CHANGAMOTO kubwa
inayowakabili watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na wale wenye kuishi na maambukizi ya
virusi vya ukimwi ni kwa ukosefu wa
mahitaji muhimu wanaopaswa kuyapata kama watoto wengine , lishe duni , pia walezi au wazazi kutokuwa na kipato huku
wengine wakiwatelekeza kwa makusudi.
Hayo yalisemwa na mwalimu Johari
Salum wa kituo cha kulelea watoto
hao cha (ECD) chini ya ufadhili wa shirika la Lara Foundation
International kilichopo kata ya Ndala
manispaa ya Shinyanga chenye watoto 45,
wakati wa mfanyabiashara Oscar Kaijage
alipotembelea kituoni hapo akiwa
ameambatana na mke wake kwaajili ya
kutoa msaada wa vitu mbalimbali yakiwemo
madaftari na kalamu.
Mwalimu Salum alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili
watoto hao ni kutokuwa na lishe nzuri,walio wengi wanaishi na walezi wao ambapo
wazazi wengine walikwisha fariki kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi huku walio bado hai
wamekwisha watelekeza kutokana na kipato
duni kwenda kutafuta maisha.
“Kituo hicho tumechukua
watoto wenye hali mbalimbali katika maisha yao ili waweze kupata elimu
ya awali,lakini walengwa wanaotakiwa
kuwepo kwenye kituo hicho ni watoto wenye kuishi na maambukizi ya virusi vya
ukimwi na mazingira hatarishi kwani wanaoishi na virusi pekee katika tathimini
iliyofanyika maisha yao waliowengi yenye uafadhali kuliko hata ambaye
hana maambukizi hayo hivyo tunaangalia kipato cha familia kikoje”alisema
mwalimu Salum.
Naye kaijage alisema kuwa aliamua kutoa msaada huo wa vitu
mbalimbali kwa kuona yuko sahihi kwa pamoja kuwa na watoto hao kwani hata yeye
ni yatima aliyefiwa na mama yake mzazi
kutokana na maradhi ya maambukizi ya virusi
vya ukimwi huku akieleza kuwa uhalisia watoto hukosa malezi yaliyobora na vitu
wanavyovihitaji ni adimu kwao na kuishia kuvitamani.
“Msaada huu ni kama kumbukumbu ya mama yangu mzazi kwani nilihitaji zaidi awepo
lakini hakuna budi ya kukumbuka kwa kutoa msaada kwa watoto hao ambao baadhi
yao ni yatima,weninge wanaoishi katika mazingira hatarishi kutokana na walezi
au wazazi kuwa na kipato duni ambapo vitu vingi hutamani na kuwa nadra kwao
kuvipata”alisema Kaijage.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa mtaa wa Mlepa John Buhembo alisema kuwa kituo hicho kimekuwa na
utaratibu wa kuwapata watoto hao kama ilivyolengwa ,aliitaka jamii ishirikiane ili iweze kuwasaidia watoto hao kufanikisha maendeleo na kuacha kuingiza mambo ya siasa kwa wazazi au walimu ,kama
yataingia ndani ya kituo hicho hakika hakita dumu .
0 Response to "CHANGAMOTO KWA WATOTO WENYE VVU NA WENYE KUISHI MAZINGIRA HATARISHI"
Post a Comment