Habari za hivi Punde

WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MAPIGANO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYA ZA KISHAPU NA IGUNGA

WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MAPIGANO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYA ZA KISHAPU NA IGUNGA




WATU watatu ambao majina yao hawajafahamika  wamefariki dunia huku  mfugaji  Gilijisiji Gilawida ambaye alichomwa mkuki na kumjeruhi  vibaya  sehemu za mwili wake  katika mapigano ya wakulima na wafugaji  huko katika kijiji cha  Isakamaliwa  kilichopo mpakani mwa mkoa wa Shinyanga  na Tabora  ambapo mapigano hayo  yalisababishwa na  kugombea  mipaka ya malisho.

Hata hivyo kwa upande wa kata ya Magalata  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga waliopo wafugaji wengi  wa kabila la kitaturu   walinyang’anywa mifugo yao zaidi ya 3000 na wakulima kutoka kijiji hicho kilichopo wilayani Igunga  mkoani Tabora huku ikionekana uchochezi huo kufanywa na wafanyabiashara.

KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...

KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...
KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...: CHANGAMOTO ya kuozesha wanafunzi wa kike mara wanapohitimu darasa la saba   huku wavulana wakiendelea kutumikishwa na shughuli za uchungaji...

KITUO CHA AFYA IKONONGO CHAKABILIWA NA UHABA WA MAJI,NISHATI YA UMEME

KITUO CHA AFYA IKONONGO CHAKABILIWA NA UHABA WA MAJI,NISHATI YA UMEME
KITUO  cha afya cha Ikonongo kilichopo kata ya Salawe  wilayani Shinyanga  kinakabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo ukosefu  wa huduma ya maji na  nishati ya umeme hali ambayo inawalazimu  mama wajawazito kutumia tochi  ya simu au taa wakati wa kujifunga huku watoto wanaougua kuchanganywa na wakubwa.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo  walimueleza mwandishi wa habari  kuwa  kumekuwapepo na tatizo la kupata huduma iliyobora kwani  vifaa vya kupimia maradhi yanayowasumbua hakuna, mama wajawazito kutumia  mwanga wa simu ya tochi wakati wa kujifungua , wamalizapo kujifungua nguo  zao hulazimika  kwenda kufulia  kwenye malambo  sehemu ambayo maji hutumiwa na watu wote.

KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...

KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...
KARENY BLOG: CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KW...: CHANGAMOTO ya kuozesha wanafunzi wa kike mara wanapohitimu darasa la saba   huku wavulana wakiendelea kutumikishwa na shughuli za uchungaji...

WAFANYABIASHARA WALALAMIKIWA KUWA CHANZO CHA UCHAFU WA MITARO NA MAKALVAT

WAFANYABIASHARA  WALALAMIKIWA KUWA CHANZO CHA UCHAFU WA MITARO NA MAKALVAT


WAFANYABIASHARA   mkoani  Shinyanga wamelalamikiwa kuwa chanzo cha kuchafua mitaro na  makalvati  ikiwemo mama lishe  kumwaga maji machafu   hali ambayo imesababisha mitaro hiyo kuziba  na kufanya   wakala wa barabara  tanroad  kuingia  gharama  kubwa ya kuzibua na  kuisafisha .

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake  meneja wa  Tanroad mkoa wa Shinyanga  Philip Witonde  amesema   kuwa  wafanyabishara wanapouza bidhaa zao mabaki  ambayo  ni uchafu hutupwa katika  mitaro  huku mama lishe nao humwaga maji machafu   hali inayopelekea mitaro hiyo kuziba kwa haraka.

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU YA RASMU YA PILI YA KATIBA.

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA ELIMU YA RASMU YA PILI YA KATIBA.





KITUO cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC)  kimetoa elimu ya Rasmu ya pili ya  katiba  kwa wananchi wa kata ya kitangili mjini shinyanga ili wananchi hao wapate kuelewa pamoja na kujitokeza kupiga kura pale Rasmu hiyo itakapo rudishwa mikononi mwa watanzania kama imekidhi vigezo na maoni waliyoyapendekeza

Akitoa elimu kwa wakazi hao kwenye mkutano wa hadhara mwanasheria wa Kituo hicho Jonsoni John alisema kuwa lengo la kutoa elimu  ya Rasmu ya pili ya katiba ni kukuza uelewa kwa watanzania iliwapate kujua nini maana ya katiba hali ambayo itachangia kupata katiba safi ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambayo itaongoza maisha ya watanzania na vizazi vyake vyote.

KARENY BLOG: HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...

KARENY BLOG: HAKIMU  AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...
KARENY BLOG: HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...: HAKIMU mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John  Chaba ameiomba serikali  mkoani  shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo l...

TIMU YA STENDI UNITED NA POLISI MARA ZALETA KIZAA ZAA UWANJA WA KAMBARAGE MKOANI SHINYANGA

TIMU YA STENDI UNITED NA POLISI MARA ZALETA KIZAA ZAA UWANJA WA KAMBARAGE MKOANI SHINYANGA
BAADHI ya  mashabiki  wa timu  ya mpira wa miguu manispaa ya shinyanga akiwemo naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele kunusurika  na wengine  kujeruhiwa vibaya  sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na  vurugu zilizozuka  ndani ya uwanja wa Kambarage  ambapo jeshi la polisi lilianza kurusha mabomu ya machozi .
Mabomu hayo yaliweza kuleta madhara kwa mashabiki  ambapo  mama mwenye ujauzito wa miezi nane aliyefahamika kwa jina la Johari Abdallah (23) mkazi wa ngokolo amelazwa kwa presha  katika hospitali ya mkoa  na mwamuzi  Steven Lutaselwa aliyekuwa  jukwaani akiangalia mpira alijeruhiwa vibaya  sehemu za makalio na hali yake bado ni mbaya yuko chumba mahututi.

KARENY BLOG: HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...

KARENY BLOG: HAKIMU  AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...
KARENY BLOG: HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UEN...: HAKIMU mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John  Chaba ameiomba serikali  mkoani  shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo l...

KUMOMONYOKA KWA MAADILI KUMEFANYA VITENDO VYA RUSHWA KUSHAMIRI NA KUCHAKACHUA MIRADI

KUMOMONYOKA KWA MAADILI KUMEFANYA VITENDO VYA RUSHWA KUSHAMIRI NA KUCHAKACHUA MIRADI



 KUMOMONYOKA  kwa maadili kwa baadhi ya watumishi wa
 umma ni moja ya sababu zinazochangia kukithiri kwa vitendo
 vya rushwa na kuchangia kuongezeka uchakachuaji wa miradi ya
 maendeleo, unaofanywa na wakandarasi kwa kushirikiana na
 wataalamu nakuwataka wanaofanya vitendo hivyo kujitathimini
 wenyewe  kuachia ngazi zao kabla ya kuwajibishwa.
 
Hayo yalielezwa jana na kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na  rushwa (TAKUKURU )mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono, kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo,ambapo alisema viongozi na  mamlaka husika zikiwa zimekaa kimya bila kuchukuwa hatua hali ambayoinatoa picha kuwa watawala hao ni waoga
wakushiriki katika vita dhidi ya rushwa.

UKOSEFU WA MITANDAO YA MAJI SAFI NA SALAMA HUFANYA BAADHI YA MAENEO KUKOSA MAJI.

UKOSEFU WA MITANDAO YA MAJI SAFI NA SALAMA HUFANYA  BAADHI YA MAENEO KUKOSA MAJI.




UKOSEFU  wa mitandao ya maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Shinyanga mjini ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SHUWASA )  hali ambayo inasababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma muhimu ya maji.

 Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA injinia Silvester Mahole wakati akisoma taarifa kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi kwenye uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria katika kijiji cha Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga .

KARENY BLOG: MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NY...

KARENY BLOG: MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NY...
KARENY BLOG: MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NY...: MTOTO   Said Joshua (12) aliyekatwa koromeo  kwa kutumia kisu na baba yake mzazi huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia waka...

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA BUBINZA.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AZINDUA MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA BUBINZA.


SERIKALI mkoani Shinyanga imezindua  mradi wa maji katika kijiji cha Bubinza kata ya mwamashele wilayani Kishapu  ambao utaondoa changamoto  kwa wananchi wa kijiji hicho ambapo walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali yakiwemo magonjwa ya mlipuko  kutokana na kutumia maji yasiyo salama.

Akizindua mradi huo  mkuu  wa mkoa  Ally  Rufunga alisema lengo la serikali hapa nchini hadi kufikia 2025 ni kuhakikisha vijiji vyote vinaondokana  na matatizo ya maji safi na salama hali ambayo itaimarisha uchumi wa nchi kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kutumia muda  wa kutafuta maji  badala yake watafanya  shughuli za kimaendeleo.

JESHI LA JADI LAPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MICHANGO YA MRADI WA MAJI

JESHI LA JADI LAPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MICHANGO YA MRADI WA MAJI


WANANCHI  wa vijiji viwili  vya Mwamalili na Seseko kata ya mwamalili wilayani Shinyanga  wamekabidhiwa  kwa Jeshi la jadi sungusungu ilikukamilisha michango ya mradi wa maji utakao sambaza maji safi na salama katika vijiji hivyo  ambao unatoka ziwa Victoria kupitia tenki la maji (Shuwasa) .

Akilikabidhi Jeshi hilo la jadi kwa wanakijiji hao  mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga wakati akizindua mradi wa maji safi na salama katika vijiji hivyo viwili alisema kutokana na wanakijiji kukaidi agizo la serikali la sera ya maji ya  mwaka 2002, ambayo inasema kila mwananchi anapaswa kuchangia fedha katika miradi hiyo ya maji kuwa hanabudi kutumia mamlaka yake

KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBE...

KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI  MAALUMU YA KUTEMBE...
KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBE...:   Na  Kareny  Masasy Simiyu.   UONGOZI  mkoani  Simiyu umeagizwa kuunda kamati maalumu itakayotembea halmashauri zote mkoani hapa...

SERIKALI IMEANZA KUTEKELEZA KUONDOA KERO YA MAJI WILAYANI KISHAPU

SERIKALI IMEANZA KUTEKELEZA  KUONDOA KERO YA MAJI WILAYANI KISHAPU



WAKAZI wa  wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameanza kutekelezewa  na serikali  tatizo  la ukosefu wa maji  la muda mrefu  kwa kuanza na usanifu wa njia za upatikanaji wa maji  safi na salama  kutoka ziwa victoria  kama maeneo mengine ndani ya mkoa huu yanavyopata maji.

Hayo yalisemwa na waziri  wa maji  Jumanne Maghembe kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya mji mdogo wa maganzo uliohudhuriwa na  baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo huku akisema kuwa  lazima kero hiyo itatuliwe na kufikia mwaka 2015 asilimia 75 wawe wanapata maji.

KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBE...

KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI  MAALUMU YA KUTEMBE...
KARENY BLOG: UONGOZI WAAGIZWA KUUNDA KAMATI MAALUMU YA KUTEMBE...:   Na  Kareny  Masasy Simiyu.   UONGOZI  mkoani  Simiyu umeagizwa kuunda kamati maalumu itakayotembea halmashauri zote mkoani hapa...

MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NYINGI SASA AFARIKI DUNIA

MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NYINGI SASA AFARIKI DUNIA
MTOTO   Said Joshua (12) aliyekatwa koromeo  kwa kutumia kisu na baba yake mzazi huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
 
Mtoto huyo ambaye alichinjwa na baba yake aitwaye Joshua Salvatory (37),fundi baiskeli akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia tarehe 4 mwezi huu katika kitongoji cha Majengo Kaskazini,kata ya Majengo,tarafa ya Kahama mjini  mkoani Shinyanga amefariki dunia jana jioni  majira ya saa kumi kasorobo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula Museven alisema mtoto huyo alifariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama alikokuwa anapatiwa kutokana na koromeo lake kukatwa lote kwa kisu na baba yake kutokana na kile kilichodaiwa kuchoka kumtibu maradhi yaliyokuwa yanamsumbua mara kwa mara. 
 
Kitendo cha kuchinjwa kwa mtoto Said Joshua na hatimaye kusababisha kifo chake kimeibua mambo mengi huku baadhi ya wakazi wa Kahama wakidai kuwa pengine kitendo hicho kinatokana na imani za kishirikina kwa madai kuwa mtuhumiwa alikuwa amemtoa sadaka mwanae kwa waganga ili kupata utajiri.
 
Baadhi ya wananchi walisema Salvatory amefanya kitendo hicho kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason na kwamba alitaka kuchangia damu ya mtoto mdogo akakataliwa.
 
 
“Ndugu mwandishi haya mauaji wengi wanayahusisha na imani za kishirikina kwani hivi sasa jamii ya wana Kahama inakabiliwa na balaa la kuamini vitu na mambo yasiyo na msingi kama lile la kubaini wachawi na imani ya Freemason ambayo haijulikani hata ilikotoka wala msingi wake”,alisema mkazi wa mmoja wa Kahama.
 
Naye  mwenyekiti wa  Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula Museven alisema kifo cha mtoto huyo kinatokana na imani za kishirikina kwani kumekuwepo na taarifa kuwa  Joshua Salvatory alikuwa amemtoa sadaka mwanaye Said Joshua kwa waganga ili awe tajiri.
 
 
Museven alisema  kuwa akiwa bado yu tajiri Joshua Salvatory alikiuka masharti ya mganga wake pesa zikamwishia na mtoto wake akaendelea kubaki katika hali ya kuugua mara kwa mara ikiwemo kuanguka kifafa kila mwezi.
 
“Kitendo cha kufirisika kwa mtuhumiwa na mtoto kuendelea kuugua kifafa,nadhani ndicho kimemfanya ammalize tu mtoto huyu,taarifa za kwamba ana matatizo ya akili siyo kweli kwani mtuhumiwa kwanza na mwizi mzuri tu,amefikishwa polisi siku za nyuma kwa wizi,sasa inakuwaje mtu mwenye matatizo ya akili aibe?”,alieleza Museven.
 
 
Katika hatua nyingine Museven kabla ya kumkata koromeo mwanaye pia mwezi Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja mke wake Mariam Idd lakini yeye (Museven) akawasuruhisha na mke wa mtuhumiwa kuamua kumkimbia mme wake kwa hofu ya kuuawa na mwanamme kubaki na mtoto Said Joshua.
 
 “Haikuishia hapo siku chache tu mtuhumiwa pia alitaka kumchinja mtoto wa jirani yake kwa madai ya kwanini huwa anacheza na mwanaye ,kama mwenyekiti wa kitongoji nikaingilia kati kitendo hicho kilimuudhi Salvatory na kutaka kunichinja pia,nikaita polisi akakamatwa,na ndiyo tuhuma iliyompeleka gerezani kwa kipindi cha miezi miwili,na mtoto kurudi kwa mama yake”,alieeleza Museven.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na  kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa  alikwisha achana na mwanamme huyo siku nyingi.

“Baba wa mtoto huyu siku za nyuma,alikuwa akimchukua mwanangu mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake,mimi nilishaachana naye, huwa anamrudisha,na amekuwa akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya”,alifafanua mama huyo.

 

KARENY BLOG: MTOTO ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI KISA ...

KARENY BLOG: MTOTO ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI KISA ...
KARENY BLOG: MTOTO ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI KISA ...: MWANAFUNZI  wa darasa la tatu katika shule ya msingi Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga Said Joshua (12) amenusurika kufa baada y...

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YAWAHUKUMU WATU WAWILI KIFUNGO CHA ZAIDI YA MIAKA 100

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YAWAHUKUMU WATU WAWILI KIFUNGO CHA ZAIDI YA MIAKA 100

MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga imewahukumu wakazi wawili wa kijiji cha  Shatimba wilaya ya shinyanga  mkoani hapa  kwenda jela  kwa miaka  242 baada ya kupatikana na makosa matatu ambayo ni  ubakaji , wizi wa kutumia silaha na kujeruhi.

Waliohukumiwa ni Mathias Kaloga (40) Jamesi Moshi (35) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho  na kutenda  makosa hayo October 10, 2012.ambapo walivamia nyumbani kwa malamikaji wa kwanza Tesha Jidomela wakiwa na bunduki na mapanga ,walimjeruhi na kuiba simu tatu za mkononi.

WAZEE KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI BURE

WAZEE KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI BURE


HALMASHAURI ya wilaya ya shinyanga  kwa kushirikiana na shirika lisilo lakiSerikali  la Tawlae  linalotetea haki za wazee mkoani Shinyanga  imeandaa mkakati madhubuti wa kutengeneza vitambulisho ambavyo watapatiwa wazee wasiojiweza  huduma bure za kijamii ikiwemo ya matibabu.

Akizungumza mjini shinyanga kwenye kikao cha kufanya tathimini na maboresho ya mkakati  wa kuwasaidia wazee kupata huduma hizo bure, mkurugenzi wa Halmashauli hiyo Mohamedi Kiyungi alisema  mrejesho wa kikao cha kwanza kilichofanyika Aprili mwaka jana  wamefanikiwa kuorodhesha majina ya wazee katika kata  16  zilizolengwa  na ambazo zitaanza na mpango huo.

WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO ZAIDI HUPATA UPUNGUFU WA DAMU NA MALARIA

WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO ZAIDI HUPATA UPUNGUFU WA DAMU NA  MALARIA
CHANGAMOTO kubwa inayowakumba  watoto waliochini ya umri wa miaka mitano  kiafya ni upungufu wa damu na ugonjwa wa malaria  hali ambayo inapekekea kuleta msongamano wa wagonjwa katika kituo cha afya kilichopo kata ya Iselamagazi tarafa ya Nindo wilayani Shinyanga.

Akiongea na waandishi wa habari waliokuwa wametembelea  katika kituo hicho mganga mkuu wa  Dkt Heleni Kaunda  aliwaeleza kuwa msongamano wa wagonjwa pia unaletwa kwa kuhudumia  wagonjwa ambao wanahitaji matibabu zaidi kutoka zahanati sita zinazozunguka kata hiyo.

Dkt  Kaunda alibainisha kuwa watoto waliochini ya  umri wa miaka mitano  zaidi ndio wamekuwa wakipata ugonjwa wa malaria ya homa kali pamoja na upungufu wa damu hali ambayo inaleta msongamano  ikiwemo kuhudumia kwa masaa 24.

CHANGAMOTO KWA WATOTO WENYE VVU NA WENYE KUISHI MAZINGIRA HATARISHI

CHANGAMOTO KWA WATOTO WENYE VVU NA WENYE KUISHI MAZINGIRA HATARISHI
CHANGAMOTO  kubwa inayowakabili watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi  pamoja na wale wenye kuishi na maambukizi ya virusi vya  ukimwi ni  kwa ukosefu wa mahitaji muhimu wanaopaswa kuyapata kama watoto wengine , lishe duni , pia  walezi au wazazi kutokuwa na kipato huku wengine wakiwatelekeza kwa makusudi.

Hayo yalisemwa na mwalimu  Johari  Salum wa kituo cha kulelea watoto  hao cha (ECD) chini ya ufadhili wa shirika la Lara Foundation International  kilichopo kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga  chenye watoto 45, wakati wa mfanyabiashara Oscar Kaijage  alipotembelea  kituoni hapo akiwa ameambatana na mke wake  kwaajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali  yakiwemo madaftari na kalamu.

VIONGOZI WA VIJIJI WILAYANI KISHAPU WAAGIZWA KUSIMAMAIA MAZINGIRA IKIWEMO UFUGAJI WA NYUKI KATIKA MISITU.

VIONGOZI WA VIJIJI  WILAYANI KISHAPU WAAGIZWA KUSIMAMAIA MAZINGIRA IKIWEMO UFUGAJI WA NYUKI KATIKA MISITU.


VIONGOZI  wa vijiji wote wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wameagizwa kuhakikisha wanasimamia mazingira ipasavyo, na wahakikishe miti  haikatwi kiholela ili kuimarisha ufugaji wa nyuki katika misitu hiyo. 

Agizo hilo limetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Willison Nkhambaku wakati wa uzinduzi wa mizinga ya nyuki uliofanyika katika kijiji cha Nyasamba kata ya Bubiki wilayani humo ambapo alisema atakaebainika anakata ovyo achukuliwe hatua kali za kisheria.

MTOTO ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI KISA KUCHOKA KUMTIBU MARADHI YANAYOMSUMBUA.

MTOTO ANUSURIKA KUCHINJWA NA BABA YAKE MZAZI KISA KUCHOKA KUMTIBU MARADHI YANAYOMSUMBUA.


MWANAFUNZI  wa darasa la tatu katika shule ya msingi Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga Said Joshua (12) amenusurika kufa baada ya kutaka  kuchinjwa kwa kutumia kisu na baba yake mzazi kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa kumtibu kwa   maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Tukio hilo limetokea jana saa 11 alfajiri katika kijiji cha Majengo ,kata ya Majengo,tarafa ya Kahama mjini ambapo mwanamme aitwaye Joshua Salvatory(37) mkazi wa Majengo,fundi baiskeli akiwa nyumbani kwake alimkata kisu shingoni mtoto huyo na kuathiri koromeo lake.

IDARA YA UHAMIAJI MKOANI SHINYANGA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI.

IDARA YA UHAMIAJI MKOANI SHINYANGA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI.

IDARA ya uhamiaji mkoani Shinyanga  inakabiliwa changamoto wa vitendea kazi kwa kukosa  magari ya kutosha ,kutokuwa na sare maalumu zinazoendana na mazingira ambazo zinaweza kuhimili mazingira ya kikazi na hivyo kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo ya kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingi
 
Hayo yalibainishwa  na mtumishi wa Idara ya uhamiaji mkoani humo Herieti Mayunga wakati akisoma Risala  kwa mgeni Rasmi katika sherehe ya kuuaga mwaka 2013 na kuukalibisha mwaka 2014 iliyofanyika mjini shinyanga na kuhusisha wakuu wa idara ya uhamiaji kutoka mikoa ya Geita,Mwanza, simiyu pamoja na Mara.
 
Herieti alisema licha ya upungufu wa vitendea kazi hivyo , pia idara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali likiwemo suala la uhaba wa watumishi ambapo idara hiyo kwa mkoa mzima inawatumishi 33, pamoja na kukosa ushirikiano wa kutosha kwa wananchi wa kuwafichua wahamiaji hao haramu
 
Naye Afisa uhamiaji mkoa wa shinyanga AnnaMaria Yondani aliwataja wahamiaji haramu waliokamatwa mkoani humo, na wanaoishi kinyume na sheria kuanzia kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana ni wahamiaji  162, walioondoka kwa OD 19,  PI 75 , waliofungwa 30, waliochiwa huru na kuambiwa kufuata taratibu za nchi 32 na kesi zinazoendelea 6.
 
Pia alitaja sababu zinazochangia kuongezeka kwa wahamiaji haramu mkoani humo ni kutokana na uwepo wa migodi ya madini ya Dhahabu , Almasi, kilimo cha Pamba, Tumbaku, pamoja na Barabara kuu iendayo Rwanda, Burundi, Uganda, Kongo DRC, hali ambayo husababisha ongezeko la watu wengi hasa katika wilaya ya kahama ambayo imekuwa ikikithili kwa wahamiaji hao.
 
Kwa upande wake mgeni Rasmi mkuu wa mkoa shinyanga Ally Rufunga aliahidi  suala la upungufu wa vitendeakazi atalifikisha katika ngazi ya taifa kwani hilo lipo nje ya uwezo wake huku akiwataka watumishi wa Idara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu za nchi  pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
 
‘’Idara ya uhamiaji huwa inakabiliwa na rushwa , hasa pale mnapo wakamata wahamiaji haramu kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wa Somali wamekuwa wakiwapa fedha na kuwa achia waendelee na shughuliza zao, hivyo na toa onyo kwenu atakaye bainika kuhusika na vitendo vya rushwa sheria itachukua mkondo wake” alisema Rufunga.
 
Akizungumza katika sherehe hiyo Afisa uhamiaji mkoa wa Mwanza Remegius Pesambili alitoa ushauri kwa Idara ya uhamiaji  licha ya mapungu waliyonayo bali washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha wanatokomeza au kupunguza wahamiaji haramu mkoani humo.
 
Alisema wahamiaji hao wanapokithiri hapa nchini huweza kusababisha kuwepo kwa matukio ya kigaidi kwani asilimia kubwa ya matukio hayo hutokana na watu kutoka nchi za jirani.
 

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO YAPUNGUA NA KUFIKIA ASILIMIA 5.6 MKOANI SHINYANGA

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO YAPUNGUA NA KUFIKIA ASILIMIA 5.6 MKOANI SHINYANGA


WANANCHI  mkoani  shinyanga  wametakiwa kuondokana na  unyanyapaa kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi  ikiwemo mama wajawazito kuhudhuria  katika kliniki  kwa  kupima afya zao na  kuondoa maambukizi ya  mama kwenda kwa mtoto ambapo kiwango mpaka sasa kimefikia asilimia 5.6.

Hayo  yalisemwa na  mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga  kwenye uzinduzi wa  kampeni ya utokomezaji  wa maambukizi  virusi vya ukimwi  toka kwa mama  kwenda kwa  mtoto huku akisema kuwa  maambukizi  hayo tangu mwaka 2011 yalikuwa asilimia 26.
KARENY. Powered by Blogger.