Wanafunzi wa shule ya msingi wakisoma katika mrundikano ambapo walimu wanashindwa kufundisha.
SHULE ya msingi iliyopo kwenye kijiji na kata ya Bugarama katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya mrundikano wa wananfunzi madarasani ambao umesababishwa na baadhi ya vijiji vya jirani kukosa shule.
Ikiwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi zaidi ya 1400, vyumba vya madarasa 20, kwa darasa moja linawanafunzi 70 hadi 80,walimu 32 huku ikikabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu kwani zilizopo ni nyumba nne pekee.
Waandishi wa habari walitembelea kijiji hicho huku baadhi ya wananchi wakieleza changamoto ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kuwa baadhi ya vijiji viwili vinategemea watoto wao wasome humo kutokana na maeneo hayo kukosa shule za msingi,ambapo mwalimu mkuu wa shule Simoni Lasana alisema hiyo yote inasabaishwa na vijiji hivyo kuwa na mgodi ambao unafanya kuwa na mwingiliano wa watu kila siku.
“Mwingiliano wa watu sababu ya mgodi wa kakola ndio umeleta idadi ya kuwa na wanafunzi wengi ,kwani vijiji vingine havina shule kutokana na mwaka 2009 kata ya Bugarama ilizalisha vijiji vitatu ambavyo ni Igudeja, Bunango na Bugarama , watoto kutegemea shule hiyo ikiwa jumla ya wanafunzi ni zaidi ya 1400 huku darasa moja likiwa na wanafunzi 70 hadi 80”alisema mwalimu mkuu Lasana.
Pia alisema kumekuwepo na changamoto ya uhaba wa ofisi ikiwa darasa moja limegeuzwa kuwa ofisi, nyumba za walimu zilizopo ni nyumba nne pekee huku walimu wakiwa zaidi ya 30 na mamboma tisa ya nyumba za walimu tayari yamekwisha jengwa ila bado hayajapata wa kusaidia kukamilisha.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Bunango Iddi Binki alisema kuwa kijiji chake kimekamilisha ujenzi wa madarasa matatu bado ukosefu wa choo ndio tatizo pindi itakapo kamilika kunategemewa kuwagawa wanafunzi wengine katika shule hiyo ili kuweza kupunguza msongamano.
Mratibu wa elimu katika kata hiyo Stanley Mduta alisema kuwa changamoto hiyo ipo ila mikakati ya vijiji vilivyoanzishwa kujenga shule vimeanza kutekeleza ikiwemo kijiji cha Bunango kimekamilisha madarasa matatu lengo kutaka kuwagawa wanafunzi hao,sababu ya kuwepo kwa wanafunzi wengi ni mwingiliano wa watu kwenye mdodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo Patrick Kalangwa alisema kuwa changamoto hiyo ni kweli kwenye baadhi ya shule ikiwemo hiyo, ikiwa zimeagizwa kamati za shule kuhamasisha ujenzi wa maboma na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu upo tayari kukamilisha maboma hayo kwa mujibu wa mkataba na mahusiano yaliyopo katika kuondoa changamoto zinazowakabili wananchi
|
0 Response to "SHULE YA MSINGI BUGARAMA ILIYOPO HALMASHAURI YA MSALALA WILAYANI KAHAMA INACHANGAMOTO YA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI IKIWA DARASA MOJA NI WANAFUNZI 70 HADI 80."
Post a Comment