Habari za hivi Punde

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YAWAHUKUMU WATU WAWILI KIFUNGO CHA ZAIDI YA MIAKA 100


MAHAKAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga imewahukumu wakazi wawili wa kijiji cha  Shatimba wilaya ya shinyanga  mkoani hapa  kwenda jela  kwa miaka  242 baada ya kupatikana na makosa matatu ambayo ni  ubakaji , wizi wa kutumia silaha na kujeruhi.

Waliohukumiwa ni Mathias Kaloga (40) Jamesi Moshi (35) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho  na kutenda  makosa hayo October 10, 2012.ambapo walivamia nyumbani kwa malamikaji wa kwanza Tesha Jidomela wakiwa na bunduki na mapanga ,walimjeruhi na kuiba simu tatu za mkononi.



Akiendesha mashitaka hayo jana katika mahakama ya wilaya ya shinyanga mwanasheria wa serikali Salome mbuguni aliambia mahakama hiyo kuwa baada ya washitakiwa hao kufanikiwa zoezi la kupora mali hizo ambapo pia waliwabaka wake za walalamikaji kwa kubadilishana zamu kwa zamu.

Pia usiku huohuo walivamia katika mji mwingine wa Sai Jidomela ambaye ni mdogo wake wa mlalamikaji namba moja walivamia kwa silaha hizohizo na kufanikiwa kupora simu moja ya mkononi na kisha kuondoka na sh, elfu 57 ambazo zilikuwa kwenye mfuko wa suruali yake.

Mbuguni alisema  kosa la kwanza la kuiba kwa kutumia silaha kila mshitakiwa atatumikia jela miaka 60 kutokana na kuvamia sehemu mbili ,ambapo shemu ya kwanza ni miaka 30 kwa kila mmoja, kutokana na kifungu cha sheria no.287 (a)16 cha kanuni ya adhabu, kuvamia na kujeruhi ambapo ni kinyume cha sheria no.225(a)44 kila mtuhumia ni miaka 2,na kulipa faini ya laki mbili.

Aliongeza kuwa kosa la kushambulia,kuzuru na kubaka ni kinyume cha sheria namba 241 kifungu cha 16 ambapo watuhumiwa wote wanatakiwa kutumikia jela miaka 60 kwa kila mmoja kutokana na kuwabaka wake wa walalamikaji wote wawili kwa zamuzamu.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya shinyanga Thomsoni Mtani alisema kuwa kutokana na mashitaka hayo mtuhumiwa wa kwanza atatumikia jela miaka 122 na mtuhumiwa wa pili atatumikia jela miaka  120, jumla ya miaka yote ni 242, pamoja na viboko kumi na mbili kwa kila mmoja kuingia na kutoka.

0 Response to "MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YAWAHUKUMU WATU WAWILI KIFUNGO CHA ZAIDI YA MIAKA 100"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.