Habari za hivi Punde

NI KWELI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YANAWEZA KUTOWEKA KUFIKIA MWAKA 2030?

DAWA  ZITASAIDIA KUONDOA CHANGAMOTO YA MAAMBUKIZI?


IMEELEZWA kwamba ifikapo mwaka 2030, kuna uwezekano mkubwa wa kudhibitiwa kwa  Janga la Ukimwi duniani,hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kupambana na Ukimwi.

Shirika hilo linasema idadi ya maambukizi mapya na wanaokufa
kutokana na Ukimwi imeendelea kushuka.

Hata hivyo jitihada zaidi za kimataifa zinahitajika kwani zilizopo hazitoshi kumaliza janga hilo.


shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.


Ripoti hiyo inaonyesha kuwa watu milioni 35 duniani wanaishi na virusi vya Ukimwi.


Ripoti hiyo ilionyesha kuwa maambukizi mapya milioni 2.1 yalitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.


Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.

0 Response to "NI KWELI MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI YANAWEZA KUTOWEKA KUFIKIA MWAKA 2030?"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.