Habari za hivi Punde

MBUNGE JIMBO LA KISHAPU ASAIDIA SHULE NNE ZA MSINGI MAJIKO YA GESI






WANAFUNZI wa shule za msingi nne wilayani Kishapu mkoani Shinyanga   wanakabiliwa na changamoto ya utumiaji wa nishati ya kuni   ambapo Mbunge wa jimbo hilo  kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM  Suleiman Nchambi amezindua mradi  wa jiko la kupikia  kwa kutumia  gesi  uliogharimu jumla ya shilingi millioni 80.

  Kabla ya kupatikana kwa  majiko hayo hivi sasa  bado wanaendelea kutumia nishati ya kuni katika shule karibu zote  za msingi ambazo zinatoa huduma ya chakula  kwa wanafunzi hali ambayo ilikuwa ikiwafanya kuacha masomo na kwenda kutafuta nishati ya kuni porini.
 
Awali akizindua mradi huo jana mbunge huyo  amesema  kuwa lengo na madhumuni ya mradi wa jiko la gesi ni kusaidia wanafunzi kuondokana na changamoto ya   muda  mwingi kutafuta kuni kwa ajiri ya kupikia chakula, ikiwa muda huo unakuwa ni wamasomo. 

Nchambi amesema  majiko hayo ya gesi pia yatasaidia kulinda na kuyatunza mazingira kwani wanafunzi pamoja na wananchi wilayani humo wamekuwa wakitumia kuni kwa asilimia kubwa kupikia vyakula vyao jambo ambalo limesababisha wilaya hiyo kuwa katika hali ya jangwa tofauti na hapo awali 

Aidha kwa upande wa  mwalimu wa shule  ya Mayanji  Onesmo Kusekwa  amesema  walikuwa wakipata shida kupikia kuni kwani wakati mwigine hulazimika kukatisha vipindi vya masomo kwa baadhi wanafunzi kwa siku  ilikwenda kutafuta kuni kwenye misitu kwa ajiri ya kupikia chakula.

Naye Afisa elimu wa sayansi, kilimo na afya wilayani humo Winifrida mkama amesema    tatizo la wanafunzi kukatishwa vipindi vyao lilikuwa ni changamoto kubwa  kutokana na alipokuwa akitembelea shule hizo nakukuta baadhi yao wakiwa nje wakitafuta kuni ,huku akiona manufaa ya   mradi huo wa jiko la gesi utaweza kukabili changamoto hiyo. 



0 Response to "MBUNGE JIMBO LA KISHAPU ASAIDIA SHULE NNE ZA MSINGI MAJIKO YA GESI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.