Habari za hivi Punde

AJINYONGA KWA KUUGUA MIAKA 18 KIFUA KIKUU BILA KUPONA,AACHA UJUMBE KWA BABA MZAZI-BUKOMBE

HII NI SEHEMU ALIYOKUWA AKIFANYIA KAZI MAREHEMU  BUTUNGO MBUGANI KATIKA KITONGOJI CHA NTEGELE KIJIJI CHA IGULWA WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA.
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la  Butungo Mbugani mkazi wa kitongoji  cha Ntegele kijiji cha Igulwa kata hiyo wilayani Bukombe  mkoani Geita amechukua jukumu la kujinyonga  kwa kutumia kamba ya katani baada kuugua kwa muda wa miaka 18 ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

Kijana huyo ambaye alianza kuugua maradhi hayo akiwa na umri wa miaka miwili alishindwa kupona  na badala yake alichukua uamuzi wa kujinyonga huku akiacha ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi kuwa    “kwa heri baba  nimeamua kujinyonga  sababu ya kuugua muda mrefu nakwenda kuanza maisha mapya ahera”.
Kwa mujibu wa maelezo  ya baba wa marehemu  Mbugani Maleka alisema kuwa  mwanaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo tangu akiwa na  umri wa miaka miwili na kumfanya asisome ,ambapo alieleza kuwa kifo hicho kimekuwa na mshtuko mkubwa kwani hawakufikiria kama angechukua uamuzi huo.
Alisema katika uhai wake licha ya kuugua muda mrefu alikuwa akitibiwa katika hospitali  ya wilaya ya Bukombe na vituo vya afya tofauti tofauti   na kupata unafuu   ikiwa ilimfanya dawa alizokuwa akipewa kuendeleza hata shughuli zake ili kuweza kujipatia kipato.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho Andrew Tungu baada ya kupata taarifa  majira ya saa 4 asubuhi kwa kutokea kifo hicho alisema kuwa  baadhi ya wananchi wenye maradhi ya kusumbua muda mrefu wanatakiwa kumuona mtaalamu mara kwa mara na sio kuchukua jukumu zito kama hilo huku akiwataka wazazi na walezi kuzingatia chanjo maalumu kwa watoto na sio kupuuza.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani  Geita Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji hicho ambapo alieleza kuwa fiko cha  kijana huyo kinatakiwa kuchunguzwa kitaalamu zaidi .



0 Response to "AJINYONGA KWA KUUGUA MIAKA 18 KIFUA KIKUU BILA KUPONA,AACHA UJUMBE KWA BABA MZAZI-BUKOMBE"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.