Habari za hivi Punde

MAJERUHI WA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MAENEO YA UCHUNGA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA, PICHANI WAKIWA HOSPITALI YA MKOA WAKIPATIWA MATIBABU AMBAPO WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA.

BAADHI YA MAJERUHI WA AJARI YA FUSO WAKIPATIWA MATIBABU
WATAALAM WA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA WAKITOA HUDUMA
UMATI WA WAKAZI WA KIJIJI CHA UCHUNGA WAKITAZAMA AJARI YA FUSO
MAJERUHI KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MAENEO YA UCHUNGA WILAYANI KISHAPU WAKIWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA; 

WATU  watatu wamefariki dunia na wengine 46 kujeruhiwa vibaya  katika ajali ya gari  iliyotokea maeneo ya Uchunga  wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo  lilikuwa  likienda kwenye mnada wa Mhunze  katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga .
Gari hilo lenye namba za  usajili T.680 ARL aina  ya  fuso mali ya Ngassa Seni  mkazi wa Kiloleli wilayani  humo lililokuwa likiendeshwa na dreva aliyejulikana kwa jina la Shija Ngassa  ambapo lilipinduka na kuacha njia.
Mmoja wa majeruhi hao Kashindye Mkaa alisema kuwa wakati wa kuanza safari  gari lilianza kwa mwendo kasi ndipo walipofika kwenye kona likaacha njia na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.
“Mara baada ya kuanza gari kuyumba dreva  wa gari hilo aliruka nje  na kukimbia porini huku gari likiendelea kuyumba mwisho  likapaa na kwenda kupinduka  ambapo liliacha njia,wakati huo tulikuwa tunakwenda mnada wa  Mhunze kufanya biashara  kwani ilikuwa siku ya mnada”alisema  Mkaa.
Hata hivyo  kaimu mganga mfawithi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga   Daniel Maguja alikiri kupokea majeruhi hao huku akisema kuwa watu wawili walifariki dunia  njiani wakiwa wanaletwa hospitali  hapo na watatu alifariki akiwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu.
“Majeruhi  46 mpaka sasa,wengine watatu wamefariki dunia ambapo  majeruhi wengi wamelazwa ikiwa hali zao ni mbaya kwani  baadhi yao wamevujika miguu,mikono,mbavu na sehemu za kichwani”alisema Maguja.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Justus Kamugisha  alithibitisha kutokea kwa   ajali hiyo  na kueleza kuwa imetokea mnamo majira ya saa tatu asubuhi  katika kijiji cha uchunga  ambapo   chanzo chake kimelezwa kuwa ni mwendo kasi.
Pia  kamanda alisema kuwa idadi hiyo inasemekana ni ndogo ikiwa gari hilo lilikuwa limewabeba wafanyabiashara  waliokuwa wakienda kwenye mnada wa  Mhunze huku wengine wakiwa na tabia ya kudandia magari hovyo aliwaomba  wananchi kuacha tabia hiyo kwani ni  hatari ikiwa gari  kuzidiwa na mizigo nayo ilichangia.KARENY. Powered by Blogger.