Ambapo mara baada ya kumalizika ufunguzi wa kusikiliza kesi hizo mahakama ilianza kwa kuangalia upande wa mtuhumiwa Mbula Mako aliyekuwa mganga wa kienyeji kufanya mauaji dhidi ya kikongwe Buguta Mashilima huko katika kijiji cha Nobora wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kesi hiyo iliendeshwa na jaji Haruna Songoro huku akisema kuwa mkoa wa Shinyanga na Simiyu unakesi nyingi ambapo jumla ya kesi 11 za mauaji zitasikilizwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Katika ufunguzi uliozinduliwa na jaji Songoro kwa kusikiliza kesi za mauaji mbalimbali Siku ya kwanza ya kuendesha kikao kulifanyika usikilizwaji wa kesi moja ya mauaji yaliodaiwa kutokea kwa imani potofu za ushirikina.
Kwa upande wa mashitaka mtuhumiwa alitenda mauaji hayo mnamo novemba 21 ,2011 kijiji cha nobora bariadi majira ya usiku baada ya kumtumbikiza kisimani marehemu ambaye alikuwa bibi yake.
Hata hivyo changamoto kubwa katika mahakama ya mkoa wa Shinyanga imedaiwa kuwepo mrundikano wa kesi mbalimbali zikiwemo za mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina ambazo hazijasikilizwa na kutolewa hukumu.
Naye hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John Meseka Chaba ameiomba serikali hapa nchini kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama kuu kanda ya ziwa linalojengwa mkoani hapa ilikurahisisha uendeshaji wa kesi hali ambayo itasaidia kesi nyingi kusikilzwa kwa wakati
“Endapo jengo la mahakama ya Rufaa kanda ya ziwa mkoani hapa litakapokamilika litasaidia kuepusha mrundikano wa kesi mahakamani kwani kesi nyingi hupangiwa tarehe kila mara kutokana na uhaba wa majengo ya mahakama kuendeshea kesi hizo pamoja na upungufu wa mahakimu kwani kesi nyingine zinakuwa hazijamaliza upelelezi”alisema Chaba
0 Response to "MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YAANZA KUSIKILIZA KESI ZA MAUAJI MKOANI SHINYANGA NA SIMIYU."
Post a Comment