KUMOMONYOKA kwa maadili kwa baadhi ya watumishi wa
umma ni moja ya sababu zinazochangia kukithiri kwa vitendo
vya rushwa na kuchangia kuongezeka uchakachuaji wa miradi ya
maendeleo, unaofanywa na wakandarasi kwa kushirikiana na
wataalamu nakuwataka wanaofanya vitendo hivyo kujitathimini
wenyewe kuachia ngazi zao kabla ya kuwajibishwa.
Hayo yalielezwa jana na kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU )mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono, kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo,ambapo alisema viongozi na mamlaka husika zikiwa zimekaa kimya bila kuchukuwa hatua hali ambayoinatoa picha kuwa watawala hao ni waoga
wakushiriki katika vita dhidi ya rushwa.
Alisema katika kukabiliana mapambano ya tatizo la rushwa
kuna changamoto ambazo ni kikwazo ukiwemo mtazamo
potofu wa baadhi ya wanajamii kuwaona wanaojihusisha na
vitendo vya rushwa na wahujumu uchumi kama mashujaa,ushahidi
kukosekana,ushirikiano hafifu toka katika baadhi ya taasisi
hasa zinapokuwa zinachunguzwa pamoja na ukosefu wa fedha
hususani kwenye uchunguzi na uendeshaji kesi kubwa .
Ni vema watumishi wa umma wakajitathimini wao wenyewe
uhalali wao wa kuendelea kuwepo katika nafasi walizonazo
wakati wanashindwa kupambana na rushwa,hivi sasa mkoa wa
Shinyanga katika kipindi cha januari hadi Desemba 2013 ni
kesi 15 zilipatikana kati ya hizo idara ya afya ni
tisa,elimu tatu na halmashauri tatu zilizolenga
Tasaf”alisem.
Akizungumza kwenye kikao hicho waziri wa nchi, ofisi ya rais
utawala bora Kapten mstaafu George Mkuchika,alisema
iwapo kila moja atazingatia maadili ni wazi hata vitendo vya
rushwa vitapungua tofauti na hali ilivyosasa rushwa
imekithiri na kuwaathiri zaidi wananchi masikini ambao
hawana kipato hasa wanapohitaji kupata huduma ya
matibabu,dhamana,elimu na kufuatilia mafao.
Alisema rushwa ndogo ambayo inawalenga zaidi watumishi wa
ngazi za chini hasa wakati wa kutoa huduma, inawatesa
wananchi maeneo mengi na kufikia hatua ya kuichukia serikali
iliyokomadarakani kwa kushindwa kupata huduma,na kutolea
mfano wa rushwa kubwa ambayo inaleta athari kubwa kiuchumi
kutokana na uroho ,tama na ubinafsi wa kujilimbikizia mali
kwa haraka.
Waziri mkuchika alisema utawala bora ukiwepo matatizo hayo
hayatakuwepo,ambapo uliutaka mkoa wa Shinyanga kuachana na
imani potofu za kishirikina zakuuwa vikongwe na albino hali
hiyo inatokana na ukosefu wa elimu na hofu ya mungu,na
kwamba mtu anapozeeka anatakiwa kupongezwa na kupewa zawadi
na siyo kumkata mapanga kwa kumtuhumu kuwa mchawi.
Awali mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga akimkaribisha
waziri,alitoa wito kwa watumishi wa umma na wananchi kwa
ujumla kujiunga na bima ya maisha ambayo itawasaidia
baadaye,na kusisitiza umuhimu wa kupanda miti ili kuhifadhi
vyanzo vya maji visitoweke na wananchi kukosa huduma ya
maji. Shinyanga
0 Response to "KUMOMONYOKA KWA MAADILI KUMEFANYA VITENDO VYA RUSHWA KUSHAMIRI NA KUCHAKACHUA MIRADI"
Post a Comment