Habari za hivi Punde

WATU 40,364 WAMEPIMWA,1,871 WAMEBAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VVU

Kati ya  watu 40,364 waliojitokeza kupima  afya kwa hiari katika halmashauri Msalala  mkoani Shinyanga   1,871 wamekutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi .

Mratibu wa ukimwi wa halmashauri  hiyo Jackson Faustine  anasema kuwa  watu hao walijitokeza kupima afya kati ya Januari hadi Novemba  2015.


Anasema mila potofu,umasikini,ukosefu wa elimu sahihi ya kuepuka maambukizi na shinikizo rika ni miongoni mwa sababu za kupata maambukizi hayo.
“Uwepo wa shughuli nyingi za kiuchumi ikiwemo migodi ya dhahabu na kilimo cha mpunga pia  kuchochoea kasi ya maambuzi”  anasema  Faustine.

Mmoja wa wadau wa mapambano dhidi ya ukimwi Rajabu Thomas alisema kuwa  wadau wanapaswa kuwashirikisha  viongozi wa dini,wanasiasa na watu maarufu ili kudhibiti maambukizi mapya  ya ukimwi.

Mwenyekiti wa kamati  ya kudhibiti  ukimwi wa halmashauri hiyo Benedicto Mwanwali alizomba asasi za kiraia  moja  ya ajenda  zao kuu iwe ni mapambano  dhidi  ya ukimwi katika jamii.

0 Response to "WATU 40,364 WAMEPIMWA,1,871 WAMEBAINIKA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VVU"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.