IDARA ya uhamiaji mkoani Shinyanga inakabiliwa changamoto wa vitendea kazi kwa kukosa magari ya
kutosha ,kutokuwa na sare maalumu zinazoendana na mazingira ambazo zinaweza
kuhimili mazingira ya kikazi na hivyo kushindwa kufanya kazi yao ipasavyo ya
kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingi
Hayo yalibainishwa na mtumishi wa Idara ya uhamiaji mkoani humo
Herieti Mayunga wakati akisoma Risala kwa mgeni Rasmi katika sherehe ya kuuaga mwaka
2013 na kuukalibisha mwaka 2014 iliyofanyika mjini shinyanga na kuhusisha wakuu
wa idara ya uhamiaji kutoka mikoa ya Geita,Mwanza, simiyu pamoja na Mara.
Herieti alisema licha ya
upungufu wa vitendea kazi hivyo , pia idara hiyo inakabiliwa na changamoto
mbalimbali likiwemo suala la uhaba wa watumishi ambapo idara hiyo kwa mkoa
mzima inawatumishi 33, pamoja na kukosa ushirikiano wa kutosha kwa wananchi wa
kuwafichua wahamiaji hao haramu
Naye Afisa uhamiaji mkoa
wa shinyanga AnnaMaria Yondani aliwataja wahamiaji haramu waliokamatwa mkoani
humo, na wanaoishi kinyume na sheria kuanzia kipindi cha Januari hadi Desemba
mwaka jana ni wahamiaji 162, walioondoka kwa OD 19, PI 75 ,
waliofungwa 30, waliochiwa huru na kuambiwa kufuata taratibu za nchi 32 na kesi
zinazoendelea 6.
Pia alitaja sababu
zinazochangia kuongezeka kwa wahamiaji haramu mkoani humo ni kutokana na uwepo
wa migodi ya madini ya Dhahabu , Almasi, kilimo cha Pamba, Tumbaku, pamoja na
Barabara kuu iendayo Rwanda, Burundi, Uganda, Kongo DRC, hali ambayo
husababisha ongezeko la watu wengi hasa katika wilaya ya kahama ambayo imekuwa
ikikithili kwa wahamiaji hao.
Kwa upande wake mgeni
Rasmi mkuu wa mkoa shinyanga Ally Rufunga aliahidi suala la upungufu wa
vitendeakazi atalifikisha katika ngazi ya taifa kwani hilo lipo nje ya uwezo
wake huku akiwataka watumishi wa Idara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia misingi
ya sheria na taratibu za nchi pamoja na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
‘’Idara ya uhamiaji huwa
inakabiliwa na rushwa , hasa pale mnapo wakamata wahamiaji haramu kutoka sehemu
mbalimbali wakiwemo wa Somali wamekuwa wakiwapa fedha na kuwa achia waendelee
na shughuliza zao, hivyo na toa onyo kwenu atakaye bainika kuhusika na vitendo
vya rushwa sheria itachukua mkondo wake” alisema Rufunga.
Akizungumza katika
sherehe hiyo Afisa uhamiaji mkoa wa Mwanza Remegius Pesambili alitoa ushauri
kwa Idara ya uhamiaji licha ya mapungu waliyonayo bali
washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuhakikisha wanatokomeza au
kupunguza wahamiaji haramu mkoani humo.
Alisema wahamiaji hao
wanapokithiri hapa nchini huweza kusababisha kuwepo kwa matukio ya kigaidi
kwani asilimia kubwa ya matukio hayo hutokana na watu kutoka nchi za jirani.
0 Response to "IDARA YA UHAMIAJI MKOANI SHINYANGA INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI."
Post a Comment