Habari za hivi Punde

WAZEE KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI BURE



HALMASHAURI ya wilaya ya shinyanga  kwa kushirikiana na shirika lisilo lakiSerikali  la Tawlae  linalotetea haki za wazee mkoani Shinyanga  imeandaa mkakati madhubuti wa kutengeneza vitambulisho ambavyo watapatiwa wazee wasiojiweza  huduma bure za kijamii ikiwemo ya matibabu.

Akizungumza mjini shinyanga kwenye kikao cha kufanya tathimini na maboresho ya mkakati  wa kuwasaidia wazee kupata huduma hizo bure, mkurugenzi wa Halmashauli hiyo Mohamedi Kiyungi alisema  mrejesho wa kikao cha kwanza kilichofanyika Aprili mwaka jana  wamefanikiwa kuorodhesha majina ya wazee katika kata  16  zilizolengwa  na ambazo zitaanza na mpango huo.


Kiyungi alisema mkakati huo utawalenga wazee  kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea ambapo mara baada ya kuorodheshwa majina yao watapigwa  picha na kutengenezewa vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia kupatiwa matibabu bure popote pale na kuondoa changamoto ambazo zinawakabili


‘’Shirika hili la TAWLAE liliwasilisha maombi yake katika halmashauli yetu kuwa linataka kushirikiana na serikali katika kuhakikisha lina waboreshea wazee wetu mazingira mazuri katika upatikanaji wa huduma kwa jamii, kutokana na wazee hao kusahaulika katika jamii na kuonekana hawana thamani tena,ombi ambalo tuliafikiana nao na kuahidi kutoa ushirikianao” alisema kiyungi.

Hata hivyo alibainisha kuwa kutokana na halmashauli kuwa na watendaji wa vijiji,  kata, hali ambayo  wameiona  kutakuwa na mchango mkubwa  katika kufanikisha mkakati huu, wakuwatoa wazee  kwenye shida ,hivyo kuwajengea miundo mbinu mizuri ,ambayo itakuwa faida.

Kiyungi alisema mbali na huduma hiyo ya matibabu bure ambapo pia watapatiwa huduma zingine kama vile maji, kilimo ,usafiri ,kusamehewa kodi za mapango, kupewa mbengu za mazao ya mtama bure pamoja na kupewa kipaumbele katika taasisi za kifedha kupitia vitambulisho vyao,

Naye mratibu wa shirika hilo la TAWLAE ambalo linahusika na kutetea haki za wazee hapa nchini,  katika tawi la shinyanga mjini Elisanya Nko alisema mkakati huo wa kusaidia wazee ni endelevu ambapo watazunguka katika wilaya zote za mkoa huo huku wakishirikana na serikali pamoja na shirika la Help Age International katika kuhakikisha wazee wanapatiwa huduma bure.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya shinyanga  Edward Lupimo alisema mkakati huo usiishie kwenye makablasha tu bali utekelezwe kwa vitendo ,huku akitoa rai kwa wananchi kuwa na tabia ya kujenga vitega uchumi ambavyo vitawasaidia kujipatia kipato wakati wa uzee na kuondokana na zana ya kuwa tegemez

0 Response to "WAZEE KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI BURE"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.