Habari za hivi Punde

RC-SIMIYU AMEWATAKA WAKUU WA WILAYA WAPYA KUKOMESHA MAHAKAMA ZA KIMILA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka amewataka wakuu wa wilaya wapya kuhakikisha wanakomesha  mahakama za kimila maarufu kama  Ndagashida  ambazo zimekuwa zikitoa adhabu kwa watumishi wa umma  wasio na hatia hali inayopelekea kutokea kwa  mauaji , vilema vya maisha sambamba na kuwafirisi mali zao.
 
Akitoa wito huo jana wakati wa kuapishwa  wakuu hao  ,Mtaka alieleza kuwa  ni muhimu kwa wakuu hao kuzingatia suala hilo  katika wilaya zao kwani  limekuwa likionekana  kuwa ni kikwazo kwa watumishi wa umma ambao hawakubaliani na mila zisizokuwa za kwao.

SHINYANGA BADO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADAWATI 9,545


KARENY. Powered by Blogger.