WAMILIKI na mameneja wa shule za msingi,sekodandari na vyuo
binafsi kutoka mikoa nane ya nchini
Tanzania wameitaka serikali kubadilisha
mfumo wa elimu kutokana
na wazazi wanaosomesha watoto
wao kukosa msaada wowote
unaopelekea kutozwa kodi mbalimbali
zenye kiwango kikubwa.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Tamongsco Jerrry Nyabululu kwenye
mkutano wa wamiliki na mameneja wa vyuo
na shule zisizokuwa za serikali kanda ya Magharibi,kanda ya ziwa na kanda ya
ziwa magharibi kwa mikoa ya
Kagera,Mara,Mwanza ,Simiyu,Geita ,Kigoma,Tabora na Shinyanga katika risala yao mbele ya mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa ameambatana na Hadija Mcheka mkurugenzi msaidizi wa usajili kutoka wizara ya elimu.
Hata hivyo waliiomba
serikali ianzishe mjadala wa kitaifa miongoni mwa wadau wa elimu ili
ikiwezekana mfumo wa elimu ubadilishwe
kwani imeonekana kuwa mtoto ambaye anasoma shule binafis hapati msaada wowote kutoka
serikalini kwa kutozwa kodi
nyingi kwa kiwango kikubwa ikiwa wazazi wao ni walipaji wakubwa wa
kodi mbalimbali za serikali kama wazazi
wengine wanaosomesha shule zingine.
Nyabululu alisema kuwa mfumo huo ukiendelea hapo badaye kutajengeka chuki
na matabaka yasiyo ya lazima katika nchi, pia katika suala hili la kodi ndio linalowaongezea
gharama za ada pia kuwa kubwa wazazi wanaosomesha watoto wao kwenye shule binafsi hivyo wanaiomba serikali kuangalia upya
sheria hiyo.
“ changamoto zilziopo
katika shule binafsi kumekuwepo na upandishiwaji wa riba kubwa wanapoomba mikopo
kwenye taasisi za kifedha kwa
kufananishwa na wafanyabishara wakati wao wanachangia suala la elimu na
kuwapatia vijana ajira ,ambapo kwa kanda
hizi tatu zilizopo mafanikio ya
baadhi ya shule zikiwemo Rockeni Hili ya wilayani Kahama na Kwema zimefanya
vizuri kwa kuongoza kitaifa katika matokea yao kwa darasa la saba mwaka
jana”alisema Nyabululu.
Mkurugenzi wa shule
ya msingi na sekondari Kwema Pauline
Mathayo aliyehudhuria mkutano huo alisema kuwa
matarajio wanayoyakusudia ni kuwepo kwa uchocheo mzuri kwa shule
binafsi ambao utawapa fursa ili
kuendeleza kiwango cha elimu, ada zinazotozwa sio kubwa kwa sababu
inaonekana hivyo kwa kutopata ruzuku kutoka serikalini,pia shule hizo
zimeipunguzia serikali mzigo kwa kutoa
ajira kwa vijana.
Naye mwakilishi kutoka wizara ya elimu kwa niaba ya kamishina wa wizara hiyo Mcheka alisema kuwa wizara sasa inampango wa uendeshaji wa
shughuli za kiserikali kwa uwazi ambapo italenga kwenye sera ya elimu ya mwaka 1995
kwa kufanyiwa marekebisho ili
kuweza kuendana na usawa kwa kuondoa changamoto hizo huku serikali
bado inatambua mchango wao wa kuchangia kuondoa umasikini.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Rufunga
alisema kuwa shule hizo zimekuwa
zikitegemea walimu wastaafu na wale wa kutoka nje huku wakiwaacha vijana wenye sifa nao wanaweza, pia tozo la kodi
nyingi na kubwa hiyo iangaliwe upya na
wizara husika huko ni kumkandamiza mzazi wengine wanashindwa kupeleka watoto
wao katika shule hizo kutokana na kiwango cha ada kinacho tozwa ni kikubwa.
Alisema sekta ya elimu ilitoa fursa kwa watu binasfi kutoa elimu ambapo wamekuwa wakijitahidi kunyanyua
kiwango cha elimu nchini hasa kwa mkoa wa shinyanga ambao ulikuwa ukishika
nafasi ya mwisho kitaifa kwa miaka mitatu
mfululuzo huko nyuma mpaka kufikia 2012 ikishika nafasi ya 13 kutoka ya 21 kwa
kusaidiwa na shule binafsi kuongoza kitaifa ndani ya mkoa.
0 Response to "WADAU WA ELIMU WATAKA MFUMO UBADILISHWE ILI KUWEPO NA ULINGANO KWA WAZAZI"
Post a Comment