Habari za hivi Punde

NANI KAFANYA UNYAMA HUU,MTOTO WA MIAKA 3 ANYONGWA NA WATU WASIOJULIKANA

Mtoto Nuru kabla yakufikwa na umauti pichani alipo kuwa na miaka 3.Mtoto huyo anadaiwa kunyongwa Alhamisi iliyopita na kuzikwa katika Makaburi ya Majohe kwa Muslim (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA BILALI) Mmiliki wa Blog ya UJIJIRAHAA.
Nguo ya Mmtoto huyo alio kua ameivaa kabla ya kunyongwa kinyama .
Mama wa marehemu Nuru Mohamedi , ambaye ni Sauda Ally. akiwa amelala kutokana na kuishiwa nguvu mwilini kwa kufikwa na tukio hilo. wakati akiongea na mwandishi wa habari.
Mama wa marehemu Nuru Mohamedi , ambaye ni Sauda Ally (wakwanza kushoto). akiongea kwa shida na mwandishi wa habari, Nyumbani kwa Mama huyo leo Dar es Salaa eneo la Majohe.




Familia ya mtoto Nuru Mohamed (7) pichani juu, wakitoka nje baada ya kumuonyesha mpiga picha wa Gazeti la sehemu iliyopo ndani ya pagala alipouawa mtoto huyo kwa kuwekewa matofari juu ya mtu asiyejulikana Alhamisi jioni eneo la Majohe Kichangani, Ukonga, Dar es Salaam.
Pagala la Nyumba hilo lipo barabarani.

SHULE YA MSINGI YA FILBERT BAYI ILIYOPO KIBAHA IMETEKETEA KWA MOTO.

 apani wanakijiji wanao kaa kalibu na shule hiyo wakishuudia shule iyo ikiwaka moto uku wakishindwa kutoa msaada wowote kutokana na gari la zima moto la mkoa wa pwani kushindwa kufika kutokana na kudai kuwa ni bovu

Mnamo majira ya saa8 usiku wa kuamkia leo Shule ya msingi iyo iliyopo kibaha mkoani pwani maeneo ya kwamatiasi usiku wa kuamkia leo imeungua moto yote.chanzo ikiwa ni shot ya umeme iliyo jitokeza kwenye chumba kimoja cha madarasa hayo na kusababisha madarasa 14 yote kuwaka moto ila cha kumshukulu mungu kuwa wanafunzi wote walipona ila vitu vyao vyote vimeteketea kwa moto mtafuta  mmiliki wa shule hiyo  alisema ni kweli kuwa shule imeungua  na vitu vingi vimeungua ila ni mapema sana kutaja thamani ya vitu vilivyo ungua mpaka tutakapo kaa na kujua ni vitugani na vitu gani

SERIKALI YA CHINA IMELAANI VIKALI KUHUSISHWA TUHUMA ZA NDEGE YA RAIS KUBEBA MENO YA NDOVU

Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.
Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

Lu alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".

Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

"Hata tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"

Alisema nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Kikao hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.

ATHONY LUSEKELO (MZEE WA UPAKO) ADAIWA KUMTISHIA MAISHA KIJANA AMBAYE NI MUUMINI WA GWAJIMA.

ATHONY LUSEKELO (MZEE  WA UPAKO) ADAIWA KUMTISHIA MAISHA KIJANA  AMBAYE NI MUUMINI WA GWAJIMA.
Kijana anayejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, anayedai kutishiwa maisha na Mchungaji Lusekelo Anthon. Akizungumza na waandishi wetu juzi jijini Dar, Robert ambaye shughuli zake ni kuuza chipsi usiku kucha, alisema mara kwa mara Mzee wa Upako amekuwa akimfuata eneo lake la kazi na kumtishia maisha kwa kumwambia maneno mbalimbali yenye vitisho.
“Mara ya kwanza ilikuwa Oktoba 9, mwaka huu saa kumi kasoro usiku. Alipaki gari lake, Land Cruiser (Toyota) nyeusi.
LILE sakata la Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo – Kibangu, Dar, Lusekelo Anthon ‘Mzee wa Upako’ kufyatua risasi mtaani limechukua sura mpya baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina la Robert Lugala, mkazi wa Kibangu kuibuka na kudai alitishiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na mchungaji huyo
Akaniangalia na kuniambia nina macho makali. Akasema ataniombea nitaanguka. Nikamkatalia na kumwambia mimi nina nguvu za Mungu wa kweli, nasali kwa Gwajima kwa hiyo siwezi kuanguka. Aliposhindwa akaahidi kurejea siku nyingine.
“Mara ya pili ni Oktoba 13, mwaka huu saa nne usiku alikuja tena. Mara ya tatu ni Oktoba 15 saa kumi usiku akaanza kugawa pesa kwa madereva wa bodaboda huku akiwaamrisha kuniimbia nyimbo ya kunilaani. Kweli waliniimbia.

WAUMINI WA KANISA LA KKKT WAMETAKIWA KUISOMA KATIBA PENDEKEZO.



WAUMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-KKKT-mission ya Tabora  wametakiwa kuisoma rasimu ya katiba iliyopendekezwa na kuielewa ili waweze kuipigia kura ya maoni.
 
Akizungumza  katika ibada ya Jumapili Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT mission ya Tabora, Patrick Kiula, alisema waumini wamekuwa ni watu wavivu wa kusoma na hivyo kubaki kulalamika tu.

WANAFUNZI WAASWA KUSOMA MASOMO YENYE TIJA YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA.

WANAFUNZI wa shule za Sekondari mkoani Shinyanga wametakiwa kusoma masomo yenye tija yatakayokwenda sambamba na soko la ajira hasa katika wakati huu mgumu wa kuajiriwa.
Kauli hiyo ilitolewa na  mkuu wa
wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwenye maafali ya kumaliza kidato cha nne kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kishimba iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kahama.
Katika mahafali hayo Mpesya aliyewakilishwa na Afisa uhamiaji wilayani humo Zacharia Misana alisema ili kupata ajira ni kusoma masomo ya sayansi yatakayoweza kuwapa ujuzi wa kupata maarifa ya kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira.

UKATILI KWA WATOTO MKOANI SHINYANGA BADO CHANGAMOTO KUBWA INAKADIRIWA KWA SIKU WATOTO 16 MKOANI SHINYANGA HUPEWA UJAUZITO.


Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaendelea  kushika kasi mkoani Shinyanga huku takwimu zikionesha kuwa watoto 16 wanapewa ujauzito kila siku na wengine 500 wakiachishwa shule kila mwaka kutokana na mimba na ndoa za utotoni.

Takwimu hizo zimetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la kiserikali linaloteteaa haki za watoto na wanawake la AGAPE mkoani Shinyanga John Myola (PICHANI)wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga.

KIJANA ALIPUKIWA NA KITU KIDHANIWACHO NI BOMU AKIWA NDANI YA GARI AINA YA FUSO.

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI MSOMAJI WETU.

Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45hrs katika center ya Mhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kumetokea kifo cha mtu mmoja na watu watatu kujeruhiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu kulipuka ndani ya gari. 

Gari  hilo ni lenye namba za usajili  T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) mkazi wa Muhunze.


Inaelezwa kuwa wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mkazi wa Ngara ambaye ni familia ya mwenye gari(aliyefariki dunia)

Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.
Pia mfanyabiashara Donard  Nzugirwa Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi. 
Wengine ni Maganga Pius (14 ), mkazi  wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto,mgongoni na mkono wa kushoto.

Seni  Edward (25 ), ambaye amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo

MKUTANO WA CHADEMA MKOANI SHINYANGA WAHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGIA KURA

Maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo ya jirani waliojitokeza jioni ya leo katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga katika mkutano mkubwa wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa ndugu Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe.Pamoja na mambo mengine viongozi mbalimbali wa Chama hicho walisisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa Desemba 14,2014 huku wananchi wakishauriwa kuachana na propaganda za CCM ambayo imeshindwa kuwaondoa Watanzania katika umaskini,kila siku maisha yanazidi kuwa magumu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga


Viongozi mbalimbali wa Chadema ngazi ya wilaya,mkoa na taifa wakiwa jukwaa kuu jioni ya leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini Hassan Baruti akifungua mkutano leo mjini Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuungana kwa pamoja ili kuing'oa CCM madarakani na kuwapuuza wanaohama chama kwani wanatumiwa na watu wasioitakia mema Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 
Mak
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga  Peter Machanga akiwasalimia wananchi wa Shinyanga huku akiwataka wakurugenzi wa  wilaya kutoa vipeperushi kuhusu taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Wananchi wakinyoosha mikono kufurahia hotuba za viongozi wa Chadema jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mbunge wa Maswa Mashariki Sylivester Kasulumbayi akiongea na wananchi wa Shinyanga leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 
Maelfu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Chadema jioni leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga pia mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema mkoa wa Shinyanga,Rachel Mashishanga akikaribisha wageni wa kitaifa wakiongozwa na mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee.Mashishanga alisema pamoja na serikali kuwapa wakazi wa Shinyanga Waziri wa madini,Stephen Masele lakini mbunge huyo hana msaada wowote kwa wananchi huku akiwataka watu wa Shinyanga kubadilika na kuiunga mkono Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

 Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa Halima Mdee jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Naibu katibu mkuu BAWACHA taifa Kunti Yusuph aliwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwataka kuungana na Chadema ili kutengeneza maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

 Mkutano unaendelea-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 Katibu mkuu BAWACHA taifa Grace Tendega akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema viongozi wengi wa CCM wanajinufaisha wao na watoto wao huku watanzania wakiendelea kuteseka na maisha magumu.Alisem njia pekee ya kuiondoa CCM ni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kupigia kura viongozi wa vyama vya upinzani.Lakini pia aliwakumbusha umuhimu wa kulinda kura zao ili zisiibiwe kama ilivyofanyika chaguzi zilizopita kwani hata mbunge wa Shinyanga Stephen Masele aliiba kura akashinda hivyo sasa wawe makini-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wananchi wakifuatilia mkutano-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 Makamu mwenyekiti BAWACHA  taifa Hawa Waipunga akizungumza mjini Shinyanga ambapo aliwataka wananchi kuunga mkono kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani (UKAWA) anayeonekana kukubalika katika jamii ili kuiondoa madarakani CCM-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
 Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema,pia mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kilimanjaro pia mbunge wa viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro Grace Kiwelu akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono Chadema na UKAWA lakini akawakumbusha kuchangia chama hicho-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapoa alisema kitendo cha CCM kuchakachua kura ulitokana na wananchi kutolinda kura zao na sasa wamejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanaingia ikulu huku akilitaka jeshi la polisi kukaa pembeni ili waishughulikie ipasavyo CCM kwani imechoka na nchi imeuzwa imebaki listi tu.Mdee alitumia fursa hiyo kuwataka wasukuma/watu wa kanda ya ziwa ambao wapo zaidi ya milioni 8 kubadilika kwani wana utajiri wa kila aina ikiwemo migodi 7 mikubwa lakini ni maskini kutokana na kukumbatia serikali isiyojali wananchi wake-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee akiwapokea wazee wawili walioamua kuokoka na kurudi Chadema kwa kile walichodai CCM kutojali wananchi.Mwenye shati la kitenge ni mzee Joseph Rweyemamu(58) aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga kwa muda wa miaka 15,akifuatiwa na mzee Robert Ng'welo(66) aliyekuwa katibu mwenezi wa CCK mtaa wa Jikolile kata yaNdembezi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Mzee Robert Ng'welo akikabidhi kadi ya CCM  kwa HaliamMdee na kupewa kadi ya CHADEMA jioni ya leo.Mdee alisema Chadema ni chama cha watanzania bila kujali huyu ni mzee au la!!-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga

KIJANA MMOJA ANUSURIKA KIFO KWA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA

 Kibaka huyo akiomba msamaha baa

da ya kupokea kichapo kutoka kwa kundi la wananchi waliofulika kwenye ukumbi huo.
Kijana mmoja anayesadikiwa kuwa kibaka  amepokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kibaka huyo kukamatwa nakijaribu kuiba boda boda .
 Mabausa wa ukumbi huo wakimtoa nje kibaka akiwa na Pingu mkononi

ASKARI WA KIKE (WP) AFANYA UKATILI AMKATA VIDOLE MFANYAKAZI WAKE WA NDANI NA KUMNYIMA MSHAHARA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake. 
Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.
AKIONYESHA NAMNA ALIVYOJERUHIWA NA MAMA HUYO

Akizungumza na waandishi wa habari kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.
KARENY. Powered by Blogger.