VIONGOZI wa vijiji wote wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga
wameagizwa kuhakikisha wanasimamia mazingira ipasavyo, na wahakikishe miti
haikatwi kiholela ili kuimarisha ufugaji wa nyuki katika misitu hiyo.
Agizo hilo limetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Willison Nkhambaku wakati wa uzinduzi wa mizinga ya nyuki uliofanyika katika
kijiji cha Nyasamba kata ya Bubiki wilayani humo ambapo alisema atakaebainika
anakata ovyo achukuliwe hatua kali za kisheria.
“Nawaomba sana viongozi wa vijiji simamieni miti isikatwe
katwe ovyo atakayeonekana anakata miti tutamchukulia hatua kali za kisheria
hivyo tuhakikishe tunalinda miti yetu ili tuweze kupata nyingi na kuondokana na
balaa la njaa”alisema Nkhambaku.
Alisema kiongozi ambaye hata simamia ipasavyo atachukuliwa
hatua kali na kama atashindwa achukue jukumu la kujiuzulu kuanzia sasa na
kuwataka wasimamie mipaka iliyopo maeneo ya nyuki yaheshimiwe.
“Sisi viongozi tukisimamia vizuri itasaidia kuinua kipato
kwa kupitia ufugaji wa nyuki ambayo inafaida nyingi unaweza ukatengeneza dawa
ya kuondoa fangazi, kupunguza mvi kwa wazee, kutengeneza ngozo iliyokunjamana,
kutengeneza mshumaa ambao utauwasha na kuweza kukimbiza mbu na faida zingine
mbalimbali”alisema Mkuu huyo.
Akisoma taarifa ya wanakikundi cha ufugaji nyuki kwa wazee
chenye jina la Upendo- kilichopo kijiji cha Nyasamba Willison Malimu ambaye ni
katibu wa kikundi hicho alisema mradi huo wa ufugaji wa nyuki ulianza rasmi
tarehe 9/4/2011.
Alisema mradi huo ulianza ukiwa na wanachama 15 kwa manufaa
ya kuinua hali ya maisha ya wanakikundi pindi mradi utakapo anza kutoa
mazao ya nyuki (Asili na nta).
Alisema katika mradi huo kuna changamoto nyingi ambazo ni
wananchi kuingia na kukata miti katika misitu, wananchi kuingia eneo la msitu
na kulima, mifugo kuingia katika msitu kulisha humo ikiwa ni pamoja na msitu
kuharibiwa na kusababisha kutokueleweka mwisho wake.
Katibu wa kikundi hicho alisema kikundi hicho kiliomba fedha
toka mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) na kukubaliwa ambapo walipewa
jumla ya Tshs 11,855,301.50/= ambazo walitumia kwa kupatiwa mafunzo kwa
ajili ya uendeshaji wa mradi.
Alisema kupitia fedha hizo pia walipata mafunzo ya ufugaji
bora wa nyuki yaliyoendeshwa na idara ya nyuki wilayani hapo, walinunua zana za
kufugia nyuki jumla ya mizinga 50, ambapo mizinga ambayo imeanza kutumiwa na
nyuki ni saba.
0 Response to "VIONGOZI WA VIJIJI WILAYANI KISHAPU WAAGIZWA KUSIMAMAIA MAZINGIRA IKIWEMO UFUGAJI WA NYUKI KATIKA MISITU."
Post a Comment