WAFANYABIASHARA wa vibanda katika soko la Nguzo nane
manispaa ya Shinyanga mkoani hapa wamelalamikia ongezeko la kutozwa ushuru
kutoka shilingi 15,000 na kupandishiwa shilingi 30,000 jambo ambalo wamemuomba
mkurugenzi wa manispaa hiyo Festo Kang’ombe kuongea nao ili kutatua suala hilo.
Wafanya biashara hao wakizungumza na waandishi wa habari
katika soko hilo jana walisema kuwa kilio chao kikubwa ni kumuomba mkurugenzi
wa manispaa hiyo waongee nae kwani wamekuwa wakipandishiwa ushuru bila hata
kuwashirikisha wao hali ambayo wanadai wananyongwa kulingana na kipato kidogo
wanachokipata katika biashara zao.
“Kwa kweli ongezeko hili hatulikubali kwani manispaa
hatuielewi ina mpango gani na sisi ukilinganisha na hali ya hewa ya sasa siyo
nzuri kipato tunachokipata ni kidogo sana lakini manispaa inatupandishia ushuru
tumeamua kwenda kwa mwanasheria wa manispaa lakini majibu yake yamekuwa
yakitatanisha”walisema wafanyabiashara hao.
“Kilio chetu sisi wafanyabiashara ni kutaka kuongea na
mkurugenzi wa manispaa kwani mwaka 2011 nikiwa kama wakala tulikuwa tunatoa
ushuru shilingi 1500 lakini ukapandishwa shiringi 15000 ambapo haileweki mara
unatozwa elfu 20 na sasa kuanzia tarehe 1 mwezi wa 3 mwaka huu
wanatupandishishia elfu 30 huku wakala anaechukua ushuru haelewi ongezeko hili
limeongezwaje”alisema Abdul Kidoda ambaye ni mfanyabiashara katika soko hilo.
Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa wafanyabiashara katika
soko hilo Hassan Baruti alisema kilio chao kikubwa ni kupandishiwa ushuru kwani
kwa sasa hali ni mbaya ya kibiashara wafanyabiashara hawapati kipato kikubwa wanawatotot
wanasomesha hivyo alimuomba mkrugenzi awakubalie aje awasikilize kilio
walichonacho.
“Sheria hii inayotarajiwa kuanza tarehe moja mwezi wa tatu
itawaumiza sana wafanyabiashara wa soko hili tunasikia diwani wa kata hii ndiye
aliyepitisha ongezeko hili lakini hahudhulii hata kwenye vikao vyetu kusikiliza
matatizo tuliyonayo katika biashara”alisema Baruti.
Salome Ntalimbo ambaye nae ni mfanyabiashara wa soko hilo
alisema wao walikubaliana na shilingi 15000 na wakasaini mkataba na kuanza
kulipa sasa mwaka huu wametupandishia ushuru hali ambayo imetufanya
tuchanganyikiwe kutokana na ongezeko hilo.
"Tunamuomba tu mkurugenzi akubali tuongee nae ili
tuweze kuyamaliza kwani wakati huu tunahali ngumu sana ya kipato ukilinganisha
na sisi wenyewe tuna watoto tuna somesha na ushuru wa manispaa unazidi kupanda
huku tunatakiwa kulipa mikopo tuliyokopa"alisema Ntalimbo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa hiyo
Mwanamisiyu Dossi ambaye pia ni afisa ustawi wa jamii alisema kuwa suala hilo
watalifuatilia.
0 Response to "WAFANYABIASHARA SOKO LA NGUZONANE WALALAMIKIA ONGEZEKO LA USHURU"
Post a Comment