Habari za hivi Punde

ASUSIA KUISHI KWA KUJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITO- CHALINZE


shambani

Mwanamme mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”


Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema  mwanamume  huyo amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Chalinze.

Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye maandishi hayo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu msaidizi, Athumani Mwambalaswa amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa na kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.


Hata hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa kijiji kipi kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta ndugu zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado hakijajulikana.
KARENY. Powered by Blogger.