Habari za hivi Punde

MBUNGE JOHN SHIBUDA AVURUGA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI -MASWA

MBUNGE wa maswa Magharibi John Shibuda  (CHADEMA ) amevuruga kikao  cha baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kutokana na kuingiza mambo ya ukawa ndani ya baraza hilo  ambapo  ilifikia hatua ya kurushiana maneno makali na  mbunge mwenzake  wa Mashariki  Slyvester Kasulumbayi  (CHADEMA) ambapo   vurugu kubwa ilitokea na kutishia kuvunjika kwa kikaoKikao hicho kilichokuwa kikifanyika  kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya
Maswa  ambapo Shibuda alianza kueleza  msimamo wake mbele ya baraza hilo kutounga mkono msimamo wa UKAWA na kuukataa muundo wa serikali tatu.

Dalili za vurugu hizo zilianza pale Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
,Stephen Dwese kumpatia nafasi Shibuda kuongea mbele ya baraza hilo
juu ya shughuli za maendeleo zilizofanyika katika jimbo lake kwa
kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Wakati mbunge huyo akitoa taarifa ya shughuli hizo alitumia muda huo
kueleza kuwa binafsi haoni faida ya kujiunga na kundi la UKAWA kwani
halina manufaa yoyote isipokuwa watu wanatafuta madaraka tu.

Shibuda wakati akiendelea kueleza  mara Mbunge wa Jimbo la Maswa
Mashariki,Slvester Kasulumbayi(CHADEMA)alinyoosha mkono na kumtaka
Mwenyekiti wa halmashauri kumzuia Shibuda kuelezea mambo ya UKAWA
katika kikao hicho.

“Mheshimiwa Mwenyekiti nakuomba sana umzuie mhesimiwa Shibuda
asizungumzie masuala ya UKAWA ndani ya baraza hili maana hapa si
mahali pake ipo sehemu ya kuzungumzia”Alisema kwa Ukali.

Hata hivyo Mwenyekiti Dwese alimtaka Shibuda amalizie muda wake huku
akisisitiza kuwa hicho ni kikao cha baraza la madiwani na mbunge ni
mjumbe halali na ana haki ya kueleza msimamo wake wa kisiasa kwa
wananchi waliompigia kura ambao ni wako Maswa.

Baada ya maelezo hayo Mbunge Kasulumbayi na baadhi ya madiwani wa
Chadema walianza kupiga kelele na kumtaka Shibuda atoke mbele ya
kipaza sauti huku madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakishangilia
na kupiga kelele huku wakisisitiza kuwa Shibuda amalize muda wake.
Hali hiyo ilibidi itulizwe na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo,Ndila Mayeka huku Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Luteni mstaafu,Abdalah
Kihato na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Trasias Kagenzi
wakibaki na mshangao.
Wakizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao kumaliza
Wabunge hao, kila mmoja alimtolea lawama mwenzake kwa kutokuwa
mvumilivu wa kisisasa huku Shibuda akisisitiza kuwa Kasulumbayi
amekuwa akiitisha mikutano na kumtukana na Kasulumbayi akisisitiza
kuwa kama Shibuda amechoka CHADEMA aende atakako kwa amani.
MWISHO.
KARENY. Powered by Blogger.