Habari za hivi Punde
Home »
Uncategories »
MFANYABISHARA HUYU AMEKOSA NINI;WATU WASIOJULIKANA WAMCHINJA
MFANYABISHARA HUYU AMEKOSA NINI;WATU WASIOJULIKANA WAMCHINJA
Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.
Mfanyabiashara
aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya
Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam ameuawa kwa kuchinjwa na
watu wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima
matikiti.
Habari
zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika
eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi
ambazo amekuwa akizifanya tangu afike katika eneo hilo mwaka 2005.
Mke
wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani), alisema siku za nyuma
kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa
ajili ya kulima matikiti.
Watu
hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo hilo na wala hawajulikani
walisema wanatokea Kijiji cha Lusu wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora
walielekezwa kwa marehemu huyo.
Ilielezwa
kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika nyumbani kwa marehemu
Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha
eneo la hekari tatu
Mke
huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale
vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba,
kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.
Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena.
Alisema
siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda
kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba
hilo.
Kwa
mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo
waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda
kuchunga ng’ombe.
“Nikiwa
bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja
anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala
na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura alikataa
kufika kwa awamu nyingine.
“Tulipofika
tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni
kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua
nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.
Mpaka
sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia watu watatu,
wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa
mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha
iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea
mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi
kutofautiana na marehemu.
via>>africanmishe blog
0 Response to "MFANYABISHARA HUYU AMEKOSA NINI;WATU WASIOJULIKANA WAMCHINJA "
Post a Comment