MADIWANI wawili wa chama cha maendeleo chadema wametamka rasmi kujiuzuru nyasifa hiyo
kutokana na madai ya uongozi ngazi ya taifa kuendelea kusikiliza
majungu,kudhalilisha baadhi ya viongozi pamoja na kuwaita
wahaini au wasaliti katika chama bila kuchambua ukweli na
kutotekeleza waliyoyaahidi kwa wanachama wao.
Madiwani hao ni Sebastiani Peter kutoka kata ya
Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo kwa pamoja jana waliongea na
waandishi wa habari katika ofisi ya naibu meya wa manispaa hiyo huku wakieleza
kuwa wanayatamka rasmi maneno mbalimbali yaliyopelekea kujiuzuru
kama inshara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa kitaifa
kwa nyakati tofauti.
Ambapo diwani Sebastiani alisema kuwa kuna sababu tatu
zilizopelekea yeye kujiuzuru nafasi ya udiwani na ukatibu wa mbunge vita
maalumu , ya kwanza ni mwezi Novemba mwaka 2013 kikundi cha Briged
kiliweza kuandika barua kwa katibu mkuu wa chama hicho taifa na kulenga
kuwadhalilisha viongozi akiwemo katibu mkoa na wilaya kuwa
wamehongwa kiasi cha shilling millioni 90.
“Tuhuma hii leo ninaamini ni tuhuma ya uongo
iliyolenga kuwadhalilisha viongozi ambao ni Nyangaki Shilungusheila katibu
wa mkoa na Siri yasini mwenyekiti wa wilaya ambapo kimsingi ndio
walipotufikisha hapa tulipo,kitendo cha katibu mkuu wa chama
kupokea barua hiyo na kushindwa kuifanyia kazi wakati viongozi hawa
wamewahi kufungiwa hata kwenye mkutano mkuu wa wilaya jambo hili
limenifanya niamini nyumba ya red brigedia wapo viongozi wa
kitaifa wanaowaagiza kufanya hayo”alisema diwani Sebastiani Peter.
Alisema jambo la pili ni kutokana na ahadi za mwenyekiti wa
taifa Freeman Mbowe kuahihdi chama kitamaliza kujenga nyumba ya marehemu
Shelembi aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini na diwani kata
ya Masekelo ambapo ahadi aliitoa siku ya mwisho kwenye mazishi ya
kiongozi huyo katika viwanja vya shy-com huku mwenyekiti huyo katika kikao
kingine alichokuwa akikiongoza kupinga ujenzi wa nyumba hiyo.
Jambo la tatu alisema kuwa tabia ya iliyozuka ndani ya chama
hicho ni kuwaita baadhi ya wanachama na viongozi ikiwa ni pamoja
kuwadhalilisha kwa kuwabatiza majina mbalimbali ya wasaliti au wahaini wa
chama ,waasisi wa kauli hizo ni viongozi hawa wa kitaifa kitendo
kinachomfanya aamini kuwa ni uongo ambao hauna tija katika chama.
“Mimi ni miongoni mwa wanachama nitakao kuwa wa mwisho
kuamini kama kweli mh Zitto Kabwe ,Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na
wengine ni wasaliti ndani ya chama hiki binafsi najiuliza kama kweli
Zitto ni msaliti wa chama na kwa mujibu wa taarifa ya chama
zinasema kuwa kutoka mwaka 2008 hadi 2009 aligundulika na kutumiwa na chama cha
Mapinduzi (CCM) swali mbona mwaka 2010 waliwezaje kumruhusu
kugombea ubunge katika jimbo la Kigoma Kasikazini ?”alisema Sebastian Peter.
Alisema kwa hiari yake kulingana na hayo
aliyoyapima ndani ya kichwa chake ameona kuna umuhimu wa kujiuzuru nafasi
ya udiwani na ukatibu wa mbunge ikiwa ni njia ya kuwafundisha
viongozi namna bora ya kuwajibika kuliko kujionesha mbele ya
wananchi kwa mavazi ya kondoo wakati ndani ya mioyo ni mbwa mwitupia sijawa na
mpango wa kujiunga na chama chochote nitabaki kuwa katika chama hicho.
Naye diwani wa kata ya Masekelo Zacharia mfuko
aliungana na diwani huyo kwa maelezo yake huku akisema kuwa uamuzi wake mpaka
kujiuzulu ni kutokana na kuwepo ubabaisha ji ndani ya chama hicho
kwani lilikuwepo sakata la mweyekiti wa mtaa kukigawa
kiwanja huku kukiwa na kamati ya ugawaji alipokieleza chama walidai
kukishughulikia lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea na uongozi wa
chama wamekaa kimya ikiwa kimeonekana dhahiri kupingana na sera ya chama
hicho kwa kuwatetea wanyonge.
Wote kwa pamoja walikabidhi barua zao za kujiudhuru
udiwani katika ofisi za manispaa huku wakimueleza kaimu mkurugenzi
Mwanamsiu Dossi taarifa juu ya uamuzi waliouchukua,kuwaombea
radhi kama sehemu waliokwaruzana na watendaji wote waliokuwa wakifanya
nao kazi kwa pamoja ambapo waliwataka wananchi wa kata zote kuwaona
kuwa kitendo walichokifanya sio kwa nia mbaya bali kulijenga taifa lililo
makini.
0 Response to "MADIWANI WA CHADEMA MANISPAA YA SHINYANGA WAJIUZURU NYASIFA HIZO"
Post a Comment