Habari za hivi Punde

WANAFUNZI WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA WAPATA NAFASI WOTE

WANAFUNZI  WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA  WAPATA NAFASI WOTE


MKOA wa Shinyanga umefanikiwa kuingiza kidato cha kwanza wanafunzi wote waliomaliza elimu ya msingi  na kufaulu kwa mwaka jana.

Katika taarifa iliyotolewa  kwa waandishi w a habari jana kaimu afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni afisa elimu  ya watu wazima mkoa huo Yohana Mkumbo amesema  kuwa   zaidi ya  wanafunzi 28,000 kati yao  wanafunzi 13604 walifaulu mtihani huo kujiunga na kidato cha kwanza .

Mkumbo amefafanua  kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana ni 7460 na wasichana ni 6144 na kuongeza kuwa wilaya ya Kahama inaongoza kwa kufaulisha wanafunzi 3868 ikifiatiwa na wilaya ya halmashauri ya mji wa Kahama iliyofaulisha wanafunzi 2953.

Amesema  katika idadi hiyo   manispaa ya Shinyanga  imefaulisha  wanafunzi 2297, wilaya ya Kishapu wanafunzi 2266 huku wilaya ya Shinyanga ikifaulisha wanafunzi 2220 ambapo mkoa umefanikiwa kuwaingiza kidato cha kwanza wanafunzi wote waliofauli kwa asilimia 100.

Aidha amesema  kuwa licha ya mkoa kujivunia hatua hiyo lakini bado unakabiliwa na changamoto ya mwitikio mdogo wa elimu kwa upande wa wazazi hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo ambapo jumla ya wanafunzi 458 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa upande wa changamoto ya uhaba wa  maabara kwenye baadhi ya shule  amesema  kuwa mkoa unafanya jitihada za makusudi ili ifikapo mwaka  2015 mkoa uwe umetatua tatizo hilo kwa shule zote za sekondari ambapo  ikiwa mkoa una maabara 59 huku mahitaji halisi ni maabara 347.
BAADHI YA WAZAZI KATA YA NDEMBEZI WALALAMIKIA UONGOZI WA SHULE

BAADHI YA WAZAZI KATA YA NDEMBEZI WALALAMIKIA UONGOZI WA SHULE


BAADHI  ya wazazi   wa  kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga  wamelalamikia uongozi wa  shule ya msingi Bugoyi (B)   kwa  kitendo cha  kuchangisha shilingi 10,000  kwaajili ya madawati  pindi wanafunzi  walipokuwa wakiandikishwa darasa la kwanza   miaka mitatu mfululizo   iliyopita  lakini matokeo yake   mpaka sasa bado wakiendelea  kukaa chini.


Wakiongea na  mwandishi wa habari   aliyetembelea katika kata hiyo  walisema kuwa  walimu walitilia mkazo wa utozwaji  wa shilingi 10,000 kwaajili ya mchango wa madawati huku wakidai kuwa kama fedha hizo hazitatolewa  mwanafunzi hataandikishwa shule.

WAZAZI NA WALEZI WAKABIDHIWA MADAWATI KWA PESA WALIZOKUWA WAMECHANGA.

WAZAZI NA WALEZI WAKABIDHIWA MADAWATI KWA PESA WALIZOKUWA WAMECHANGA.
Na  Kareny  Masasy
Shinyanga.

WAZAZI na walezi wanaowasomesha watoto wao katika shule ya msingi Bugoyi (A) iliyopo manispaa ya  shinyanga  wamekabidhi jumla ya madawati sabini na mbili kwa ajili ya kuondokana na changamoto ya   kusoma na kuandika  huku wakiwa wamekaa chini na kuwajengea  msingi wa kupata elimu bora. Zoezi hilo limefanyika jana wakati mwenyekiti wa kamati ya shule Peter Sangwa akikabidhi madawati hayo kwa mkuu wa shule hiyo Suleimani Shabani Kipanya na kusema kuwa lengo la kutengeneza madawati hayo limetimia kwa asilimia tisini ambapo walitarajia kukabidhi madawati miamoja kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kukamilisha michango yao kwa wakati.

 kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Suleimani  Kipanya ameshukuru wazazi hao kwa kujali maendeleo ya watoto wao katika suala zima la kuchangia miradi ya maendeleo ya shule hiyo hali ambayo itawafanya wanafunzi hao kuongeza kiwango cha kufauru kutokana na mazingira ya shule kuwa mazuri.

Kipanya amesema  kuwa  zaidi ya madarasa mawili ya wanafunzi katika shule hiyo walikuwa wanasoma huku wamekaa chini  zaidi ya miaka miwili  pia kwa kuanza na  mwaka huu 2014 tatizo hilo limekwisha na hakuna mwanafunzi anayesoma huku akiwa amekaa chini.

Amesema  shule hiyo mpaka hivi sasa itakuwa na jumla ya madawati 300 huku ikiwa na jumla ya wanafunzi 1200 pamoja wanafunzi wa  darasa la awali 126, walimu ishirini na saba wakiume wawili,wakike ishirini na tano na  ilianzishwa mwaka 1975.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mbuyuni Chief Abdalah Sube  ambaye  alishuhudia ukabidhiwaji wa madawati hayo amesema kuwa jambo walilolifanya wazazi hao ni jema huku akiwataka wazazi wengine waige mfano huo kwani kusomesha watoto katika mazingira mazuri ni kuwapatia urithi wa elimu bora.

Sube amesema  baadhi ya wazazi katika shule za msingi
  wamekuwa na tabia ya kuchanganya masuala ya siasa na maendeleo  ambapo suala likipelekwa hivyo linafanya  kushindwa  kukamilisha michango ya madawati kwa ajiri ya watoto wao hivyo kuwafanya wakiendelea kukaa chini pasipo na sababu za msingi.

JESHI LA POLISI LAWATAKA WAUZAJI WA TINDIKARI KUJISAJIRI ILI WAPATIWE VIBALI

JESHI LA POLISI LAWATAKA  WAUZAJI WA TINDIKARI KUJISAJIRI ILI WAPATIWE VIBALI


 Na  Kareny  Masasy
Simiyu.

JESHI la polisi mkoani Simiyu limewataka wauzaji wa tindikari mkoani humo  kuhakikisha wanasajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali, ili kutambulika kisheria sambamba na kupewa utaratibu wa matumizi sahihi ya bidhaa hiyo kwa lengo la kuondoa matumizi mabaya ya bidhaa hiyo ikiwemo kuwadhuru watu.

Mbali na hilo kamanda  wa jeshi hilo Charles mkumbo amewatahadharisha wananchi wote ,kuwa kwa yeyote atakayekutwa na tindikari mtaani, atakamatwa, ikiwa pamoja na kufikishwa mahakani.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda Mkumbo alisema kuwa katika utaraatibu uliowekwa kwa sasa kwa wauzaji wa bidhaa hiyo unamtaka kila muuza tindikari kusajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu,sambamba na kupewa maelekezo ya jinsi ya kutumia au kuuza bidhaa hiyo.

Alisema kwa kila atakayehitaji tindikari kwa matumiuzi sahihi, atatakiwa kuja na mtu au kupewa kibali na mtu atakayetumia tindikari hiyo,kama kwenye magari au pikipiki atatakiwa kuja na fundi makenika dukani kuchukua bidhaa hiyo.

 Katika utaratibu huu ambao ni mpya unao lenga kukomesha matukio ya kumwagiwa watu tindikari,utamtaka muuzaji wa bidhaa hiyo kuhakikisha kila anayenunua tindikari anaitumia katika matumizi sahihi  na  atakayeruhusiwa kutumia au kuja na kibali”alisema.

Alibanisha kuwa  baadhi ya maofisa kutoka ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa iliyoko Jijini Mwanza wamewasili mkoani hapa na watakuwepokwa siku kumi,ili kufanya usajili huo,sambamba na kutoa elimu pamoja na utaratibu wa juu ya matumizi ya tindikari.

Kamanda huyo alieleza  kuwa jeshi la polisi halitakuwa na huruma kwa yeyote atakaye kutwa na tindikari mtaani, kuwa atakatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria  huku akiwataka watumiaji wa bidhaa hiyo kufuata utaratibu huo mpya.

WAKAZI WA KIJIJI CHA NGAGANULWA KATA YA USANDA WAKABILIWA NA UHABA WA MAJI.

WAKAZI  WA KIJIJI CHA NGAGANULWA KATA YA USANDA WAKABILIWA NA UHABA WA MAJI.
Na  Kareny  Masasy
Shinyanga.
WAKAZI  wa kijiji cha Ngaganulwa  kata  ya Usanda wilayani Shinyanga wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa upataji maji safi na salama ya kunywa ambapo wamekuwa wakitumia maji  yaliyojitenga  kwenye mito hali ambayo imeweka kuhatarisha maisha yao kwa kupatwa na mlipuko wa magonjwa kama kuhara na kipindupindu.
Wakiongea na mwandishi wa habari  aliyetembelea kwenye kata hiyo  baadhi ya wananchi  walisema kuwa kilio cha muda mrefu kwa uhaba wa maji kipo ambapo huwalazimu kunywa maji yasiyo salama huku wangine wenye uwezo hununua dumu moja la lita ishirini  shilingi 500.
Wakazi hao walisema kuwa imekuwa ni ndoto kwao kupata maji safi na salama ya kunywa kwa muda wa miaka mingi huku wakiiomba serikali  kuwafanyia ufumbuzi wa kuwachimbia  visima virefu ili waweze kuondokana na changamoto hiyo ikiwa awali waliweza kuchimbiwa visima vifupi ambavyo  havihifadhi maji iwe masika au kiangazi.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho  Mhoja Daudi alisema kuwa   maji salama yanayasikia mjini na sio ndani ya kijiji hicho  hivyo wanaiomba serikali  kuwawezesha  kwa visima virefu au kuwachimbia mabwawa yakuweza kuhimili hata kilimo cha umwagiliaji  kwa  kuweze kupata maji safi na salama na kupunguza tatizo la njaa.
 Naye diwani wa kata hiyo  Ndaji  Al-Jabri  alisema kuwa changamoto ya uhaba wa maji sio tu kwa kijiji hicho bali ni kata yote  ambayo haina mabomba,visima virefu wala mabwawa  bali kulikuwepo na visima vifupi ambavyo hukauka mapema hata kipindi cha masika pia  kunakuwa hakuna maji wananchi kulazimika kutumia maji ya mitoni ambayo sio salama kwa kutembea umbali mrefu kuyapata.
Alisema  tangu mwaka 2007  tatizo hilo lilielezwa na kupangiwa bajeti,kuwekewa michoro  kwaajili ya ujenzi wa mabwawa   kwenye vijiji viwili vya Ngaganulwa na Singita  lakini utekelezaji wake umekuwa ni mugumu  mpaka leo hii michoro hiyo ipo.
“Changamoto ya ukosefu wa maji katika kata yangu ipo, ninacho hitaji hapa ni  visima virefu  ambavyo wananchi wataweza kupata maji safi na salama ya kunywa ,mabwawa ili kuweza kumudu kilimo cha  umwagiliaji  kama hayo yote hatata tekelezwa itabaki kuwa ni tatizo njaa haitakoma kwa wananchi pia maisha yao kuwa hatarini kwa kukosa maji safi na salama ya kunywa”alisema Diwani huyo.

WAGONJWA MKOANI SHINYANGA WALALAMIKIA HOSPITALI YA MKOA KUKOSA DAWA MARA KWA MARA

WAGONJWA MKOANI SHINYANGA WALALAMIKIA HOSPITALI YA MKOA KUKOSA DAWA MARA KWA MARA


Na  Kareny  Masasy
Shinyanga.

 WAGONJWA wenye malaradhi mbalimbali wakiemo wa malaria mkoani Shinyanga  mara nyingi wamekuwa wakikumbwa na uhaba wa dawa  pamoja na vifaa tiba ndani ya hospitali hiyo ambapo hulazimika kwenda kununua katika maduka ya dawa  ya watu binafsi .

Wakiongea na  mwandishi wa habari hospitali aliyetembelea hospitalini hapo  baadhi ya wagonjwa walisema kuwa dawa katika hospitali hiyo zimekuwa zikija kwa msimu  wakati mwingine unakuta dawa zipo ambapo muda mwingine tena ukirudi unaelezwa dawa hakuna.

 Walisema hospitali ya mkoa imekuwa na changamoto ya ukosefu wa dawa mara kwa mara inafikia hatua ya mpaka kubahatisha , kwani zimekuwa  upatikanaji wake wa  msimu wakati  mwingine zinakuwepo na sio dawa  za aina zote isitoshe hata vifaa tiba  kwa wagonjwa wanaofanyiwa  oparesheni  ndogo inabidi vikanunuliwe na mhusika.

Mmoja wa  wagonjwa waliohudhuria hospitalini hapo  Dotto Juma alisema kuwa dawa  kwa sasa zinapatikana sio za aina zote  bali zingine hulazimika kwenda kununua katika maduka ya watu binafsi kama vile vidonge vya watu wenye vifua vya kubana (Athumar)  jambo ambalo linaonyesha  hospitali hiyo kutokuwahuduma zilizojitosheleza.

“Dawa zimekuwa za msimu kuna wakati unapatiwa dawa za aina zote ulizoandikiwa na daktari  lakini kuna wakati hakuna hata  aina moja ya dawa inayopatikana, angalau  kwa wale wanaoumwa malaria  kwao inakuwa  nafuu,magonjwa mengine ikiwemo kubanwa kifua (athumar)   dawa zake zimekuwa adimu  mpaka uende kununua maduka ya watu binafsi  tena kwa gharama kubwa”.

Kwa upande wake  mganga mfawithi wa hospital hiyo Dkt    Fredrik Mlekwa  wakati akiongea na mwandishi wa habari  baada ya kupata malalamiko  ya wagonjwa kukosa dawa ikiwemo vifaa tiba alisema  huchelewa kuwafikia  hali ambayo imepelekewa wagonjwa   kupata changamoto ya ukosefu wa dawa hospitalini hapo.

Hata hivyo Dkt Mlekwa  alisema kuwa  katika suala hilo aliiomba Serikali  kuangalia upya utaratibu wake wa kusambaza madawa pamoja na vifaa tiba viweze kufika kwa muda muafaka,huk akilalamikia kitengo cha  bohari ya dawa  (MSD) kilichopewa jukumu la kusambaza  wamekuwa wakichelewa kufikisha na pia kuleta  vifaa  ambavyo hawaku agizwa..
  “Bohari ya dawa (MSD) ambayo wamekuwa wasambazaji wakuu    uwezo wao wakusambaza dawa ni asilimia 25 au 30 na asilimia inayobaki   hununua dawa kidogo kwa vyanzo vilivyopo hospitalini hapo  ambazo hazitoshelezi mahitaji ya idadi ya wagonjwa wa kila siku wanaohudhuria hospitalini”alisema  Dkt Mlekwa.
MWISHO.
KARENY. Powered by Blogger.