Habari za hivi Punde

WANAFUNZI WA VYUO MKOANI SHINYANGA WAHIMIZWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO.


Bi Halima Sharif ambaye ni mkurugenzi wa mradi wa Mpango wa uzazi ( Advanced Family Planning) nchini Tanzania unaogharamiwa na mfuko wa  Bill and Melinda Gates kutoka  Marekani na wafadhili mbalimbali na kutekelezwa na nchini Tanzania na Chuo Kikuu Cha John Hopkins cha Marekani akizungumza wakati wa mkutano wao na wawakilishi wa vyuo vikuu mkoani Shinyanga leo katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga. Alisema mradi huo unalenga kuwafikishia elimu ya uzazi wa mpango wanafunzi katika Chuo cha Ualimu cha Shinyanga,VETA ,Musoma Utalii,na Chuo cha Ushirika(MUCCOBS)
Halima Sharif(katikati) akizungumza katika mkutano wa leo uliolenga kuangalia jinsi gani vyuo hivyo vitafanya kazi na kuweka ratiba nzuri kwa wanafunzi wao kujifunza sambamba na kufuatilia maamuzi waliyokubaliana ili chuo cha Uuguzi cha Kolandoto kilichopo katika manispaa ya Shinyanga kiweze kupeleka wataalam wake katika vyuo hivyo kuzungumza nao kuhusu matatizo ya vijana hususani masuala ya afya ya uzazi mpango ambao unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.Wa kwanza kulia ni mkuu wa chuo cha Musoma Utalii bwana Moses Michael,kulia ni mkuu wa idara ya uuguzi Kolandoto Dkt Paschal Shiluka
 Kushoto ni afisa Mawasiliano mradi wa uzazi wa mpango(Advanced Family Planning) unaogharamiwa na mfuko wa Bill & Melinda Gates Institute for Population and Reproductive Health bi Harshi Hettige kutoka nchini Marekani,kulia kwake ni mkurugenzi mkuu wa mradi huo bi Beth Fredrick kutoka Marekani wakiwa katika mkutano na wawakilishi wa vyuo vikuu mkoani Shinyanga wakijadiliana namna ya kufanikisha mradi wa uzazi wa mpango wakitumia wataalam kutoka Chuo cha Kolandoto

Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga ,ambao ni wadau wa mradi wa Uzazi wa mpango katika vyuo vikuu.Manjerenga alisema wao wanajihusisha zaidi na masuala ya vijana na hivi karibuni walifanya utafiti katika elimu ya juu na kubaini kuwa vijana wengi wamekosa elimu ya uzazi wa mpango matokeo yake wanapata maambukizi ya VVU,magonjwa ya zinaa,kupata mimba zisizotarajiwa na utoaji wa mimba kiholela hivyo wakaona umhimu wa kuwapa elimu ya uzazi wa mpango.Kulia kwake ni Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA),Moses Mongo 
Majadiliano yanaendelea
Mkurugenzi mkuu wa mradi wa Uzazi wa mpango katika elimu ya vyuo vikuu bi Beth Fredrick kutoka Marekani akizungumza katika mkutano huo ambapo alipendekeza kila chuo kipange ratiba yake ili kufanikisha mradi huo ambao unalenga kusaidia vijana walioko vyuoni kwani imebainika kuwa wengi wao wanahitaji elimu ya uzazi wa mpango ili kufikia malengo yao
 Mwalimu Christian Balalusesa kutoka chuo cha VETA Shinyanga akiwa ukumbini 
Kushoto mwakilishi wa chuo cha Ushirika cha Muccobs bwana Athumani Mustapha,akifuatiwa na mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Marco Maduhu,Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga Ezra Manjerenga na Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA),Moses Mongo 
 Kushoto ni mkuu wa idara ya uuguzi chuo cha Kolandoto Dkt Paschal Shiluka akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema chuo chake akimejitolea kuwafikia wanafunzi wa elimu ya juu(vyuo vikuu) kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango ikiwa ni sehemu ya kazi ya chuo ambazo ni pamoja na kufundisha,kutoa huduma na utafiti.Dkt Shiluka alitoa wito kwa wanafunzi kujitokeza kupata elimu hiyo pindi mradi utakapoanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka huu

Afisa Mawasiliano mradi wa uzazi wa mpango(Advanced Family Planning) unaogharamiwa na mfuko wa Bill & Melinda Gates,bi Harshi Hettige  akifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinajiri ukumbini leo
Bi Halima Sharif ambaye ni mkurugenzi wa mradi wa Mpango wa uzazi ( Advanced Family Planning) nchini Tanzania unaogharamiwa na mfuko wa  Bill and Melinda Gates kutoka  Marekani na wafadhili mbalimbali na kutekelezwa na nchini Tanzania na Chuo Kikuu Cha John Hopkins cha Marekani akizungumza katika mkutano huo.Sharif alisema wanashirikiana na serikali ya Tanzania,asasi za kiraia,UNA na wadau mbalimbali katika kufanikisha mradi huo katika mkoa wa Shinyanga na mkoa wa Mara na Mwanza
Kushoto ni katibu wa  taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga Yusuph John
 
Katika kufanikisha mradi wa uzazi wa mpango katika vyuo vikuu,PSI watashiriki katika kuhakikisha kuwa vijana wanafikiwa kwani lengo la mradi huo unajihusisha zaidi na utetezi wa mambo ya uzazi wa mpango.Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kuna huduma na uwekezaji katka uzazi wa mpango,kulinda afya ya mama na mtoto.Kupitia mradi huo vijana walioko vyuoni watapata ushauri,taarifa na huduma mbalimbali kuhusu uzazi wa mpango kutokana na mtandao wa vyuo husika kusaidiana kitaaluma.
Picha ya pamoja waliohudhiria mkutano huo

0 Response to "WANAFUNZI WA VYUO MKOANI SHINYANGA WAHIMIZWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.