Habari za hivi Punde

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU TISA KWA TUHUMA YA MAUAJI YA WANAWAKE WAWILI WALIOTUHUMIA KUZUIA MVUA ISINYESHE KATIKA KIJIJI CHA MWABULIMBU WILAYANI MASWA





JESHI  la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake wawili wa kijiji cha Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya akina mama wawili kuuawa na kuchomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha.

Licha ya wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi wa jadi "Sungusungu" akiwemo Mtemi  na Kamanda wake mkuu kwa tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao waliochomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani  humo.

 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo  akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake alisema  kuwa viongozi waliokamatwa ni Mtemi mkuu wa sungusungu Ntalage Mabula (50) na Kamanda wake mkuu Sosoma Mamuda (50) wote wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu,kata ya Mwang'honoli tarafa ya Sengerema  wilayani Maswa.


Wanawake waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ni Tabu Mongo (31) na Joyce Kija (30) watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu kata ya Mwang'honoli  tarafa ya Sengerema wilayani Maswa.
Akielelezea tukio hilo kamanda  huyo alisema watuhumiwa wote walikamatwa Februari 4  mwaka huu kufuatia viongozi hao wakuu wa sungusungu ambapo   tarehe mbili mwezi huo  walitoa  amri na agizo la kupiga yowe na filimbi za hatari na kukusanya wananchi.

 Ambapo  walianza shambulio la kuwapiga   bila kusikiliza maelezo yoyote kutoka kwao  ikiwa walionekana kuwa na hali mbaya kutokana na majeraha waliyoyapata hatimaye walifufa papo hapo na badaye kuanza   kuwachoma moto  miili yao .
Alisema wananchi hao wakiwa na silaha zao za jadi,marungu,fimbo mawe  waliwauwa wanawake hao na kisha  kuchomwa moto, waliofahamika kwa jina la Gilya Chile (70) na Nyang'au Nyambalya (30) wote wakazi wa kijiji hicho.

Kamanda Mkumbo alisema kuwa kabla ya mauaji hayo, kijiji hicho na maeneo mengine wilayani Maswa na hata mkoa wa Simiyu yalikuwa yakikabiliwa na ukame wa mvua kutonyesha, na inadaiwa kuwa akina mama hao waliomba kuchangiwa gunia moja kila mmoja kwa vile wanatoka katika ukoo wa kichifu ili mvua iweze kunyesha.

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda wake mkuu wa Sunsungu  walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi.

Kamnda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao  wameshikiliwa na jeshi la polisi mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

0 Response to "JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU TISA KWA TUHUMA YA MAUAJI YA WANAWAKE WAWILI WALIOTUHUMIA KUZUIA MVUA ISINYESHE KATIKA KIJIJI CHA MWABULIMBU WILAYANI MASWA "

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.