MKUU wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro
ametoa amri ya kumuweka
ndani mhandisi wa ujenzi wa manispaa
ya Shinyanga Saimon Ngagani ,
kutokana na kukaidi agizo lake
la kufanya maandalizi mapema
ya shughuli za kuchimbia mapipa
ya kuweka taka
nyepesi katika maeneo
mbalimbali ya manispaa hiyo.
Akizungumza na baadhi ya
wananchi katika stendi
ya mabasi ya zamani
wakati wa kuweka mapipa hayo ,mkuu wa wilaya alisema zoezi hilo lilitakiwa lifanyike saa 1.30 asubuhi lakini wamelazimika kufanya saa
3.30 kutokana na uzembe uliofanywa na injinia ambaye alipewa kazi ya
kuandaa kokoto na
mchanga mapema matokeo yake hakufanya
hivyo.
“ Kwanza aliagizwa na mkurugenzi
wa manispaa hiyo Lewis
Kalinjuna kufanya maandalizi
mapema ya vitu vinavyotakiwa kwenye
kazi ya kuweka mapipa
ya taka nyepesi,matokeo yake mpaka
leo asubuhi hakuna
kilichofanyika hak una kokoto wala simenti eneo la kufanyika kazi huu ni uzembe , mkuu wa kituo uko wapi kamata huyu muweke
ndani”aliagiza mkuu wa wilaya.
Hata hivyo mkuu
wa wilaya aliwataka wananchi
kuyatumia kwa kuweka taka nyepesi
huku akiwatahadharisha wafanyabiashara wa vyuma
chakavu, kuwa makini na watu wanaowauzia
vyuma hivyo na kuwafichua watakao yaharibu
na kwenda kuuza wakibainika
hatua kali zitachukuliwa
dhidi yao.
Alisema iwapo mazingira
yatakuwa katika hali ya
usafi jamii haiwezi kukumbwa na
ugonjwa wa kipindupindu na
magonjwa mengine ,nakusisitiza
kuwa suala la usafi linatakiwa kuwaendelevu
kuanzia sehemu wanayoishi,
kwenye biashara na maeneo
yanayowazunguka.
Awali akijitetea mhandisi huyo wa manispaa Ngagani alisema tatizo lililofanya achelewe kufanya maandalizi
ni kutokana na kukosa fedha za kununua kokoto na simenti na kulazimika kuanza
kuomba kwa wadau na kufanikiwa kupata muda ukiwa umeenda.
Kwa upande wake ofisa
afya wa manispaa hiyo
Elly Nakuzerwa alisema
jumla ya mapipa 50 ya kuweka taka
nyepesi yametolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa
ni kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi na kujiepusha na mlipuko
wa magonjwa kikiwemo kipindupindu.
Aliwatahadharisha
wananchi kutoweka mabaki ya vyakula
kwenye mapipa hayo
na kuwataka kuzingatia usafi
kwa kila
mmoja, ambapo atakayebainika
anatupa uchafu hovyo atatozwa faini ya
papo kwa papo sh 50,000 na
akishindwa anapelekwa mahakamani.
|
0 Response to "DC SHINYANGA ATOA AGIZO MHANDISI WA MANISPAA KUWEKWA RUMANDE"
Post a Comment