayo,

 

 Naibu mstahiki meya  David Nkulila amesema  kuwa  hali ya kituo hicho  hairidhishi  kutokana na kuachanizwa kwa manispaa pekee kutunza watoto hao  isitoshe imepangiwa  kuchangia shilingi millioni 24 ambapo haiwezekani 

 

 Mkuu wa kituo hicho mwalimu Peter Ajali amesema  kuwa   watoto walipo ni 258 ambapo  walemavu wa ngozi  172,wasioona 48,viziwi  38  ikiwa changamoto kubwa iliyopo ni uhaba wa chakula na deni la shilingi millioni 4.8  kutoka mamlaka ya maji  manispaa (Shuwasa) kudai  kituo hicho.

 

Ambapo suala la deni la maji injinia kutoka shuwasa Slyvesta Malole alieleza madiwani kuwa  deni hilo  linadaiwa tangu mwaka jana  huku akilalamika kutofahamu hali halisi ya maisha ya kituo hicho kwa watoto ikiwa alisisitiza kuwa akaunti inayosoma kwa sasa ibadilishwe na kufahamika na deni hilo lazima lilipwe.

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose  Nyamubi alisema kuwa  kwa upande wa wilaya ya Bukombe mkoa wa  Geita kuna watoto zaidi ya 30 hivyo idara ya maendeleo ya jamii wanatakiwa kufanya mawasiliano ili halmashauri ziwatambue watoto wao pia suala la kuletwa watoto wapya kila siku waletwe kwa utaratibu  utakao ridhia pande zote mbili.

 

MWISHO.

 
KARENY. Powered by Blogger.