KITUO cha afya cha
Ikonongo kilichopo kata ya Salawe
wilayani Shinyanga kinakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo
ukosefu wa huduma ya maji na nishati ya umeme hali ambayo inawalazimu mama wajawazito kutumia tochi ya simu au taa wakati wa kujifunga huku
watoto wanaougua kuchanganywa na wakubwa.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo walimueleza mwandishi wa habari kuwa
kumekuwapepo na tatizo la kupata huduma iliyobora kwani vifaa vya kupimia maradhi yanayowasumbua
hakuna, mama wajawazito kutumia mwanga
wa simu ya tochi wakati wa kujifungua , wamalizapo kujifungua nguo zao hulazimika kwenda kufulia kwenye malambo sehemu ambayo maji hutumiwa na watu wote.
Hata hivyo walisema
wamekuwa wakipata shida ya kubata
huduma katika kituo hicho kwani
hakuna maji mara wanapojifungua hivyo hulazimika kwenda
nayo , hakuna vipimo vya kubaini maradhi
yanayowasumbua ,nishati ya umeme hakuna
kulazimika kutumia mwanga wa tochi ya simu.
Nao wakazi wa kata hiyo Nicodemus
Mashalla na Chausiku Kashindye
walisema kuwa suala hili wanaiomba serikali iwasaidie kwani nyanya za umeme tayari zimepita katika kata hiyo, maji,wodi
ya watoto hakuna inawalazimu
kuchanganywa na wakubwa hali ambayo inawafanya kuhofia afya zao.
Mwenyekiti wa kijiji cha
Azimio Twiga Mashimba
alisema kuwa kituo hicho
kinahudumia vijiji zaidi ya vitano na kata nne ambazo ni Mwakitolyo,mwenge na Salawe ambapo kijiji chake kinaidadi zaidi ya watu 3000
kituo kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wodi ya watoto
ambao hulazimika kuchanganywa na
wakubwa, kina mama hujifungua kwa kutumia mwanga wa simu ya tochi pia uhaba wa
maji upo.
“ Kina hudumia zaidi
ya watu 21,000, awali kulikuwepo na sola ambayo ilikuwa ikisaidia kurahisisha huduma mbalimbali kwa wagonjwa
lakini ilikwisha ibiwa na sasa hakuna sola vifaa vya kupimia maradhi mbalimbali ikiwemo malaria hakuna
,wodi ya kulaza watoto hakuna
inawalazimu kuwachanganya na wakubwa hata
wenye magonjwa ya kifua kikuu na kuhara”alisema .
Naye mkuu wa kituo
hicho Dkt Saimon Wilson alisema
kuwa vifaa vya kupimia baadhi ya maradhi
vipo ila kuna wengine wagonjwa hulazimisha kupata vipimo vyote vingine havipo ila kwa
upande wa kupima malaria kipimo kipo,
suala la kujifungulia tochi ya simu sio
kweli bali wanatumia taa ikiwa sola iliyopo haina nguvu na huzimishwa
ifikapo saa tano usiku.
Kituo hicho
kinakabiliwa na changamto ya maji
na nishati ya umeme, suala la sola
kuibiwa siwezi kulizungumzia mimi
nilikuta sola iliyopo na inatumika mpaka sasa ni hii nayo haina nguvu
huwashwa na kuzimishwa saa tano usiku ,tunatumia
taa za kawaida,pia wagonjwa kwa siku ni zaidi ya 80.
Diwani wa kata hiyo
Joseph Budonho alisema kuwa kweli
kituo hicho cha afya
kinachangamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme na maji ila tatizo hilo linashughulikiwa ikiwa tayari nyaya za umeme zimekwisha wekwa isitoshe kuondoa tatizo la maji lililopo, kuhusu sola ilikuwepo
zamani lakini iliibiwa na kesi bado ipo mahakamani.
0 Response to "KITUO CHA AFYA IKONONGO CHAKABILIWA NA UHABA WA MAJI,NISHATI YA UMEME"
Post a Comment