Habari za hivi Punde

WATU 40,364 WAMEPIMWA,1,871 WAMEBAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VVU

Kati ya  watu 40,364 waliojitokeza kupima  afya kwa hiari katika halmashauri Msalala  mkoani Shinyanga   1,871 wamekutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Mratibu wa ukimwi wa halmashauri  hiyo Jackson Faustine  anasema kuwa  watu hao walijitokeza kupima afya kati ya Januari hadi Novemba  2015.

DC SHINYANGA ATOA AGIZO MHANDISI WA MANISPAA KUWEKWA RUMANDE

MKUU wa  wilaya  ya  Shinyanga  Josephine  Matiro  ametoa  amri  ya kumuweka  ndani  mhandisi  wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga  Saimon  Ngagani ,  kutokana  na kukaidi  agizo lake  la kufanya  maandalizi  mapema  ya  shughuli  za  kuchimbia  mapipa  ya  kuweka  taka  nyepesi  katika  maeneo  mbalimbali  ya manispaa  hiyo. 

Akizungumza na  baadhi ya   wananchi  katika  stendi  ya  mabasi  ya zamani  wakati wa kuweka mapipa hayo ,mkuu wa wilaya alisema zoezi  hilo lilitakiwa lifanyike saa  1.30 asubuhi lakini wamelazimika kufanya saa 3.30  kutokana  na uzembe uliofanywa na injinia  ambaye alipewa  kazi ya  kuandaa  kokoto  na  mchanga mapema matokeo  yake  hakufanya  hivyo.
KARENY. Powered by Blogger.