MADIWANI waliojiuzuru
nyasifa hiyo na kuamua kuondoka
katika chama cha CHADEMA ambao ni
Sebastiani Peter na Zacharia Mfuko wamejiunga rasmi na chama cha Mapinduzi (CCM) mbele ya katibu wa itikadi na uenezi
Nape Nnauye na uongozi wa mkoa wa chama hicho.
Maelfu ya wakazi wa
mkoa wa Shinyanga wakihudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
Mahakama Nguzo nane huku
wakishuhudia waliokuwa wananchama na
viongozi ndani ya Chadema wakipanda jukwaani ghafla huku wakiwa wamevaa kofia za
CCM na kueleza kiliwafanya kujiunga na chama hicho kutokana na kutuhumiwa kila kukicha kuwa ni
mamluki ndani ya Chadema.
Madiwani hao walisema kwa nyakati tofauti huku wakiwa
wamepanda katika jukwaa na kuwaeleza
wananchi kuwa wasione ajabu kuwa ndani
ya CCM kwani wamekuwa wakituhumiwa kutumika na chama hicho pale wanapofanya
vizuri na kupinga yasiyo halali hivyo hawawezi kuwa na chama ambacho hakina
utaratibu na utovu wa nidhamu.
“Wananchi wa kata yangu ni mashuhuda walinichagua masikini
sina hata uwanja na sasa nimeamua kuondoka ndani ya chadema, ni miongoni mwa madiwani manispaa nilofanya
vizuri kwa kutekeleza ahadi yangu,naondoka
yanabaki majungu kuwa nimenunuliwa lakini ningejiunga na chadema natoka CCM wangeniita komando wanayoyasema hayo wote ni mbumbu wa mawazo”alisema diwani aliyejiuzuru chadema kutoka kata ya Ngokolo Peter.
Diwani wa kata ya Masekelo
Mfuko alisema kuwa mara baada ya kutoa taarifa katika vyombo vya
habari amekuwa akipata ujumbe katika
simu yake ya mkononi ya vitisho huku
akidaiwa kupewa fedha na chama cha mapinduzi jambo ambalo linamshangaza kwani kila mmoja
anauhuru wa kuamua aende chama gani
kitakacho mfaa.
Naye Nape Nnauye katika mkutano huo aliwapokea kwa shangwe wanachama hao kwa kuwapatia kadi za CCM huku akisema kuwa vijana wanatakiwa
wasifukuzwe katika vyama kwani ndio
nguzo inayofanya kuwepo kwa mabadiliko nchini,akitolea mfano wa Mh Zitto Kabwe
aliingia chadema akiwa na umri wa miaka
16 lakini sasa wanamwita msaliti ingawa
ameitengeneza chama hicho na kusimama imara.
Hata hivyo madiwani hao
wawili ambao wanatoka katika kata za Masekelo na Ngokolo walijiuzuru ndani
ya wiki hii huku wakitoa sababu
mbalimbli za kutofurahishwa na mienendo mibaya ndani ya chadema kwa viongozi wa kitaifa kuwadhalilisha viongozi wa mkoani Shinyanga huku wakiacha
kutekeleza waliokuwa wakiyaahidi.
0 Response to "MADIWANI WALIOJIUZURU NA KUJIVUA UANACHAMA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM MKOANI SHINYANGA"
Post a Comment