KITENDO
cha vijana kutokujitambua kumesababisha
washindwe kushiriki kikamilifu katika mchakato
wa kutoa mawazo yao kuhusu rasmu ya katiba mpya.
Hayo yalielezwa na Mkurungenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali inayotetea haki za
wanawake na watoto wenye maambukizi ya
virusi vinavyosababisha Ukimwi
(AGAPE) John Myolla
katika ufunguzi wa kongamano la vijana kujadili rasmu ya
katiba mpya lililofanyika mjini hapa
jana.
Myolla alisema kundi
la vijana lina umuhimu wa pekee kwa jamii, lakini wameshindwa kujitambua na kujikuta wakijishughulisha na mambo ya
mzaha na kupuuza yale yenye
kuleta tija kwa taifa.
Alisema idadi kubwa ya vijana haikujitokeza kushiriki katika
mikutano ya kujadili na kutoa mapendekezo yao na kueleza wangelipenda katiba mpya itaje mambo yapi yatakayowasaidia vijana
nchini.
“Vijana wengi nchini hawakujitokeza
kwenye mikutano ya kujadili rasmu ya
katiba mpya kwa kisingizio cha kukosa nafasi ya
kwenda kushiriki katika mikutano hiyo na badala yake walikwenda kwenye viwanja
vya michezo na kumbi za Mziki”
alisema Myolla.
Alisema kuwa ukitaka kupima ushiriki wa vijana katika
mikutano ya kujadili rasmu ya katiba mpya tazama rasmu ya katiba sura ya nne
sehemu ya kwanza ya Ibara ya 44 inayozungumzia haki na wajibu wa vijana
zimeandikwa senteso mbili pekee hiyo ni
kudhihirisha kuwa vijana hawakutoa mapendekezo yao katiba mpya iwe ya ainagani.
Naye kijana Nyangata Sungura mkazi wa kitongoji cha Ndala,
Manispaa ya Shinyanga alisema vijana hawapaswi
kuilalamikia serikali kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kutokana na kupuuza mipango
muhimu.
Kwa upande wake mwezeshaji na mtoa mada wa kujitolea kutoka
katika Shirika lisilo la kiserikali la Restless
Develoment (RDT) John Eddy alisema licha ya vijana kushindwa kutoa
mawazo yao kuhusu rasmu ya katiba mpya,
hata hivyo aliwashauri kuisoma
rasmu ya katiba mpya kwa lengo la
kubaini maeneo yalio na upungufu na kutoa mawazo yao yanayohusu kupata
katiba inayokidhi haja.
0 Response to "VIJANA KUTOJITAMBUA WAMESHINDWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MCHAKATO WA KUTOA MAWAZO YAO RASMU YA KATIBA MPYA"
Post a Comment