SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) katika mikoa ya simiyu
na shinyanga limewaonya wale wote
watakao haribu miundo mbinu ya shirika hilo
wakiwemo vishoka ambao wamekuwa
wakililetea shirika hasara kubwa kwa
kuharibu mita na kufanya gharama za uzalishaji na uendeshaji kuwa kubwa hivyo
watakao bainika kwa uhalibifu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hayo yalibainishwa mjini shinyanga kwenye mkutano wa hadhara
na Afisa mkuu wa huduma kwa wateja TANESCO katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga
Musa Kasimu wakati akitoa elimu kwa wakazi wa mjini humo juu ya huduma
zinazotolewa na shirika la TANESCO kwa wananchi
Kasimu alisema baadhi ya wananchi katika mikoa hiyo
miwili wamekuwa na tabia ya kuharibu miundo mbinu ya shirika hilo huku wengine
wakishirikiana na vishoka kuharibu vifaa hivyo hasa kwa upande wa Meter na Luku
ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikichokonolewa kwa lengo la kupunguza gharama
za umeme
Alisema vitendo hivyo vinafaa kukemewa kwa nguvu zote kwani
kufanya hivyo ni kuhujumu miundombinu ya shirika hilo na uchumi wa nchi ikiwa
ni pamoja na kusababisha hitilafu katika vifaa hivyo vya umeme “METER” NA
“LUKU” hali ambayo husababisha kuongezeka kwa bili za umeme tofauti na
matumizi.
Naye Afisa uhusiano wa shirika hilo katika mikoa ya
shinyanga na Simiyu Amosi Michael alikiri kuwepo kwa baadhi ya vishoka
kutoka ndani ya shirika hilo mara baada ya kuulizwa ni watu gani ambao wamekuwa
wakishirikiana na baadhi ya wateja
kuharibu miundombinu kwa lengo la
kukwepa gharama.
‘Nikweli kuna baadhi ya vishoka wanatoka ndani ya shirika
letu kushiriki na wananchi kufanya shughuli za kuharibu miundo mbinu ,kwani mtu
anayefanya kazi hiyo lazima awe na ujuzi na tunapo wabaini kuhusika na vitendo
hivyo tunawafukuza kazi ,na upande wa wananchi tunawatoza faini lakini katika
kipindi hiki ni mahakamani tu” alieleza Michael
Afisa usalama
washirika la TANESCO kutoka mikoa hiyo miwili Kenedi Peter aliwataka wakulima
wa mikoa hiyo ya Shinyanga na Simiyu kuacha tabia ya kulima mazao karibu na
nguzo za umeme kitendo ambacho husababisha nguzo kuanguka na kutokea
katizo la umeme kutokana na kufanya marekebisho ya nguzo hizo.
Pia alisema Shirika hilo hivi karibuni limetoa elimu
mkoani Simiyu katika vijiji 15 kutoka katika wilaya za Meatu, Maswa ,Bariadi,
na Itilima huku katika mkoa wa Shinyanga elimu hiyo ikitolewa katika vijiji vya
Salawe, miganha pamoja na mjini shinyanga
0 Response to "TANESCO MIKOA YA SIMIYU NA SHINYANGA YAWAONYA VISHOKA WANAOHARIBU MIUNDOMBINU"
Post a Comment