WANANCHI mkoani shinyanga wametakiwa
kuondokana na unyanyapaa kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi
ikiwemo mama wajawazito kuhudhuria katika kliniki kwa
kupima afya zao na kuondoa maambukizi ya mama kwenda kwa
mtoto ambapo kiwango mpaka sasa kimefikia asilimia 5.6.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Annarose Nyamubi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi
wa kampeni ya utokomezaji wa maambukizi virusi vya
ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto huku akisema kuwa
maambukizi hayo tangu mwaka 2011 yalikuwa asilimia 26.
Nyamubi alisema kuwa mkoa umepiga hatua kubwa ya
kuweza kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto ,ikiwa suala la unyanyapaa bado ni tatizo kubwa katika jamii hivyo
kwa kushirikiana kwa pamoja maambukizi hayo yanaweza kutokomezwa na
kuondoa unyanyapaa.
“Kweli maambukizi ya virusi vya ukimwi sio tishio la kuweza
kumuogopa mtu kwani ni kama magonjwa mengine kinachotakiwa jamii
kushirikiaana kwa kufuata wataalamu wa afya wanavyosema kama mtu
anakuwa hajaathirika basi atajilinda na yule ambaye atakuwa amegundulika
atapata ushauri wa kuweza kuishi vizuri kwenye jamii na mwenza wake”alisema
Nyamubi.
Alisema kuwa kwa takwimu za kitaifa kwa mwaka
wa 2010 zilikuwa ni asilimia 5.3 ambapo katika mkoa wa Shinyanga mpaka
sasa unamaambukizi ya asilimia 7.4 kwa takwimu za mwaka wa 2012,ambapo
alidai kuwa kwa pamoja kwa kushirikina ugonjwa huo unaweza kutokomezwa na
usiwepo .
Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga
Dkt Ntuli Kaborogwe alisema ushauri uliopo kwa wananchi
kuwa ifikapo mwaka wa 2015 mkoa huu uondokane na maambukizi mapya ya
virusi ikiwa idadi ya maambukizi inaenda ikipungua tofauti na miaka mingine ya
2011 kuwa asilimia na asilimia 26 na kupungua kufikia asilimia 5.6 mwaka 2012.
Kwa upande wake meneja wa shirika lisilo la
kiserikali linalotoa elimu dhidi ya kujikinga na virusi vya
ukimwi (Agpahi) kwa mkoa wa Shinyanga Dkt Gastor Njau alisema
kuwa uzinduzi wa kampeni hii lengo lake ni utokomezaji wa
maambuziki ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
katika hatua muhimu ya kuondoa ukimwi kwa watoto.
Hata hivyo Ngwashi Salehe ni mmoja wa shuhuda aliyejieleza
katika hadhara iliyohudhuria uzinduzi huo kuwa ni mwaathirika tangu mwaka
2002 na kuendelea kunywa ARV kwa kubahatika kupata mtoto
mwaka 2012 akiwa hajapata maambukizi yoyote kutoka kwa mama ambapo
alieleza pia ni kutokana na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya na kuzingatia
maelekezo.
0 Response to "MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO YAPUNGUA NA KUFIKIA ASILIMIA 5.6 MKOANI SHINYANGA"
Post a Comment