Dkt Ntuli Kapologwe akiwa na mwandishi wa habari gazeti la habari leo Grace Chilongola
KUFUATIA kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi
jirani ya Rwanda mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt,Ntuli Kapologwe
amewatoa hofu wakazi wa mkoa wa Shinyanga juu ya uvumi wa kuingia kwa ugonjwa hatari
wa Ebola mkoani Shinyanga.
Mganga huyo wa mkoa amewatoa hofu
wananchi kufuatia kuenea uvumi kuwa kuna mgonjwa wa Ebola aliyefikishwa katika
hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutoka moja ya mitaa katika Manispaa ya Shinyanga
aliyefikishwa akitokwa damu puani na mdomoni kisha kuzimia.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu huyo
alieleza hayo leo hospitalini hapo kuwa mgonjwa huyo ambaye alikuwa akitokwa damu
mdomoni na puani alifika hospitalini hapo Agosti 12 mwaka huu na mara baada ya
kufika wauguzi na madakitari walitaharuki.
Mgonjwa alilazimika kupelekwa chumba
cha wagonjwa mahututi (ICU) huku baadhi ya wauguzi na madaktari wakimkimbia
hali iliyotia hofu kwa baadhi ya wahudumu na hata wagonjwa hospitalini hapo.
Hata hivyo Mganga Mkuu huyo lisema hakuna mgonjwa wa Ebola na kuwataka wananchi
waamini hivyo na kuwa uongozi wa mkoa umejipanga kukabiliana na ugonjwa.
Alisema mgonjwa aliyepokelewa ana
matatizo ya kutokwa damu mara kwa mara na kuwa baada ya uchunguzi wa awali
imebainika siyo Ebola.
Hata hivyo katika kukabaliana na
ugonjwa huyo waganga wakuu katika halmashauri zote 6 za wilaya za mkoa
wamekubaliana pindi atakapogundulika mtu mwenye dalili za ugonjwa huo taarifa
itolewe mara moja katika ngazi ya mkoa na kuna timu maalum ya kushughulika na
ugonjwa huo hatari.
Alisema mara baada ya taarifa
kutolewa timu hiyo ndiyo itakayo thibitisha kama kweli mgojwa huyo ana dalili
zote za ebola na taarifa kutolewa.
Mganga huyo pia alisema hospitali
zote katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga zimepewa maelekezo juu ya
kukabiliana na ugonjwa huo.
|
0 Response to "MWENYE DALILI KAMA ZA UGONJWA WA EBOLA AWEKA HOFU MKOANI SHINYANGA"
Post a Comment