Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt Seif Rashid.
SERIKALI imeshauriwa kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa wa homa ya ini sambamba na kutoa elimu kwa jamii ambao umeanza kuonekana ni tishio hapa nchini ili kunusuru afya za wananchi.
Ugonjwa huo umeonekana kwenda sanjari na maambukizi ya virusi vya ukimwi ikiwa kampeni inatakiwa wananchi kuelewesha juu ya kujikinga kwake na madhala yake kama inavyo fanya kwa magonjwa mengine.
Ushauri huo umetolewa na kaimu mganga wa Hosptali ya wilaya ya Kahama Dkt Deo Nyaga alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hospitalini hapo huku akieleza kuwa kugundulika kwa ugonjwa huo wa ini nipale wanapochukua vipimo vya vvu kwa wale wanaojitolea damu kwa ndugu zao.
“ugonjwa huu tumekuwa tukiuona tunapo chukua damu kwa watu wanao kuja kujitolea au wanao tolea ndugu zao na kugundua kuwa licha maambukizi ya ukimwi tumegundua waliowengi bado wanatatizo la ugonjwa wa ini hapo baadaye litakuwa tishio , hivyo serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka wananchi kupatiwa elimu’ alisema dkt Nyaga.
Aidha changamoto inayoikabiri Hosptali hiyo ni mrundikano wa wagonjwa kitendo ambacho wauguzi pamoja na madaktari hawatoshi licha ya jitihada za serikali kujenga vituo vingi maeneo ya vijijini ikiwemo kuna upungufu wa watumishi ndio maana wagonjwa wengi hukimbilia hospitali ya wilaya zaidi.
Katika tuhuma za uuzwaji wa damu hosptalini hapo alisema kumekuwa na mawazo potofu kwa baadhi ya watu kwani utaratibu ni kuwa anapo letwa mgonjwa ana tatizo hilo ndugu zake huambiwa watafute mtu wa kumtolea damu na anapo patikana huwekewa damu iliyoko kwenye kiba na hiyo iliyochukuliwa huwa ni bahati nasibu kama itakutwa ni salama.
Pia aliobgeza kuwa wengine wanapo ambiwa watafute ndugu na kukosa huenda mjini kutafuta watu wasio wajua kwa makubaliano ya malipo na wanapo fika kazi ya wao ni kutoa damu tu si vinginevyo. |
0 Response to "SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA MIKAKATI JUU YA UDHIBITI WA UGONJWA WA INI AMBAO UMEANZA KUWA TISHIO."
Post a Comment