Habari za hivi Punde

MKUTANO WA UWT SHINYANGA VIJIJINI WAFANYIKA,WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA MSAADA WA BAISKELI

Ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na wanawake kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zinazokuja za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015

Aliyeshikilia kipaza sauti(mic) ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga bi Helena Daudi akitambalisha wageni walioko meza kuu akiwemo katibu wa ccm mkoa wa Shinyanga Adam Ngalawa(kulia kwake)

Wajumbe wa UWT kutoka kata 26 za wilaya ya Shinyanga vijijini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo,ambapo ajenda mbalimbali zilitolewa na viongozi wakiwemo wabunge wa viti maalum ambao ni Mheshimiwa Azza Hilal na mheshimiwa Lucy Mayenga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora


Mbunge viti maalum Lucy Mayenga akizungumza wakati wa mkutano wa UWT ambapo aliwataka wanawake kuwa wabunifu,wajasiriamali ili kujinyanyua kiuchumi katika familia zao.Pia aliwasisitiza kujenga tabia ya kuhifadhi fedha badala ya kuzitumia kwenye mambo yasiyofaa kwani hali hiyo inachangia kuwepo kwa umasikini katika jamii.

Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azzah Hilal akizungumza kuhusu mchakato wa katiba mpya ambapo alisema mchakato wa katiba ni siasa hivyo wananchi wasidanganyike kwamba kuwa na serikali tatu kutaondoa kero za wananchi kwani zitaongeza gharama hivyo suluhisho la kero za watazania ni serikali mbili pekee,ambazo zitaendelea kuifanya nchi kuwa kisiwa cha amani

Mbunge wa viti maalum Azzah Hilal akiendelea kuzungumza na wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini leo mjini Shinyanga

Baadhi ya wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini

Hizi ni baiskeli 8 kwa ajili ya watu wenye ulemavu zilizotolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azzah Hilal baada ya mkutano wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini kumalizika leo mjini Shinyanga.  
Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azzah Hilal akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu.Mbele wa kwanza kulia ni bi Anna Sengati kutoka Kata ya Tinde,kushoto kwake ni bi Nyanzobe Jimwenda kutoka kata ya Nyamalogo,wa tatu ni Zainabu Juma  kutoka kata ya Itwangi ambao ni miongoni mwa watu wenye ulemavu waliozaliwa nao waliopata msaada wa baiskeli kutoka kwa mbunge leo
Watu wenye ulemavu wakiwa kwenye baiskeli walizopewa na mbunge Azzah Hilal leo mjini Shinyanga

Mtoto mwenye ulemavu akiwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu,ambacho ni miongoni mwa viti vilivyotolewa na mbunge huyo wa ccm shinyanga

Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azza Hilal akishikana mkono wa shukrani na bi Nyanzobe Jimwenda,ambaye ni mlemavu ambaye alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wa baiskeli kwani itamsaidia katika shughuli zake mbalimbali za kujitafutia kipato

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu Medard Hamis mwenye umri wa miaka mitatu.Mbunge huyo alisema ameguswa kwa kiasi kikubwa na watu wenye ulemavu na kwamba anatambua wako wengi wenye mahitaji lakini amewafikia wachache (watu wanane)na kuongeza kwa jukumu la kuwatunza na kuwalea walemavu la watu wote katika jamii na kwamba watu wenye ulemavu hawakupenda kuwa hivyo.

TUME YA UCHAGUZI IMEKUJA NA MFUMO MPYA WA UANDIKSHWAJI MAJINA KWAAJILI YA KUPIGA KURA.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Damian Lubuva  akifungua  semina kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga ambapo alieleza kuwa  kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi, sasa kuna maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura   ambapo zoezi la uandikishwaji utaanza hivi karibuni. Anasema kwa awamu ya kwanza  watatumia mfumo mpya wa teknolojia  ya BIOMETRIC VOTER REGSTRATIO (BVR)  ambao ni mfumo wa kuchukua  au kupima  taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi data kwa njia ya utambuzi,mfumo huo pia hutumika katika kumtambua mtu na kumtofautisha  na mwingine.
 

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini taarifa hiyo kutoka kwenye tume ya uchaguzi huku wakieleza kuwa muda wa siku 14 uliotengwa hautoshi  kwa wananchi kujiandikisha hiyo itakuwa changamoto hasa kwa kuangalia mazingira ya nchi yetu na jiografia yake miundombinu mibovu sanjari na msimu wa kilimo kuanza  wananchi watashindwa kwenda kujiandikisha  kwa muda huo hivyo walimshauri mwenyekiti wa tume kuweza kuangali suala la muda wa kujiandikisha.


Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini  taarifa iliyokuwa ikitolewa na  wawakilishi wa tume ya uchaguzi taifa .


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi taifa Damian Lubuva akiandika hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na waandishi wa habari ambao hawapo pichani.


Afisa elimu mpiga kura taifa  Salvatory Alute akieleza historia fupi ya daftari la kudumu la wapiga kura ambalo  mchakato  wa kuanzishwa kwakwe ulikuwa mwaka 2004 ambapo ulienda sambamba  na matumizi  ya teknoloji  ya ukusanyaji taarifa  za wapiga kura  pamoja na uhifadhi wa taarifa hizi kielektroniki hicho anasema kuwa changamoto iliyojitokeza  kwenye daftari hilo ni baadhi ya watu kukosa majina,viongozi wa vijiji na kata kutopeleka taarifa ya waliofariki hivyo tume imeona kuna umuhimu wa kufanya maboresha  upya na itatoa kadi tofauti na zilizvyokuwa awali  na kutumika kama ilivyokuwa  mwanzo  mpaka pale vitakapo patikana vitambulisho vya taifa.
Mwandishi wa habari gazeti la jamboleo Steven Kidoyai akitoa hoja ya kwanini  mtu hawezi kupiga kura akiwa kwenye eneo tofauti na alipojiandikishia kwani inaonekana kumyima haki mtanzania kupiga kura isitoshe wengine ni wafanyabishara mara nyingi husafiri.
Baada ya kukamilisha semina hiyo fupi kwa waandishi wa habari mwenyekiti aliwashukuru waandishi hao na kuwataka waweze kusambaza habari hizi katika maeneo yote ili wananchi waweze kufikiwa na taarifa za tume,huku akieleza kuwa kumekuwepo na changamoto ya kusema kuwa tume inapendelea chama fulani sio kweli ingawa viongozi wake wanateuliwa na Rais haiwazuii kufanya kazi kwa kuwa huru.


WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI WANAPASWA KUSAIDIWA KWA HALI YOYOTE ILI KUWEZA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZO WAKABILI IKIWEMO MARADHI.Mlemavu wa ngozi anayesumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu ambao umeshindwa kutibiwa kwa ykosefu wa fedha.
 

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA MANISPAA CHA DHARURA MKAGUZI NA MDHIBITI WA HESABU ZA NDANI (CAG) MKOANI SHINYANGA AKIGUNDUA MAMBO MENGI IKIWEM UDANGANYIFU WA MIAKA NA TAREHE ZA KUZALIWA.

Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga  akifungua kikao cha baraza la madiwani cha dharura kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa wa shinyanga.Madiwani wa  manispaa ya Shinyanga  wakifuatlia taarifa inayosomwa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali  mkoa wa Shinyanga Mussa Slyvester.
Mkuu wa wilaya ya  Shinyanga Annarose Nyamubi alisema kuwa iwapo manispaa ya  Shinyanga inataka ujenzi wa ofisi ionyeshe eneo la ujenzi huo sio kuweza kujadili suala ambalo hata  eneo halio.


Naibu katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Projectus Rugonzibwa  akitoa ushauri katika baraza la madiwani.


KAIMU AFISA KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI AKIWA KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA MASHAMBA YA MAZAO MBALIMBALI.

Hili ni moja la zao la ufuta katika shamba darasa lililolimwa na mbwana Shayo katika kijiji cha Kwakonje wilayani Handeni.

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji na ushirika  Yibarila Chiza Kamele akiwa na meneja masoko wa   pembejeo Hamza  Ibrahim wakikagua shamba  lenye zao la ufuta 

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji  na ushirika  akiwa katika moja la shamba lililolimwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora  

Baadhi ya  wakulima wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na mtaalamu Hamza Ibrahim na kuwasihi kutumia mbolea kwa wakati wa kuanza kupanda na baada ya kuchipua  huku akieleza kuwa  shina moja lenye  magunzi mawili ya mahindi yaliyojaa vizuri huweza kutoa robo kilo ya  mahindi,ambapo pia wameelezwa kutokubali kupima mahindi yao kwa gunia pindi wanapouza bali wapime kwa kilo ili waweze kupata faida .

Hapa meneja wa masoko ya pembejeo Hamza Ibrahimu akimuonyesha  a kaimu afisa kilimo mbegu mpya itakayo anza kutumika kwa msimu wa kilimo wa mwaka  huu.


HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI WAKULIMA WAKE WAKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA UZALISHAJI MAZAO NA UVUNAJI IKIWEMO MASOKO.

Kaimu afisa kilimo,umwagiliaji na  ushirika  Yibarila  Chiza akiwaelezea waandishi wa habari ambao hawapo pichani mazao mbalimbali yanayolimwa katika wilaya ya Handeni na changamoto ya ukosefu wa masoko  huku akisikitishwa na baadhi ya wakulima kuendelea kutumia zana ya jembe la mkono na kutofuata kilimo cha utaalamu.

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji na ushirika Yibarila Chiza  Kamele akiangalia shamba darasa la zao la mtama katika kijiji cha Mazingara kata ya Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga.

Chandaru chatumika katika matumzi yasiyo sahihi kwa malengo yake ikiwa vijana hawa walikutwa wakitumia chandarua hicho kuchekecha  zao la ufuta jambo ambalo liliwashangaza waliokuwa wametembelea kijiji  cha Mazingara kata ya mkata  ambapo wanaishi ndani ya kitongoji cha  Mbuzi.

Mwenyekiti  wa kijiji cha Kwachaga Tuliani  katika halmashauri ya wilaya ya  Handeni  Miraji  Ahamed akiwa katika trekta ya kijiji hicho ambalo ndio mradi wa kuongeza kipato ambao  ulimwaji wa ekari moja hukodishwa kwa shilingi 40,000.

KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA TANGA AKIELEZA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA WAHALIFU.

kesho jeshi la polisi mkoani Tanga  limeandaa kikao cha kuongea na wadau wa mkoa huo kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama Kamanda wa mkoa huo  Costantine Massawe amewaeleza waandishi wa habari mkoani humo.

BAADHI YA WAFANYABISHARA WAKUBWA NA WAJASILIAMALI WAKIONYESHA BIASHARA ZAO KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YALIYOFANYIKA JIJINI TANGA KWENYE VIWANJA VYA TANGAMANO.

WAZRI WA AFYA DKT SEIF RASHID AKIFANYA ZIARA KATIKA HOSPITALI YA MKOA,PIA AKIKAGUA WODI YA WAZAZI.


Waziri wa afya  Seif Rashid  akiondoka katika hospitali ya mkoa ,ambapo mganga mkuu wa mkoa Dkt Ntuli Kapologwe wakipeana mikono ya shukurani na kuagana  pembeni ni katibu tawala mkoa Anselmo Tarimo   na Dkt Ramadhani Kaballa.


Waziri wa afya Dkt Seif Rashid akiwa ndani ya wodi ya wazazi wanaojifungua kwa upasuaji na kisha anapata maeleo kutoka kwa  mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa Fredrick Mlekwa


Moja ya waodi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji mkoani Shinyanga ,pia kina mama hawa ni moja ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji .


Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ntuli Kapologwe  akitoa maelezo mbele ya waziri wa afya pamoja na mbunge wa jimbo la Kishapu Selemani Nchambi  na wageni walioambatana na waziri huyo.


Waziri wa afya  Dtk  Self Rashid akiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa  katikati ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang'ombe pamoja  mkuu wa polisi  wilaya ya Shinyanga  Pili Misungwi.


Waziri wa afya akisalimiana na mama aliyekatika wodi ya wazazi tayari amekwisha jifungua kwa njia ya upasuaji hivyo mbunge wa jimbo la Kishapu Seleman Nchambi  akimpa pongezi kwa kujifungua.


Waziri wa afya Dkt  Seif Rashidi  akisalimiana na  baadhi ya madaktari katika  hospitali ya mkoa wa Shinyanga  mara baada ya kuwasili katika ziara yake ya siku moja kushuhudia malalamiko yanayosemwa na wananchi.


WAZIRI WA AFYA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA,AKUMBANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA WILAYA YA kISHAPU KWA KUKOSA HOSPITAL YA WILAYA NA KUGEUZWA KITUO CHA AFYA KUWA HOSPITALI YA WILAYA.


Waziri wa afya Seif Rashid akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga mara baada ya kutembelea wodi ya wazazi waliojifungua kwa njia ya upasuaji na pembeni yake ni mbunge wa jimbo la Kishapu Seleman Nchambi.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akimpatia waziri wa afya Seif Rashidi taarifa ya afya kuhusiana na changamto walizonazo katika wilaya hiyo.


Kituo cha afya kilichopo kata ya Kishapu ndicho kinachotumiwa kama hospitali ya wilaya baada ya kukosa  hospitali ya wilaya ikiwa kinakabiliwa na changamoto za uhaba wa maji,msongamano wa wagonjwa na umbali mrefu wananchi kupata matibabu ikiwemo ukosefu wa dawa na vifaa tiba,ambapo kituo hicho cha afya kilijengwa mwaka 1940 na miundombinu yake imeonekana kuwa chakavu.


Mganga mkuu wa wilaya ya Kishapu Dkt Daniel Nsaningu akisoma taarifa na mikakati iliyopo ya kuondoa changamoto zilizopo katika wilaya hiyo za afya ambapo alieleza kuwa wilaya hiyo haina hospitali ikiwa mikakati iliyopo ujenzi unaendelea na tayari baadhi ya majengo yamekwisha kamilika.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akitoa taarifa ya wilaya yake kuhusu  changamoto ya upande wa afya kwa waziri wa afya Seif Rashid alipokuwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo na kabla ya hapo alisaini kitabu cha wageni ndani ya ofisi hiyo.Waziri wa afya akijibu changamoto zinazowakabili kwa upande wa afya wilaya ya Kishapu ambapo walieleza kukosekana na hospitali ya wilaya imesababisha vifo vinne vya mama wajazito na watoto wapatao 105 kutokana na umbali mrefu wa kupata huduma ya afya wilayani humo.Hili ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi millioni 291 mpaka hapo lilipofikia.Hii ni moja ya wodi ya wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mara baada ya waziri wa afya kutembelea ujenzi huo ambao bado haujakamilika kwa baadhi ya majengo.

KARENY. Powered by Blogger.