Akiongea na waandishi wa habari waliokuwa wametembelea katika kituo hicho mganga mkuu wa Dkt Heleni Kaunda aliwaeleza kuwa msongamano wa wagonjwa pia unaletwa kwa kuhudumia wagonjwa ambao wanahitaji matibabu zaidi kutoka zahanati sita zinazozunguka kata hiyo.
Dkt Kaunda alibainisha kuwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano zaidi ndio wamekuwa wakipata ugonjwa wa malaria ya homa kali pamoja na upungufu wa damu hali ambayo inaleta msongamano ikiwemo kuhudumia kwa masaa 24.
“Msongamano wa wagonjwa upo,wengi wamekuwa wakipelekwa rufaa kwa malaria kali na upungufu wa damu ikiwa zaidi watoto kwa siku wawili mpaka wanne, pamoja na akina mama wanaoshindwa kujifungua “alisema Dkt Heleni.
Pia Shija Ramadhani mkazi wa kijiji cha Iselamagazi alionekana kuhudhuria katika hospitali ya mkoa huku akiwa amembeba mtoto wake mgongoni baada ya kuulizwa na mwandishi alidai kuwa mtoto huyo alilazwa katika kituo cha afya lakini hali ilionekana kuwa mbaya kutokana na kutopatiwa dawa tangu alazwe.
Naye afisa mtendaji wa kata Paul Kulwa alisema kuwa kata ya Iselamagazi inazahanati mbili ambazo zipo katika vijiji vya Mwamakaranga na Homango ambapo inahudumia zaidi ya vijiji sita pamoja na kata ya Lyabusalu mpya yenye vijiji saba ikiwemo vijiji vya jirani ya wilaya ya Kishapu na mkoa wa Mwanza.
Hata hivyo alisema kuwa kata hiyo inaidadi ya watu zaidi ya 20,000 vituo vya kutolea huduma ya afya vichache na upatikanaji wa dawa unakuwa wa shida kwani huja chache ambazo hazitoshelezi idadi ya watu waliopo na wanaotoka nje ya kata hiyo.
Aidha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwamakaranga Rafael Paul na shija Masalu walisema kuwa upatikanaji wa huduma umekuwa shida ziku zote kutokana na msongamano wa wagonjwa katika zahanati na kituo cha afya ikiwemo kukosa madawa hivyo hulazimika kwenda kununua dawa.
Changamoto hiyo imetokana na zahanati pamoja na vituo vya afya hasa vijijini kutokuwa nadawa hata kama zikiletwa hazikidhi matakwa ya idadi ya watu waliopo kwenye eneo husika ,ambapo jamii huamua kwenda kununua kwenye maduka binafsi huku zingine zikiwa feki.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dtk Fredrick Mlekwa alisema kuwa kweli wagonjwa wanaotoka nje walio wengi ni kutoka maeneo ya vijijini,wakifika hapa wanakuwa na hali mbaya kiafya hiyo inatokana na uelewa mdogo wa wananchi hao au huduma zinazotolewa katika vituo vya afya na zahanati pamoja na za watu binafis kuwa na kiwango kisichokidhi kiafya kwa kujali maslahi yao.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema kuwa mkoa huu umetenga jumla ya shilingi billion 3.5 kwaajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kupata afya bora katika jamii ambapo mpaka sasa ni asilimia 70 ya vituo vya afya na zahanati ni asilimia 60 huku halmashauri mbili zikiwa na hosptal.
0 Response to "WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO ZAIDI HUPATA UPUNGUFU WA DAMU NA MALARIA"
Post a Comment