Habari za hivi Punde

KIKONGWE WA MIAKA 75 ACHARANGWA MAPANGA MTUHUMIWA MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus  Kamugisha.

KIKONGWE   Sayi Nyenje (75) mkazi wa kijiji cha Mwagata kata ya mwamalilli  manispaa ya shinyanga  ameuwawa kwa kucharangwa  mapanga  mwili na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kwa mujibu wa taarifa ya  kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga  Justus Kamgisha amesema  tukio hilo limetokea  jana mnamo  majira ya saa tano usiku ambapo kikongwe huyo alikuwa amelaa nyumbani kwake na wajukuu zake wawili ghafla alivamiwa na watu wawili na kukatwa mpanga .
Kamanda Kamugisha  amesema  kikongwe huyo alivamiwa na watu hao na kukatwa mapanga Shingoni, pamoja na kiganja cha mkono wa kushoto na kusababishia kifo.
Ambapo amesema  kuwa   mmoja wa wauaji hao Joel Machia (45) msukuma  mkazi wa wa  Mwamalili anashikiliwa na Jeshi la polisi  kwa tuhuma huenda akausika na mauaji hayo.
Kamanda alisema mwenzake ambaye hakufahamika jina alifanikiwa kutoroka  huku jeshi la polisi katika uchunguzi wa awali  ilisema chanzo cha mauaji hayo  kunatetesi za kuwepo kwa ugomvi wa mashamba .


KARENY. Powered by Blogger.