Hiki ni kituo cha afya cha kilichopo kijiji cha Ikonongo kata ya Salawe kinachokabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.
KITUO cha afya kilichopo kijiji cha Ikonongo kata ya Salawe halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji hali ambayo
inawafanya mama wanaotaka kujifungua
kwenda na maji ikiwemo ndugu wanaowasindikiza kuhaha kutafuta maji umbali wa kilomita mbili ili waweze kufulia
nguo baada ya kuwa wamejifungua hospitalini hapo.
Wakiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea kwenye kituo
hicho baadhi ya mama waliojifungua na
wagonjwa walisema kuwa wanalazimika kwenda na maji kutokana na shida ya
upatikanaji wa maji katika kituo hicho
hata ya kumezea dawa hakuna mpaka
wakanunua ikiwa wengine hawanapesa.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Ikonongo Twiga Mashimba alisema kuwa uhaba wa maji
upo wagonjwa wanateseka hata ya kumezea
dawa shida,mama wanaokuja kujifungua hulazimika kwenda na maji wakati mwingine
walikuwa wakichota kwenye malambo nayo yamekauka hivyo hulazimika ndugu kufuata
umbali wa kilomita mita mbili.
“Licha ya kufuata
huko maji wengine huvizia nyakati za
usiku kwa kujikokoteza kwenye chemchem
yanayotoka polepole ili kupata maji
karibu , jambo ambalo linahatarisha maisha yao kwa usalama ,ikiwa tatizo hili
limekuwa la muda mrefu hivyo tunaiomba serikali kutatua kero hii na kuweza
kunusuru afya za wagonjwa ikiwemo mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu kwa
maji yanayopatikana ni machafu sio salama”alisema mwenyekiti wa kijiji.
Naye muuguzi katika kituo hicho Yusuph Adonji alisema
kuwa uhaba wa maji upo mama wanaokuja
kujifungua hulazimika kuja na maji au ndugu
zao kufuata umbali wa kilomita mbili,maji yanayopatikana kituoni hapo
siyo kwaajili ya wagonjwa au mama wanaojifungua bali ni kwa watumishi kwaajili ya kujisafisha na kufanyia usafi kwa
upigaji deki.
Mganga mkuu katika
kituo hicho dkt Saimon Wilson alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa
maji kituoni hapo huku akieleza kuwa
wamekuwa wakitumia gari kuleta maji
wakati mwingine kumpatia mtu kiasi cha shilingi 5000 na kujaza mapipa
yaliyopo kwani awali kulikuwepo tanki na
mashine ya kusukumia maji, lakini tanki lilihamishwa baada ya
mashine kuharibika.
Kituo hiki kwa siku kinahudumia wagonjwa kati ya 40 hadi 50,kwa mwezi ni watu zaidi ya 25,000 wakiwemo
mamawanaojifungua kutoka vijiji vya
Amani,Songambele,Ikonongo Zonza na Zunzuli ambapo maeneo hayo yote hayana zahanati
na changamoto iliyopo uhaba wa maji hutumia
gari la wagonjwa kama likiishiwa
mafuta hutumia watu kusomba maji na kuwalipa pesa.
|
0 Response to " UHABA WA MAJI KWENYE KITUO CHA AFYA CHA IKONONGO WAWATESA MAMAWANAOKWENDA KUJIFUNGUA KITUONI HAPO."
Post a Comment