BAADHI ya wananchi wa
kijiji cha Songambele kata ya Salawe
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
wamedai kutosomewa mapato na matumizi
ya mradi wa maji ziwa victoria na
kufanya upotevu wa kiasi cha zaidi ya
shilingi millioni nane hali ambayo imefanya mtendaji wa kijiji Paschal Chuma
Kusimamishwa kazi na kamati ya usimamizi wa maji kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo inadaiwa
kuwa kwa mwezi walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi millioni 1.6 katika
kituo kikubwa na kituo kidogo ni kiasi
cha shilingi millioni 1.5, lakini katika akaunti ya benki kulikuwa na kiasi cha shilingi laki tatu ikiwa mradi huo ulizinduliwa mwezi wa tano mwaka 2008.
Wakiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea kijijini
hapo,ambapo baadhi ya wananchi akiwemo mwenyekiti wa tawi Songambele wa chama cha mapinduzi (CCM) Madukwa Gulaka
alisema kuwa changamoto ipo ya
kutoitishwa mikutano ya hadhara na kusomewa mapato na matumizi ya kiasi cha fedha zilizokusanya ikiwa mradi wa maji umeanza siku nyingi.
Gulakwa alisema kuwa
mara baada ya kusimamishwa na
mkurugenzi wa halmashauri Mohamed Kiyungi
jukumu la usimamizi na ukusanyaji
wa fedha lilipewa sungusungu na kwa muda wa siku 27 walifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi
millioni 1.3 ikiwa ndoo moja wanawauzia
wananchi kwa shilingi 25.
Mmoja wa wananchi hao Hermani Sanane alisema tangu kuanzishwe kwa mradi huo hawajawahi
kusomewa mapato na matumizi ya kuhusiana
na fedha zinazokusanywa ikiwa ni haki yao kisheria kuzifahamu lakini kumekuwepo na ubabaishaji
mpaka uongozi kutoka halmashauri uliopata malalamiko hayo na kuyachunguza
ikaamua kuwafikisha mahakamati kamati nzima iliyokuwa na watu wanne.
“Mimi huwa nikisema wananiita muongo mnafiki hakuna mkutano
wa hadhara ulioitishwa na kutusomea
mapato na matumizi,mwenyekiti na mtendaji wa kijiji hujichukulia maamuzi wenyewe mpaka kufikia hasara
ya shilingi millioni nane , na
hapo itakuwa ni zaidi maana mradi huo wa
ziwa Victoria ulizinduliwa mwaka 2008 na kuundwa kwa kamati ya usimamizi na
wananchi”alisema Sanane.
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Songambele Seke Kakonge alisema kuwa sakata la ukusanyaji wa fedha za maji kweli mtendaji wa kijiji huyo
alisimamishwa na mkurugenzi wakiwemo watu wanne kwenye kamati ya maji ambao wamefikishwa mahakamani baada ya
wakaguzi kukagua na kubaini upotevu wa kiasi cha shilingi million nane.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ngassa Mboje
alisema kuwa oparesheni ya kuzikagua
kamati za maji zimeanza na sio kijiji hicho tu bali kwenye maeneo mengi
yalipo na kamati za usimamizi wa maji
kwani kumekuwepo na ubadhirifu mkubwa kupitia kamati hizo ikiwa zinachaguliwa
na wananchi wenyewe,huku mbunge wa jimbo la Solwa Ahamed Salum akisisitiza wananchi kusomewa mapato na matumizi kwa muda
muafa na kuchagua watu
wa kamati wenye uadilifu.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Kiyungi alisema kuwa kweli amemsimamsiha
mtendaji wa kijiji hicho kwa kutosimamia vizuri majukumu yake huku kamati ya watu wanne wa usimamizi wa maji wakifikishwa mahakamani
kwa kutuhumiwa kufanya upotevu wa
fedha,hivyo kilichobainika hapo ni viongozi kutowasomea wananchi mapato na
matumizi ndio maana kumekuwepo na kelele nyingi.
|
0 Response to "KAMATI YA MAJI YAFIKISHWA MAHAKAMANI KIJIJI CHA SONGAMBELE KATA YA SALAWE KWA UBADHIRIFU."
Post a Comment