huyu ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila. |
Wakiongea katika baraza hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa mkoa baada ya mchumi wa manispaa hiyo Christopher Nyarubamba alisoma taarifa ya maazimio yaliyoafikiwa na madiwani kuwa daladala zote za baiskeli hazitakiwi , ambapo zimelekezwa ziwe kando ya mji kwa kusajiliwa na kupewa vitambulisho ikiwa utekelezaji wake unatakiwa kuanza mara moja.
Nyarubamba katika taarifa yake alisema kuwa waendesha daladala za baiskeli wanatakiwa kuondoka kutokana na kushamiri kwa vitendo vya kikatili dhidi ya watoto,huku baadhi ya madiwani akiwemo diwani viti maalumu Shella Mshandete kuunga mkono azimio hilo na kueleza kuwa wananchi wa manispaa wanatakiwa kubadilika kama maeneo mengine mbona kuna daladala za magari hakuna baiskeli wao wanashindwa nini?.
Pia diwani vitimaalumu (chadema) Siri Yasin alisema kuwa hakuta wezekana kuwafukuza waendesha daladala za baiskeli bila kufahamu mbadala wake,hivyo inatakiwa usafiri upatikane ndipo zoezi la kuwaondoa lianze bila hivyo jamii haitaelewa kwani wamezoea usafiri huo kuwakatisha ghafla italeta tatizo pia.
“Jamani tunapoanza kuziondoa daladala za baiskeli tufahamu wazi kwamba tutawapa shida wananchi waliozoea usafiri huo,kinachotakiwa kuwepo na mbadala wake mimi sipingi kuwa wasiondolewa kwani vitendo vya ukatili kwa watoto manispaa vimezidi kuongezeka ukiangalia chanzo ni madreva wa daladala wenye kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta utajiri wa haraka”alisema Yasini.
Katibu tawala wa wilaya Boniface Chambi alisema kuwa daladala za gari zilikuwepo na uzinduzi ulifanywa na mkuu wa mkoa Ally Rufunga lakini cha kushangaza watu walikuwa hawazipandi huku wakiwakatisha tamaa wenye daladala hizo matokeo yake zikasitishwa mpaka leo hii kunaonekana daladala za baiskeli pekee.
Kwa upande wake naibu mstahiki meya manispaa hiyo David Nkulila alisema kuwa daladala za baiskeli ziondolewe kama lilivyopitishwa azimio,pia aliwanyooshea kidole baadhi ya maaskari kukamata magari ya abiria hovyo kwa mitazamo yao ya kimaslahi hivyo kwa hilo halitavumiliwa hata kidogo inatakiwa wajirekebishe kwenye utendaji wao wa kazi.
0 Response to "AZIMIO LIMEPISHWA USAFIRI WA DALADALA KUONDOLEWA MANISPAA YA SHINYANGA KUTOKANA NA BAADHI YA MADREVA KUFANYA VITENDO VYA KIKATILI KWA WATOTO IKIWEMO UBAKAJI NA KUWATOBOA MACHO. "
Post a Comment