WAAJIRI wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani
hapa wametakiwa kuacha kupokea rushwa na kupendelea pindi wanapoteuwa
wafanyakazi bora ambao wanastaili kupewa zawadi katika siku ya kilele cha
maadhimisho ya sikukuu za wafanyakazi Duniani Meimosi
Akizungumza katika kikao cha wadau wa sherehe za Meimosi
juzi mjini shinyanga mkuu wa mkoa Shinyanga Ally Rufunga, wakati wadau hao
wakijadili mikakati ya kufanikisha maadalizi ya sherehe hizo alisema kumekuwa
na tabia kwa baadhi ya waajiri kupokea Rushwa na kuteuwa wafanya kazi wasio na
vigezo.
Rufunga alisema sherehe za Meimosi ziliwekwa kwa madhumuni
ya kuwapongeza wafanyakazi wanaofanya vizuri kwa kuwapa zawadi mbalimbali
pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi ambao ni wazembe
ili kuleta chachu ya maendeleo na kukuza uchumi wa nchi
“Muajiri unapopokea Rushwa au kupendelea kuteuwa wafanyakazi
wasio staili kuzawadiwa katika sikukuu za Meimosi, utawavunja moyo wafanya kazi
wanaojituma na hivyo kufanya utendaji kazi kwa wafanya kazi wako kushuka
kiwango “alisema Rufunga
Naye mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi
mkoani Shinyanga (TUKTA) Fue Mlindoko aliahidi kuwa mstali wa mbele katika
kuhakikisha suala zima la Rushwa wala upendeleo halishiki nafasi katika sherehe
za mwaka huu (2014) kama ilivyotokea mwaka jana katika manispaa ya Shinyanga
ambapo zoezi la utoaji zawadi lilisitishwa
‘Sherehe za Meimosi mwaka jana katika Halmashauli ya
manispaa ya shinyanga kulitawala Rushwa ,upendeleo na kuteuwa wafanyakazi wasio
staili kutunzwa zawadi hizo, mfano katika idara ya afya aliyeteuliwa kupokea
zawadi ni mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti lakini akachakachuliwa na
kupewa muuguzi ‘’alieleza Mlindoko na kuongeza kuwa
‘’Kutokana na kugundulika kwa kitendo hicho tuliamua kutoa
taarifa kwa mgeni rasimi ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wetu Ally Rufunga
kusitisha kutoa zawadi kwa baadhi ya wafanyakazi wa manispaa ya shinyanga mpaka
hapo uchunguzi utakapo kamilika nani aliyekuwa anastaili kupewa zawadi hizo,
hivyo kwa mwaka huu tunaomba isijitokeze tena”
Hata hivyo Mlindoko alizitaja zawadi zitakazo tolewa
kwa wafanyakazi bora katika siku hiyo ya madhimisho ya sikukuu za Meimosi
mkoani humo ambapo katika sekta Binafsi zawadi ni shilingi 300,000,sekta ya
Umma shilingi 500,000 ,Migodi ya kati shilingi 500,000 , Migodi mikubwa ni
shilingi 1,000,000
Pia wadau hao walijadili mambo mbalimbali yatakayo fanikisha
kukamilisha sherehe hizo ambapo waliziingiza taasisi zingine zikiwemo za
kifedha ambazo hazikuwemo kwenye bajeti, huku kikitarajiwa kukusanywa kiasi cha
shilingi milioni 90.6 fedha ambayo itakusanywa kutoka kwa wadau hao ambazo
ndizo zitakazo fanikisha sikukuu hiyo.
0 Response to "WAAJIRI WATAKIWA KUACHA KUPOKEA RUSHWA KWA LENGO LA KUMPITISHA MFANYAKAZI BORA SIKU YA MEIMOSI"
Post a Comment