Habari za hivi Punde

MPANGO WA UZAZI BADO NI CHANGAMOTO KATIKA JAMII IKIWA KILA MWAKA NI ONGEZEKO LA ASILIMIA 2.9 NA SASA NI ASILIMIA 27 KITAIFA MALENGO YA 2015 NI KUFIKIA ASILIMIA 60.

Dkt Ntuli  Kapologwe   ambaye ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akifungua semina ya uzazi wa mpango kwa waandishi wa habari wa kanda ya ziwa na magharibi  huku akiwaeleza kuwa waandishi wa habari wakitumiwa kwenye sekta ya afya wanaweza kuleta mabadiliko katika jamii na kupatikana maendeleo huku akieleza kuwa mkoa wa Shinyanga unaunyanyasaji wa watoto wa kike kwa kuwalazimisha kuolewa umri ukiwa mdogo na kufanya idadi ya  mimba za utotoni kuongezeka na kufikia asilimia 59 ambapo alieleza kuwa asilimia 80 ya vifo vinavyotokana na uzazi ni kushindwa kuwahi mapema katika  vituo vya afya pia ongezeko la watoto ni kina mama na baba kutotumia uzazi wa mpango na kufikia asilimia 12.5 kwa mkoa huu.
Waandishi wa habari  ambaye ni  Grace  Chilongola   wa gazeti la habarileo kutoka jijini Mwanza na  Samweli  Mwanga ambaye ni mwandishi wa gazeti  la Mtanzania kutoka mkoa wa Simiyu wakiandika yanayozungumzwa ndani ya semina  ya waandishi wa habari inayohusu uzazi wa mpango.

Waandishi  wa habari  na wawezeshaji kutoka wizara ya afya wakiwa katika picha ya pamoja.


Mratibu wa  afya na mtoto kanda ya ziwa Theresia  Shile  akieleza changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika utendaji wa kazi ikiwemo kuelimisha jamii.

Mwakilishi kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii  kitengo cha mtoto Zuhura  Mbugumi  akiwawezesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani  kuwa vikwazo vinavosababisha   wanawake kushindwa kutumia uzazi wa mpango  ni kutowaruhusu  kujiunga na uzazi wa mpango, kuishi mbali na vituo, dhana na uvumi potofu, ikiwemo mila na desturi.

Mwandishi wa habari  wa gazeti la mwananchi  Jaqueline Masinde  kutoka mkoani Geita akiwa amesimama na kueleza changamoto za baadhi ya wanawake kushindwa kutumia uzazi wa mpango mkoani humo,

Waandishi wa habari wakisikiliza kwa umakini  mada iliyokuwa ikitolewa na mwezeshaji Anna Mwalongo ambaye hayupo pichani.

Mwandishi wa gazeti la habarileo  Grace Chilongola aliteuliwa kuwa mwenyekiti  wa semina hiyo   akiwa amekaa pamoja na mganga mkuu wa mkoa dkt Ntuli Kapologwe.

Berensi  China  mwakilishi wa ITV kutoka mkoani Simiyu  akiongea mara baada ya   mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ntuli Kapologwe  baada ya  kufungua semina hiyo.


Mwakilishi  kutoka wizara ya afya  kitengo cha mama na mtoto Zuhura  Mbuguni akiwasilisha mada  mbele ya waandishi wa habari  ambao hawapo pichani  .

Mwezeshaji Anna Mwalongo  akiwaeleza waandishi wa habari kuwa   zaidi ya wanawake 85,000 hufariki dunia  kwa matatizo yanayohusiana na uzazi wa mpango, ikiwa kwa sasa  ni asilimia 27  kwa watu wanaotumia uzazi wa mpango ambapo alisema kuwa ongezeko hilo ni asilimia  2.7 kwa kila mwaka  na malengo ya  mwaka 2015 ni kufikia asilimia 60, hivyo  watoto  1000 kati ya 51 hufariki dunia pia  ,bado aliwaelimisha  kuwa  wanaotumia njia za asili ni asilimia saba na wanaotumia njia zote ni asilimia 34,waandishi wa habari wanatakiwa  kuwezeshwa  na kutoa taarifa  ili kupatikane mabadiliko          Add caption

Martha  MLimba ambaye ni mratibu wa afya ya mama na mtoto kutoka kanda ya Magharibi kwa mikoa ya Tabora na Kigoma  akiwa na mratibu wa afya ya mama na mtoto kutoka kanda ya ziwa Therezia Shile wakisikiliza kwa umakini mada ya uzazi wa mpango iliyokuwa ikitolewa na mwezeshaji Anna Mwalongo.


Mwezeshaji  Anna Mwalongo akiwa katika uwezeshaji kwa waandishi wa habari kanda ya ziwa na magharibi.

Mwandishi Samweli Mwanga akiwa na Mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio Free Afrika  (RFA)  Debora  Mpagama.Wakwanza ni mratibu wa afya ya uzazi mama na mtoto kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga  katikati ni mwandishi wa habari  Grace Chilongola  pamoja na mganga mkuu wa mkoa Ntuli Kapologwe.

KARENY. Powered by Blogger.