WAZIRI wa afya na ustawi wa jamii
dkt seif Rashidi amesema kuwa jumla ya shilingi Billioni 1.8 kwaajili ya
kuthibiti ugonjwa wa ebola ambapo wizara
sambamba na hilo imeweka mkakati
unaoendelea wa kuwabaini watu wenye maambukizi ya virus vya ugonjwa huo katika
mipaka ya nchi pamoja na viwanja vya ndege nchini.
Akiongea Jijini Dar es Salaam,
Waziri wa wizara hiyo Dkt. Seif Rashid amesema wizara hiyo imeongeza kiwango
cha ufuatiliaji katika maeneo hayo kwa kuwakagua abiria katika viwanja vya
ndege vya kimataifa hapa nchini ambapo pia wizara imeagiza kifaa cha
Thermoscaner kitakachosaidia kuwabaini wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huo.
Dkt. Rashid amesema vifaa vya
kujikinga na ugonjwa huo vipo vya kutosha kwa ajili ya matumizi kwa watoa
huduma na tayari vimeanza kusambazwa kutoka Bohari ya Dawa MSD kwenda hospitali
za wilaya, mikoa na rufaa nchini.
Katika hatua nyingine, Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya ndani katika
hospital ya rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania Dkt.
Kariameli Wandi ameitahadharisha jamii dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini ambao
imeonekana kushika kasi hapa nchini huku wananchi wakishindwa kutambua dalili
za ugonjwa huo mapema.
Akizungumza na Kurasa leo jijini Dar es Salaam Dkt. Wandi amesema hata matibabu
ya ugonjwa wa homa ya ini yamekuwa ni changamoto kutokana na mgonjwa wa homa ya
ini kulazimika kutumia dawa za kufubaza ugonjwa UKIMWI, ARVs.
|
0 Response to "WIZARA YA AFYA IMEWEKA MIKAKATI YA KUTHIBITI UGONJWA WA EBOLA "
Post a Comment